Hao wataalamu wenyewe sasa ambao wapo serikalini mtihani mkubwa. Ila nikupongeze kwa andiko zuri. Kwa kifupi umeandika hoja nzito sana.
Nimekuelewa zaidi hasa katika eneo la kuitafutia ndoa maana mpya badala ya kushika maana au mahitaji ya ndoa kwa sababu za kikale.
Ila sasa nilikuwa nataka kuhoji jambo, haiwezekani kuwa tuna changamoto ya kutoa mafunzo ya ndoa kama taasisi kuu kijamii na kitaifa na kuiwekea misingi ya kuhehsimiwa ikiwamo kuwa na kanuni na sheria za kuisimamia kiserikali na pia kuwa na mifumo ya kijamii kama Jando na Unyago?
Maana kwa nilichokiona sasa ni kwamba ukiacha haya mafunzo ya juu juu ya ndoa kama kitchen party, semina za makanisani na taasisi za kiimani, ambayo hayalengi kutrain watu seriously na kuwaandaa kwaajiri ya NDOA bali ni kama kupiga soga tu juu ya changamoto za kindoa, hakuna platforms kama zilizokuwapo miaka hiyo ambapo mtoto wa kike alikuwa anakalishwa chini anafunzwa na akina mama wanaoitumikia ndoa na kuitambua kama taasisi muhimu katika jamii kiasi kwamba akitoka hapo hata akakutane na mwanaume wa aina gani atajua kumudu kuishi nae kama mume na kuweza kufika mbali nae.
Pia watoto wa kiume walikuwa wakipewa mafunzo yao ya Jandoni kuwajenga kuwa na kaliba ya kiume na kujua wajibu na majukumu yao kifamilia na sio kutangatanga na kuzaa hovyo kama mbwa koko.
Kimsingi nadhani tunahitaji haya mafunzo yarejee kwenye jamii na kuaddress hili uliloliandika. Kimsingi mahitaji ya ndoa ni yake yale ila Shughuli za kiuchumi na kiasiasa ndizo zimeingilia masilahi ya ndoa.
Ndoa ikiheshimiwa kama taasisi namba moja katika taifa na Serikali ikaacha kiherehere cha kuingilia maswala ya Ndoa na kuwa muamuzi pekee wa nini kifanyike katika Ndoa huku ikipuuza asili ya jamii husika, tamaduni, maadili, na nguvu ya wanafamilia katika kusimamia haya mambo tutafeli mchana kweupe.
Nishauri tu kwa sasa tuanze kuchukua hatua sababu madhara yanayokuja kutokea miaka 100 kutoka sasa kwa namna hali jinsi ilivyo sidhani kama tutakuwa na salama ya kizazi chetu. Na yote ni matokeo ya kupuuza misingi au kutokutazama upya misingi ili jamii iweze kushikiria ndoa na kuiheshimu.