Mwanajeshi amdharirisha mwanamke Kigamboni feri!!!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,027
Reaction score
20,516
Katika hali nisioiamini machoni pangu asubuhi hii,mwanajeshi wa jwtz aliyekuwa akiongoza magari kuingia kwenye pantoni amezua hofu baada ya kumtandika vibao na kumkwinda mwanamama ambaye ni sawa na mama yake mzazi! Tukio hilo lilinifanya kujifanya mwandishi wa habari nikajitosa kutaka kujua kuliko lakini ilikuwa ngumu kumhoji au kumpiga picha yule kija wa jwtz kuwa aligeuka na kuwa mbogo! Nikaamua kumfuata yule mama ndani ya pantoni lakini nilishangaa baada ya mama huyo kuniambia kuwa nae ni afande! Akanipa masharti ya kutompiga picha! Akasema amemweleza kuwa yeye ni askari mwenzie lakini yule kijana hakumwelewa,"unajua mwanangu askari huwa tunatumia geti lile sasa nashangaa yule kijana namuonyesha kitambulisho lakini hajanielewa nadhani analake jambo hawa vijana walioingia siku hizi wanaweuka na ujeshi" Ndugu wanajamvi je sheria zipoje juu ya udharirishaji huu?
 
Kama na yeye ni Mjeshi wangezichapa ili waheshimiane.
 
wanajeshi siku zote kwao huwa hamna sheria..! huyo mama ni vile tu labda alikua hana nguvu, lakini ili kuonesha kama na yeye ni afande wangezichapa tu..angempa kofi la nguvu,potelea mbali kitakachofuata mbele kwa mbele!
 
Angekuwa raia kungekuwa na cha kusema.
 
wanajeshi siku zote kwao huwa hamna sheria..! huyo mama ni vile tu labda alikua hana nguvu, lakini ili kuonesha kama na yeye ni afande wangezichapa tu..angempa kofi la nguvu,potelea mbali kitakachofuata mbele kwa mbele!

Yeye kwa maneno yake amesema lazima amuonye kazi popote pale alipo! Anasema anakwenda kutafakari nin cha kumfanyia huyo bw mdogo!
 
wanajeshi wanavisa sana,sina hamu nao
nahisi wako juu ya sheria ati!!wajeuri sana
 
si wanajidai mwenzao ndo yuko pale magogoni...mtawafanya nini kwani???
 
Mbali na huyo Mama Mwanajeshi,pia kuna raia wengi wanadhulumiwa,wanadhalilishwa na hata kujeruhiwa na wanajeshi wasiojiheshimu wala kujali utawala bora! Nadhani ni wakati muafaka vyombo vyote vya haki za binadamu kutoa msaada wa kisheria ili kukomesha ufedhuli wa wanajeshi wachache wanaowafedhehesha raia wema!
 
Tatizo hilo sio dogo kama mnavyo fikiria, kama huyo kijana angemsababishia maumivu au kilema kwa kitendo hicho tungesema ahaah wajeshi wako juu ya sheria bwana tuwaache tu, Kwa wenzetu huo ndo mwanzo wa maandamano, Civil war nk.
 
Ukweli ni kwamba hawa jamaa wanajisahau sana, hakuna mtu alie juu ya sheria na wao wanajua hivyo sema wanajua hakuna hatua iliyowahi kuchukuliwa juu ya wanaofanya vitendo kama hivi. Boss wao Mwamunyange ameshasema mara nyingi tu kujana mpumbavu kama huyu akiripotiwa anafutwa kazi.
Nadhani ni wakati muafaka sasa jamii ikaamka na kukataa vitendo kama hivi. Tuanze kuvichukia tangu mioyoni na tuchukue hatua. Hapo asubuhi kama wananchi mngeungana kwanza kumwambia kuwa anafanya kosa kisha mngemkamata kumpeleka sehemu husika siku nyingine yeye au mwenzake angejiuliza kabla ya kufanya hivi.
Nachukia sana vitendo vya miaskari mijinga kama hii, kama anajiona shupavu si angezuia mabomu yasilipuke Gongolamboto huko
 
Nchi hii ni mashaka katika majeshi yote, ukienda Uhamiaji wanataka RUSHWA! Polisi Usiseme kwa Rushwa tena wameacha kutulinda mitaani wamekuja na POLISI JAMII, Magereza nako Rushwa, JWTZ ni kutoa vipigo kwa raia!
 
wanajeshi waliokamilika wana w tatu yaani www meaning war,wine,women.cc wakwetu wanakosa w ya kwanza, hivo wamejielekeza kwenye w mbili za mwisho... wahajiona sana hawa jamaa.... cjui tuwapeleke wengine libya?
 
Ni pole zao hao, wanajeshi wanatumia nguvu kuliko akili. Mazoezi wanayofanya ni ya kinyama, hawawezi kuwa na roho nzuri labda Yesu ashuke ndani yao.

God have Mercy!
 
Kurusha kombora(guided missile) , kurusha ndege, kuongoza ndege, kulinda anga(radar surveillance),electronic warfare na submarire hunting from surface, air and underwater unatumia nguvu? Akili inatumika ila basi tu some of my fellows are out of their minds.
 
Katika hali nisioiamini machoni pangu asubuhi hii,mwanajeshi wa jwtz aliyekuwa akiongoza magari kuingia kwenye pantoni amezua hofu baada ya kumtandika vibao na kumkwinda mwanamama ambaye ni sawa na mama yake mzazi! Tukio hilo lilinifanya kujifanya mwandishi wa habari nikajitosa kutaka kujua kuliko lakini ilikuwa ngumu kumhoji au kumpiga picha yule kija wa jwtz kuwa aligeuka na kuwa mbogo! Nikaamua kumfuata yule mama ndani ya pantoni lakini nilishangaa baada ya mama huyo kuniambia kuwa nae ni afande! Akanipa masharti ya kutompiga picha! Akasema amemweleza kuwa yeye ni askari mwenzie lakini yule kijana hakumwelewa,"unajua mwanangu askari huwa tunatumia geti lile sasa nashangaa yule kijana namuonyesha kitambulisho lakini hajanielewa nadhani analake jambo hawa vijana walioingia siku hizi wanaweuka na ujeshi" Ndugu wanajamvi je sheria zipoje juu ya udharirishaji huu?

Tatizo ni kwamba wanajeshi na polisi wanataka wawe wanavuka bure yani Tshs.100/= kuitoa wanaona tabu. Hivi nani aliyewaruhusu wawe wanapita bure? si na wao ni watumishi wanamishahara kama wengine? wananikera sana kwa kweli hata mpirani wanataka waingie bure
 
Back
Top Bottom