Mwanahamisi Singano: Ndoa hazina maana tena

Mwanahamisi Singano: Ndoa hazina maana tena

Unayosema ni kweli ila bado ndoa ni muhimu. Kwasababu, kuna amani mtu anapokuwa na mahusiano na mtu mmoja, anakuwa na uhakika kuwa yuko nae kila siku wataishi pamoja miaka yote. Talaka zipo ila binadamu kaumbwa kuwa na mazoea ya kutaka kuishi na mtu maishani mwake

Halafu kuhusu mali, hilo ni Suala la elimu tu, wanandoa wana haki ya kumiliki mali binafsi.

Kama umeamua kujenga nyumba yako peke yako jenga na sheria itatambua kuwa hiyo ni mali yako binafsi, maana kwenye talaka ni mali za wanandoa ndio hugawanywa sio mali za mtu mmoja.
Mtazamo huu ni kinyume cha misingi ya ndoa. Ni heri kutokuoa kuliko hivi. Huwezi kuwa na mali binafsi ndani ya ndoa, hilo ni nadharia tu, labda kama hamna kizazi. Hizi ni ndoa za mwendokasi
 
Ndoa hazijawahi, na wala hazitakuja kupitwa na wakati, mengine ni porojo tu. & This is fact.

Kama hazikufa SODOMA basi tena.
Asante mkuu. Misingi ya ndoa itabaki imara, wanadamu walioharibika akili ndio watajaribu kushambulia taasisi ya ndoa.
 
Mtoa mada haupo sahihi na upo kwaajili ya kuleta hofu na upotoshaji kwa wanandoa na wanaotarajia kuingia kwenye ndoa,jambo la msingi la kutambua sio kila mwanandoa anapitia unachokisema hapana maisha ya ndoa ni matamu changamoto za hapa na pale hazikosekani kikubwa wanandoa waishi kwa kupendana,kuheshimiana na kuepukana na tamaa ambazo hazina msingi hasa kuwa waaminifu kwa wenza wao.

Ndoa na ziheshimiwe hapa kuna ma single mother suala la kupata ndoa lilishindikana na wanawatoto tayari wanabaki kutoa maneno ya kukashifu tu watambue kama huta kama hujabahatika kupata mume sio kesi fanya kazi kwa bidii tu maisha yatasonga na vijana ambao maisha bado hayajakaa sawa kiasi kwamba anawaza akioa atampa nini mwanamke aliyemuoa ajipe muda saizi ale ugali wa shemeji yake kwanza.
 
Mtazamo huu ni kinyume cha misingi ya ndoa. Ni heri kutokuoa kuliko hivi. Huwezi kuwa na mali binafsi ndani ya ndoa, hilo ni nadharia tu, labda kama hamna kizazi. Hizi ni ndoa za mwendokasi
Suala la kuwa na mali binafsi lipo tena kisheria na hata kidini, kwa sheria za kiislamu ni jambo linalokubalika kwa mke ama mume kuwa na mali zake binafsi, linakubalika kabisa kuanzia kidini hadi kisheria za kidunia ni vile tu watu hawaangalii hilo kuwa kuwa kwenye ndoa sio lazima usiwe na mali zako binafsi
 
Wenye wake wengi wanaishi kwa raha? Migogoro ni kwa Wakristo pekee?
Kwaa uzoefu wangu mahakamani na mashauri ya ndoa kwa ujumla, Wakristo ndiyo wenye shida zaidi kwenye ndoa.

Yaani ugomvi wa ndoa ya Kikristo unakuwa mzito sana kulinganisha na upande wa pili
 
umenijibu kwa ustadi lakini kwa vile sisi wanaume tuna supremacy ndani yetu tuliyopewa na mungu na tunahtaji kumaintain ile status quo. bac nashauri kwenye ile knowledge is power wanawake wafundishwe pia kumheshimu mwanaume no matter ones degree or wealth. ndoa ni taasis yenye mamlaka, hatuwezi kumdharau rais wa nchi kwa vile yeye ni mr. na sis ni maprofesa lazma tutaumia..halaf jmn cmu yangu haiwez kumake paragraphs ndo mana nabananisha..nimshukuru alie edit andiko langu la kwanza.
Wanawake wapi wafundishwe? Wakati hayo mambo wanakutana nayo mtandaoni kila kukicha...watu wanawafollow hao feminist mpaka wanaume ndo hao wanakuja na story za kutunga daily ili mradi tu ndoa ichafuliwe hii kampeni ni ngumu mkuu kushinda hata inavyojengwa .Elimu imekuwa nayo Haina maana zaidi ya kuleta civilization za magharib huwezi kukuta nchi ya Korea Ina mambo ya kijinga kama haya coz wanashikilia tamaduni zao milele ....mwanamke akijua kingereza akapata kakazi TRA basi ni boss lady , pretty na cutie....mazingira ni magumu mno ndo dunia iyo hata wafundishwe watu walishachelewa
 
