Mwanahamisi Singano: Ndoa hazina maana tena

Mwanahamisi Singano: Ndoa hazina maana tena

Coming from a single mother, no wonder! Ndoa ni taasisi, kama huamini katika ndoa, usiamini katika taifa...
 
Ameandika Mwanahamisi Singano.

Labda wewe ni mmoja wa wengi ambao baada tu ya kusoma kichwa cha habari na jina la mwandishi, tayari hasira zimekupanda. Pengine unasoma haya makala siyo kwa sababu ya kutaka kujua kilichoandikwa, bali unasoma ili upate cha kukosoa na kunidogosha. Nikuombe ushushe pumzi! Kuwa mpole kidogo, ni vizuri kwa afya yako.

Alright! Najua wajua kuwa mijadala ya migogoro ya ndoa na ongezeko la talaka imeshika hatamu, huku waliojibatiza utaalam wa ndoa wakiwa busy kutoa uchambuzi na masomo kwa wanandoa hasa wanawake, na serikali ikianza kuhamasisha midahalo ya ndoa.

Kwanza kabisa ni vema kufahamu kuwa muasisi wa ndoa ni Mwenyezi Mungu na ndiye ajuaye kile kinachopaswa kufanyika ili ndoa idumu. Unapotoka nje ya sheria ya Mungu ndipo ndoa inapogeuka mzigo mzito na malalamiko kama haya hujitokeza.

Kufuatia makanisa na serikali za kidunia kuuteka mchakato wa ndoa na hivyo kuibatilisha sheria ya Mungu, ndoa nyingi zimeingia matatani, wameibuka watu wanaojiita wanasaikolojia washauri wa ndoa wenye uwezo wa kuwapa wanandoa "manual" ya namna ya kuishi ili ndoa iwe ya amani na furaha nk. Hii yote ni ubatili na kutoelewa msingi wa ndoa. Ni kwa mtazamo huu vijana wa kileo wameona kwamba sheria ya Mungu imepitwa na wakati na sasa dunia inahitaji mtazamo mpya wa ndoa. Wameshindwa kuelewa kwamba wao ndio wamekaidi sheria ya Mungu wakifuata mawazo yao wenyewe, lakini pale walipokutana na ugumu wakamgeukia Mungu na kuanza kumshutumu kwa kushindwa kwao. Hiki ndicho alichokifanya mwandishi huyu.

Serikali haina nafasi yoyote kwenda ndoa zaidi ya kuweka rekodi. Sababu kubwa ya hili ni kuwa ndoa ni tendo la kiroho, wala sio la kimwili kama wengi wanavyodhani. Katika mwili haiwezekani kuungana na kuwa mtu mmoja, bali jambo hili lawezekana kabisa katika roho na hili ndilo kusudi la Mungu. Sasa serikali yaweza kuwaunganisha watu wawili wakaishi pamoja lakini watabaki kuwa wawili katika mwili na roho, hapo ndipo ilipo siri ya ndoa.

Kwa nini Kanisa? Kimsingi ndoa ni agano linalowekwa kati ya mume na mke mbele ya Mungu. Kwa maana nyingine ndoa ni agano lenye pande tatu tu, mume, mke na Mwenyezi Mungu. Tangu zamani za agano la kale ndoa zilifungwa mbele ya familia na watu wengine. Makuhani walishiriki pamoja na wana familia lakini hawakuwa na mamlaka ya kufungisha ndoa, kwani taratibu zote ziliwekwa wazi kabisa na Mungu ambaye ndiye shuhuda wa agano.

Ndoa ilifungwa kitandani, ambapo mwanamke alitarajiwa awe bikira na damu ilikuwa ishara ya agano. Bila damu hakuna ndoa, wala sio tamko la kuhani. Kumbe agano la ndoa limebebwa na mwanamke.

Sasa kanisa lilipoingilia mchakato wa ndoa kwa kusimama sehemu ya Mungu, kwamba ndilo lenye mamlaka ya kuamua ndoa ipi ni halali na ipi sio halali. Nje ya hapo limeweka masharti mengi ya kibinadamu na kulikaidi agano la Mungu. Tulipo sasa, bila kanisa kuidhinisha, ndoa ya Kikristo hukosa uhalali, lakini si hivyo mbele ya Mungu.
Kwa baadhi yetu tunaona jambo hili linafanywa kuwa jipya ila si jipya. Labda ukubwa umeongezeka. Pengine watu wamekuwa wepesi kulizungumzia kuliko ilivyokuwa awali, lakini migogoro na kuvunjika kwa ndoa ilikuwepo na ipo.

Tuseme tu ukweli. Watu wanaumia kwenye ndoa jamani. Wanawake kwa wanaume.

