'Mwanajeshi' aliyepiga Picha na Lema Mbaroni

'Mwanajeshi' aliyepiga Picha na Lema Mbaroni

Mbona mafisadi wanayatetea badala ya kuyakamata? Au kwa kuwa policcm ni kitu kimoja na mafisadi?
Yule mtu aliyedaiwa kuwa ni mwanajeshi wa JWTZ wa kikosi cha monduli emetiwa mbaroni leo kwa ushirikiano wa jeshi la wananchi na Police. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kijana huyu hakuwa mwanajeshi wa JWZ kama alivyojitambulisha kwa waandishi wa habari ila aliwahi kuwa JKT na akaacha, ila amekuwa akivaa ngua hizo za jeshi kwa miaka mingi na wananchi wa melerani wanamtambua kama mwanajeshi. Maswali ya kujiuliza inakuwaje raia anavaa nguo za jeshi kwa miaka mingi bila kuchukuliwa hatua, hayo mavavi kayapata wapi? Je Lema asingepiga picha naye angejulikanaje kuwa ni raia anavaa nguo za jeshi na kujitambulisha kama mwanajeshi???
 
Hivi yule kichaa(mkenya) aliyemteka Ulimboka ameishia wapi?
 
Ndio maana niliwaambia kuwa swala la kumpata dogo ni rahisi sana. Sasa amepatikana, ngoja atoe majibu ya malengo yake then hatua muafaka zifuate.
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha
ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha! Mkuu hebu badili kwanza title ya
habari...
ha ha ha hii hatari mpaka nimepaliwa du atiwa m boroni, mods saidien kurekebisha.
 
Kaka nikweli
nimepata taarifa toka kwa raia wa Melerani muda si mrefu walinipigia
simu kwakuwa nilikuwa nafuatilia na kwenye huo mkutano
nilikuwepo

Only in Tanzania. Huyo 'mwanajeshi' fast tu amekamatwa, lakini wezi wa EPA, wenye ela nje na mafisadi wa hapa mjini (mfano Jeetu Patel, baba yake wa kambo Nape), inakuwa ngumu kuwakamata au kuwachukulia hatua. Wanyarwanda waliojaa hapa town for special mission hawakamatwi, kweli hii ndo bongo...
 
Naomba kuuliza mbona nchi za wenzetu mfano Itali spain Urusi raia wao wanasafiri wakiwa wamezivaa nguo zinazo fanana na sare za jeshi lao iweje huku kwetu imekuwa ni makosa kuvaa au kubeba kitu chenye rangi ya jeshi?
 
Moderator tunaomba ubadili kichwa cha habari hiki, maana sasa watu wanajadili mambo mengine kabisa kwa typo error iliyoko kwenye kicha cha habari cha uzi huu.
 
Aliyepiga picha na Lema kasakwa mpaka kakamatwa, wale polisi walioua raia wenyewe hapana kukamatwa. Tanzania ni zaidi ya kuijuavyo.
 
hivi walioiba 150m kariakoo wamekamatwa?picha tuu inawanyima usingizi!majambazi yanapeta
 
Wandugu mniwie radhi kwa tittle nilimaanisha ametiwa Mbaroni, najribu kuedit inagoma, naomba mod anisaidie! Ila habari ni ya kweli nimepewa na afande mmoja wa jeshi la police wa huko melerani!
 
Hao wanaojiita inteligensia mbona hawakumkamata siku zote?Haya yote ni usanii mtupu.Mungu atufikishe 2015 salama.
Yule mtu aliyedaiwa kuwa ni mwanajeshi wa JWTZ wa kikosi cha monduli emetiwa mbaroni leo kwa ushirikiano wa jeshi la wananchi na Police. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kijana huyu hakuwa mwanajeshi wa JWTZ kama alivyojitambulisha kwa waandishi wa habari ila aliwahi kuwa JKT na akaacha, ila amekuwa akivaa ngua hizo za jeshi kwa miaka mingi na wananchi wa melerani wanamtambua kama mwanajeshi. Maswali ya kujiuliza inakuwaje raia anavaa nguo za jeshi kwa miaka mingi bila kuchukuliwa hatua, hayo mavazi kayapata wapi? Je Lema asingepiga picha naye angejulikanaje kuwa ni raia anavaa nguo za jeshi na kujitambulisha kama mwanajeshi???
 
Wandugu mniwie radhi kwa tittle nilimaanisha ametiwa Mbaroni, najribu kuedit inagoma, naomba mod anisaidie! Ila habari ni ya kweli nimepewa na afande mmoja wa jeshi la police wa huko melerani!

baada ya kubonyeza edit hapo chini yake pembeni ya save bonyeza go advanced then baada ya kuedit title yako juu yake utakutana na kibox hapo kinasema reason for editing andika typing error then save changes itakubali
 
Back
Top Bottom