Wakati wew na wanasosholojia wako mkiandaa reforms kwa ajili ya ndoa, nakukumbusha tu kwamba kwa sisi waislam al maaruf kam wavaa kobadh kwa hapa jukwaani.

Sisi kwetu ndoa ni ibada yenye hadhi ya nusu ya dini, na kama ni ibada basi kitabu chetu kitukufu kimeshaelekeza taratibu za ibada zote.

Sasa kubadili sheria za kiibada ni sawa na kumchokoza alieziweka, na aliziweka akijua kuwa itakuja karne ya ishin na moja na alijua itakuwaje sas kwa vile anaifaham karne hii kama itampendeza atatoa maelekezo yeye mwenyewe ya kubadili au kumantain, manake sie tumekatazwa kupunguza wala kuongeza doctrines katika mambo ya kidini ikiwemo ndoa. So kwa niaba ya wavaa kobadh acces denied.

Me niseme tu kwa dhati kwamba ninyi wanawake wa kisomi mkijihic mmeota mapembe kwa taaluma za mlimani bas mna hiari ya kukataa kuolewa.

Mama na dada mliopo hapa: hakunaga viongozi wawili wanaolingana mamlaka sehemu moja, ni lazma mmoja awe juu na wa chini areceiv orders ama nyie elimu yenu inasema vp? Mnadanganywa na Marekani? Taasisi ni ileile ambae hataki akumbatie mto.

Tell them
Tell them
Waambie waelewe kua mke ni msaidizi wa mumewe
Hawezi kufanya,kuamua, au kufanya chochote bila ya mimi kufahamu

Ewe dada unaesoma andiko hili
Ukiona kichwan kwako umeweka neno 50/50 Basi elewa mambo yameshakushinda.
 
Unayosema ni kweli ila bado ndoa ni muhimu. Kwasababu, kuna amani mtu anapokuwa na mahusiano na mtu mmoja, anakuwa na uhakika kuwa yuko nae kila siku wataishi pamoja miaka yote. Talaka zipo ila binadamu kaumbwa kuwa na mazoea ya kutaka kuishi na mtu maishani mwake

Halafu kuhusu mali, hilo ni Suala la elimu tu, wanandoa wana haki ya kumiliki mali binafsi.

Kama umeamua kujenga nyumba yako peke yako jenga na sheria itatambua kuwa hiyo ni mali yako binafsi, maana kwenye talaka ni mali za wanandoa ndio hugawanywa sio mali za mtu mmoja.

Naomba kuuliza
Hivi mfano nkawa na nyumba yangu nkaowa mke kanikuta nayo
Ikkitokea mmeachana nyumba haihusiki kimgawanyo?
 
Andiko hili laweza kuonekana ni jema sana hasa katika zama hizi, lakini nasikitika kusema kuwa LIMEKWEPA KUONGELEA UKWELI wa matatizo ya ndoa, kisababishi chake. Ukitaka kujadili jambo lolote linalobadilika kutokana na wakati ni vema basi kukaangazia nini kilifanyika mwanzo, kumetokea mabadiliko yapi kwa sasa.

Bila hata kuandika makala ndefu zaidi, asili ya migongano kwenye ndoa ni FEMINISM. Fuatilia ukianzia sasa kurudi nyuma, utafikia pale wimbi la kwanza la feminism lilipoanza ndipo ndoa zilipoanza kugeuka jehanam.

Kuna program mbalimbali zilizokuja kwa jina la ukombozi wa mtoto wa kike, lakini tazama content zake, hizi zote zimechangia kuvuruga uhalisia wa ndoa. Kudhani kwamba ndoa zimebaki kwa wenye imani tu, ni kutoelewa kwamba msingi wa ndoa ni IMANI. Ni lazima mke amwamini mumewe na mume amwamini mkewe ndipo ndoa itakaa. Nje ya hapo hakuna ndoa.

Kujaribu kutafuta maana tofauti ya ndoa ni kujaribu kutengeneza kitu tofauti ambacho sio ndoa, mfano mwanamume kuoa mwanamume nk. Nitarudi baadaye kuchambua hii makala inayopotosha, hatua kwa hatua.
Nipo hapa kujifunza nimeanza kuelewa nilivhopitia hapa na kwakutumia akili zangu, safi sana mkuu aya umeandika yamenifikilisha nikapata kitu[emoji848]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Wanawake wapi wafundishwe? Wakati hayo mambo wanakutana nayo mtandaoni kila kukicha...watu wanawafollow hao feminist mpaka wanaume ndo hao wanakuja na story za kutunga daily ili mradi tu ndoa ichafuliwe hii kampeni ni ngumu mkuu kushinda hata inavyojengwa .Elimu imekuwa nayo Haina maana zaidi ya kuleta civilization za magharib huwezi kukuta nchi ya Korea Ina mambo ya kijinga kama haya coz wanashikilia tamaduni zao milele ....mwanamke akijua kingereza akapata kakazi TRA basi ni boss lady , pretty na cutie....mazingira ni magumu mno ndo dunia iyo hata wafundishwe watu walishachelewa
sawa kaka, basi watachagua kimoja kati ya kuw boss lady au kuolewa
 
Andiko hili laweza kuonekana ni jema sana hasa katika zama hizi, lakini nasikitika kusema kuwa LIMEKWEPA KUONGELEA UKWELI wa matatizo ya ndoa, kisababishi chake. Ukitaka kujadili jambo lolote linalobadilika kutokana na wakati ni vema basi kukaangazia nini kilifanyika mwanzo, kumetokea mabadiliko yapi kwa sasa.

Bila hata kuandika makala ndefu zaidi, asili ya migongano kwenye ndoa ni FEMINISM. Fuatilia ukianzia sasa kurudi nyuma, utafikia pale wimbi la kwanza la feminism lilipoanza ndipo ndoa zilipoanza kugeuka jehanam.

Kuna program mbalimbali zilizokuja kwa jina la ukombozi wa mtoto wa kike, lakini tazama content zake, hizi zote zimechangia kuvuruga uhalisia wa ndoa. Kudhani kwamba ndoa zimebaki kwa wenye imani tu, ni kutoelewa kwamba msingi wa ndoa ni IMANI. Ni lazima mke amwamini mumewe na mume amwamini mkewe ndipo ndoa itakaa. Nje ya hapo hakuna ndoa.

Kujaribu kutafuta maana tofauti ya ndoa ni kujaribu kutengeneza kitu tofauti ambacho sio ndoa, mfano mwanamume kuoa mwanamume nk. Nitarudi baadaye kuchambua hii makala inayopotosha, hatua kwa hatua.
absolutely yes ! tunasubiri makala
 
Acha uongo hakuna ndoa za kikafiri kama za waislam walahi ni wapumbavu sana wanaume tena ndio mpangwe weh no shida kubwa bora mtu anajua anamke mmoja

Maana ngoja nikupashe watu wakishapendana wakajuana vyema na kuwekeana mipaka ndoa itadumu muislamu gani amweshimu mkewe sindoto .
Walahi hawaeshimu wake zao wanawaweka kama products zao za madukani upendo zero , wao nimaonyesho tu mwislamu huwa anavisasi
Hakuna ndoa ya kikafiri mtoa mada labda kakosea kutaja ubaya wa ndoa upande wa wakristo tu ila kote Kuna matatizo inategemea na wenza wenyewe...Ndugu zangu walioa sijui ni malezi ila wameoa pwani ndo zao wengi mpaka miaka 11 wengi machalii miaka 5 sijawai kuona malumbano ila wakristo wengi hwana ndoa ...sina maana kwamba upande fulani ni mbaya hapana ni kwamba sehemu zote zinategemeana na wenza husika
.hakuna mwanamke anawekwa kama products wacha kukariri kutoka kwa mafenist maana hata wewe ukiolewa utahitaji kuhudumiwa !! So usiwe na mtazamo kisa umepata sehemu fulani ishu ni kwamba ndoa hazina tatizo ila binadamu ndo hawaeleweki
 
Hujasoma vizuri pwani hawaachwi kisa wanatoa kote kote tukifanya utafiti waweza kulia watoto wananajisiwa hadi mbaya yaani tena na baba zao waliowazaa na pia wanawake hawana usemi ndio maana ndoa zinadumu
 
Hyo ni propaganda ambayo ipo kichwani mwenu fanya utafiti utaona
 
Ameandika Mwanahamisi Singano.

Labda wewe ni mmoja wa wengi ambao baada tu ya kusoma kichwa cha habari na jina la mwandishi, tayari hasira zimekupanda. Pengine unasoma haya makala siyo kwa sababu ya kutaka kujua kilichoandikwa, bali unasoma ili upate cha kukosoa na kunidogosha. Nikuombe ushushe pumzi! Kuwa mpole kidogo, ni vizuri kwa afya yako.

Alright! Najua wajua kuwa mijadala ya migogoro ya ndoa na ongezeko la talaka imeshika hatamu, huku waliojibatiza utaalam wa ndoa wakiwa busy kutoa uchambuzi na masomo kwa wanandoa hasa wanawake, na serikali ikianza kuhamasisha midahalo ya ndoa.

Kwa baadhi yetu tunaona jambo hili linafanywa kuwa jipya ila si jipya. Labda ukubwa umeongezeka. Pengine watu wamekuwa wepesi kulizungumzia kuliko ilivyokuwa awali, lakini migogoro na kuvunjika kwa ndoa ilikuwepo na ipo.

Tuseme tu ukweli. Watu wanaumia kwenye ndoa jamani. Wanawake kwa wanaume.

Mpaka leo kuna familia kama mume mtarajiwa hana nyumba, hana gari, hana kazi nzuri, hawakubali aoe binti yao, hata kama wanapendana kiasi gani. Kaka zangu walio kwenye ndoa wanajua jinsi matarajio yalivyo makubwa. Kuwa mume bora ni kuwa na kipato kikubwa kuliko mume wa rafiki wa mke wako na kumpa mkeo, mashemeji na wakwe, kila wanachotaka hata kama hakipo kwenye uwezo wako.

Shida ya afya ya akili ni kubwa mno kwa ‘wakaka’. Hawasemi tu. Wanalazimika kufanya dili hatari. Wanaumizana kenye kutafuta kipato na ‘wanasnichiana’, ili mradi ‘makasiriko’ kama yote ili ndoa iende. Kimsingi, tumevurugwa.

Huku kwa dada zangu ndio mtume salale. Hakuliki wala hakulaliki. Tunastiriwa na make-up tu.

Ila kila mtu analia na lake. Huyu analia mume hana muda naye, kama hayuko safari kikazi, yuko baa na marafiki, akiuliza, anajibiwa, kwani umekosa nini? Yule analia mume hajigusi kwenye majukumu ya kifamilia kwa kuwa mke ana kipato kikubwa.

Mke hakumbuki mara ya mwisho lini mume kumnunulia hata upande wa kanga, achia mbali kulipa ada au kununua bidhaa za nyumbani. Na akifungua mdomo kumuuliza anaambulia kipigo au matusi, eti anataka kumpanda kichwani mume kwa kuwa yeye ana hela kuliko mume.

Shangazi yangu mie analia machozi yasiyokauka. Kuamua kwake kuukimbia upweke na kuogopa dhambi ya kuzini kukamfanya akubali kuolewa mke mdogo, sasa anafanywa mwizi wa penzi la Bi Mkubwa. Anajiona hana thamani na hastahili mapenzi wala faraja ya mume. Huo uadilifu unaosemwa haujui unafananaje.

2-1.jpg

Na jirani yangu anasema japo anafanya kazi ngumu na anachoka kama punda mbeba mizigo jangwani, inabidi akirudi apike, afue n.k maana alishamfumania mumewe na mdada wa kazi. Tena mume akamkanya eti kama hatatimiza majukumu yake, ataoa dada wa kazi. Aibu ya kuolelewa dada kazi bora akomae na kufua majeans.

Halafu kuna wakina sie – Wasimbe.

Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa shida zote hizi zinakuja kwa sababu tumekataa kabisa kubadilisha taasisi ya ndoa, mfumo na matarajio ya wanandoa. Mpaka leo tunataka kuishi, kama wahenga walivyoishi kwenye zama za mawe za kale. Tunakwama. Ndoa zinakosa maana.

Zama hizo walizoishi wao waliyofanya yali-make sense. Kwa mfano, japokuwa wanadini wanaamini ndoa ilianza na Adam na Hawa/Eva, wataalam wa historia na sayansi ya jamii watakwambia ndoa kama taasisi ilianza pale ambapo jamii zilianza kukaa pamoja na kumiliki Rasilimali. Kabla ya hapo, kwa mujibu wa wataalam hao, watu walikuwa wanajamiiana ila si kwa taratibu za kindoa kama tunavyozijua sasa.

Enzi zile upatikanaji wa mali ulitokana na uwezo wa watu kutumia nguvu, iwe kuwinda, kutengeneza zana (za mawe au chuma), kulima, kuvua n.k. Wanafamilia wenye nguvu kazi kubwa (watu wengi) walikuwa na uwezo mkubwa wa kufanikiwa zaidi.

Kutokuwepo na mbinu za uzazi wa mpango kuliwafanya wanawake wengi, wawe aidha wana mimba au mtoto mchanga muda wote. Si mnaujua ule msemo wa ‘masika mimba, kiangazi mtoto’? Ewaaa, ndivyo ilivyokuwa!

Na hapo ndipo mgawanyo wa majukumu ulipotokea na shughuli na tamaduni za kuozeshana zilipoanza. Wanawake wakitolewa mahari ili wawe wazalishaji wa nguvukazi (watoto). Nguvukazi hiyo ilipewa ubini wa baba au wajomba kama alama ya umiliki. Pale ambapo walizaliwa watoto wa kike, basi baba au mjomba alipokea ‘mali’ (mahari) na kuwatoa mabinti zake wakazalishe nguvukazi kwenye jamii nyingine.

Uhitaji wa nguvukazi kubwa kwa haraka ulilazimisha wanaume waoe wake wengi. Ndoa za mitala zilikuwa ni jambo la kawaida kabisa. Kabla ya ujio wa dini zilizokataza au kuweka ukomo ya idadi ya wanawake wa kuoa, kwenye jamii nyingi za kale ukomo wa idadi ya wake ilitegemea ukomo wako wa kulipa mahari.

Katika jamii hizi, ndoa zilikuwa na kazi maalum, kuzalisha nguvu kazi, kuwa sehemu ya utambulisho wa mtu, kuwa taasisi ambayo mali na rasilimali zinamilika na kusaidia jamii kuendelea kwa maana ya mgawanyo wa kazi.

Pale ambapo wanaume walitoka kwenda kutafuta rizki, muda mwingine iliwachukua siku kadhaa, wanawake walibaki kijijini na kwa umoja wao wakilea nguvukazi na kufanya kazi za nyumbani ikiwa ni pamoja na kuzalisha chakula. Ndoa hazikuwa kuhusu mapenzi na mahaba, bali kutimiza mahitaji ya jamii (practical purposes).

3.jpg

Leo tuko mwaka 2022, tunausogelea mwaka 2023, rizIki na mali kwa sehemu kubwa hasa huku mijini, hazitafutwi tena kwa kutumia nguvu na misuli, bali akili na maarifa. Maboresho katika sekta ya elimu na kupanuka kwa huduma za uzazi wa mpango kumeongeza ushiriki wa wanawake kwenye shughuli za kiuchumi. Maendeleo ya teknolojia yameleta matarajio tofauti hasa kwenye sekta ya mahaba.

Ukuaji wa uchumi na kukua kwa miji kumevunja mshikamano wa Kijamii. Ubepari umeleta umimi na ubinafsishaji wa mali. Sasa mafanikio ya familia yanategemea zaidi ubora na si wingi wa wanafamilia. Katika muktadha huu tulitarajia kama jamii tuanze mchakato wa kubadilisha matarajio na labda mfumo wa ndoa.

Niliwahi kuongea na rafiki yangu mwanaume na kumuuliza kwa nini hataki kuoa tena baada ya kuachana na mtalaka wake? Jibu lake lilikuwa, “Naogopa mgogoro wa mali, hiki nilichokichuma nataka kirithiwe na wanangu, ndoa zetu ni ‘all inclusive’, chake changu na changu chake, sasa kwa sisi ambao tuna watoto ukioa tena unatafuta majanga kuliko furaha.”

Majibu yake yalinifanya nimvutie waya swahiba wangu, msimbe mwenzangu, nimpe hizi habari njema kuwa kuna wakaka ambao wanataka kuwa na mahusiano/ndoa ila wanaogopa migogoro ya mali, mana huyu swahiba wangu kila siku alikuwa anasema, yeye hafuati mali kwenye ndoa, ana zake.

Kiherehere changu kilizimishwa na majibu yake mafupi ila mazito, aliniambia, “Mishy, wakaka wengi kama hao wako emotionally unavailable, wanataka tu kuwa na independent women but they have no idea, what to do with them.” Hapa alikuwa anamaanisha kuwa wanaume wa aina hiyo hawana muda wa kuwa pamoja na wewe vilivyo kihisia, wanataka tu kuwa na wanawake walio huru na wanaojitegemea lakini hawajui wafanye nini na wanawake hao wanapokuwa nao.

Kimsingi, alinieleza yeye anataka kuwa na mwenza atakayekuwa mwandani, msiri, na mfariji wake. Mwenza wa kumuonea ruhuma, wa kumtia moyo, wa kufurahi na kuhuzinika nae. Kwa kizungu tungesema soulmate maana kwa mujibu wake, japo anaweza kukimbizana na maisha, na anajua kuitafuta pesa haswa, ila kuna hitaji la moyo la kupendwa na kujaliwa.

Shida ni pale huyo mwenza, na jamii inayomzunguka, bado wanapokuwa na matarajio yaleyale ya mke wa zama za mawe za kale. Ndoa haitakuwa ‘yeye (mke) anataka nini’ bali ‘mume anataka nini’. Hakuna hata kauchochoro ka kusema, basi tupange wote tunataka nini – utaambiwa wewe sio wife material, sio kama bibi zetu. Hawakumbuki kuwa bibi zetu hawaishi maisha yetu. Kigumu ni kipi hapo kuelewa?

Anyways, kwa hapa tulipofika, ndoa siyo tena sehemu ya kuanza au kupata maisha. Siku hizi wadada na wakaka wote wanaweza kuyatafuta maisha nje ya ndoa na wakafanikiwa. Siyo tena sehemu pekee ya kupata watoto maana zamani kuzaa nje ya ndoa dunia ingeweza kukumeza mzimamzima. Ila siku hizi wala. Mpaka baadhi ya makanisa yana utaratibu wa kurejesha watu kundini japo sijawahi kuona wakaka wanarejeshwa kundini kwa kuzaa nje.

4.jpg

Ndoa sasa zinaacha kuwa kipimo pekee cha mafanikio na heshima, japo ka-pressure bado kapo hasa kwa wadada. Ila nawajua wadada na wakaka wengi wanaoana ili ‘watoe nuksi’ basi ‘waridhishe wazazi’ na maisha yanaendelea kuwa bukheri baada ya talaka. Mjini wanasema heshima pesa, mengine yanaongeleka.

Maana pekee iliyobaki ni ya kiimani. Katika jamii zetu ambazo dhambi haziogopwi kivile tena, siku si nyingi maana hii nayo itapotea. Kama alivyoniambia kaka yangu senior bachela, kuliko kujibebesha stress za kuandaa harusi za gharama, kuishi maisha ya kuwafurahisha wakwe na kudeal na mke na shida zake, bora aendelee kuwa na rafiki tu, atatubu.

Kama kweli, tunataka ndoa ziendelee kuwepo, basi tuzitafutie maana mpya na mifumo mipya inayoakisi mahitaji wa wanandoa wa karne hii ya ishirini na moja. La sivyo tutaendelea kuhesabu talaka, single mothers and fathers na ongezeko la kutisha la ukatili wa kijinsi(a) pamoja na mauaji baina ya wenza. Ni muda sasa wataalam wa sayansi wa jamii kuanzia wanasosholojia hadi wanasaikolojia kufanya kazi yao ipasavyo au tuendelee kutia ndoa doa.
 
Back
Top Bottom