Mpaka leo kuna familia kama mume mtarajiwa hana nyumba, hana gari, hana kazi nzuri, hawakubali aoe binti yao, hata kama wanapendana kiasi gani. Kaka zangu walio kwenye ndoa wanajua jinsi matarajio yalivyo makubwa. Kuwa mume bora ni kuwa na kipato kikubwa kuliko mume wa rafiki wa mke wako na kumpa mkeo, mashemeji na wakwe, kila wanachotaka hata kama hakipo kwenye uwezo wako.

Hapa napo pana tatizo kubwa sana. Kabla ya kuoa ni vema kufahamu kusudi la ndoa. Hatuingii kwenye ndoa ili kutafuta mali kama wengi wanavyoamini hivi leo. Kuna watu wanajiwekea malengo kwamba wataoa wanawake ambao wana kipato ili kusaidiana kwenye maisha. Hili sio kusudi la ndoa, mwanamume ataingia kwenye ndoa akiwa na utayari wa kubeba majukumu yake kama mume. Mke pia ataingia kwenye ndoa akiwa tayari kubeba majukumu ya mke.

Ndoa ni taasisi MUHIMU ZAIDI katika maisha ya binadamu. Nasema hii ndio taasisi muhimu zaidi kwa sababu ndoa imara ndio msingi wa familia bora, malezi bora, kizazi bora nk. Nje ya ndoa ni ukweli usiopingika kwamba sio rahisi hata kidogo kutengeneza kizazi kinachozingatia mila na tamaduni fulani. Ndoa haikukusudiwa kuwa taasisi ya kusaka utajiri bali mali ni matokeo ya ndoa imara, yaani ni baraka za ndoa yenye msingi imara. Kupima mafanikio ya ndoa kwa kutazama umiliki wa mali ni kulikosa kabisa lengo la ndoa, ni kumpoteza mshirika muhimu wa ndoa, mtoto, pale anapopatikana (malezi bora). Ni mtazamo huu wa hovyo unaopelekea ndoa nyingi kuvunjika.

Ukiona familia inaweka kigezo cha mali kama sababu ya kumpata binti basi hiyo ni dalili ya wazi kwamba hujapata mke bado.

Shida ya afya ya akili ni kubwa mno kwa ‘wakaka’. Hawasemi tu. Wanalazimika kufanya dili hatari. Wanaumizana kenye kutafuta kipato na ‘wanasnichiana’, ili mradi ‘makasiriko’ kama yote ili ndoa iende. Kimsingi, tumevurugwa.

Huku kwa dada zangu ndio mtume salale. Hakuliki wala hakulaliki. Tunastiriwa na make-up tu.

Ila kila mtu analia na lake. Huyu analia mume hana muda naye, kama hayuko safari kikazi, yuko baa na marafiki, akiuliza, anajibiwa, kwani umekosa nini? Yule analia mume hajigusi kwenye majukumu ya kifamilia kwa kuwa mke ana kipato kikubwa.

Mke hakumbuki mara ya mwisho lini mume kumnunulia hata upande wa kanga, achia mbali kulipa ada au kununua bidhaa za nyumbani. Na akifungua mdomo kumuuliza anaambulia kipigo au matusi, eti anataka kumpanda kichwani mume kwa kuwa yeye ana hela kuliko mmume

Hizi ni aina ya ndoa ambazo zimepewa jina la ndoa lakini hazikufungwa kwa kuzingatia msingi wa ndoa. Hii inaitwa majuto ni mjukuu. Mwanamke asiyemjua Mungu daima yuko kwenye mashindano. Sasa huwezi kamwe kumridhisha mwanamke ambaye yuko kwenye mashindano na wanawake wengine. Ndio maana utakuta mke licha ya kuolewa anapambana kushinda taji la urembo mtaani, mke wa mtu anashindana na vibinti 'single' kwamba aonekane yeye ni mrembo zaidi, ana shepu bomba nk. Hizi ndio ndoa za kileo, matokeo yake wake wengi wanaishia kuwa vitoweo vya wahuni. Kwa ujinga huu ndoa zitadumu vipi? Ukitazama mwanamke wa kikristo anavyovaa atakwambia Kristo amemweka huru. Je Kristo alikufa ili wanawake wavae kama makahaba? Si kweli, huu ni uongo wa makanisa na hii ni mojawapo ya sababu za migogoro ya ndoa.

Halafu kuna mwanamume asiyemjua Mungu. Huyu anawezaje kuyafahamu majukumu yake kama mume? Si kila mwanamke ni mke na sio kila mwanamume ni mume, kumbuka hilo.
Shangazi yangu mie analia machozi yasiyokauka. Kuamua kwake kuukimbia upweke na kuogopa dhambi ya kuzini kukamfanya akubali kuolewa mke mdogo, sasa anafanywa mwizi wa penzi la Bi Mkubwa. Anajiona hana thamani na hastahili mapenzi wala faraja ya mume. Huo uadilifu unaosemwa haujui unafananaje.

Katika Ukristo hakuna bi mdogo au bi mkubwa. Mume mmoja, mke mmoja.
2-1.jpg


Na jirani yangu anasema japo anafanya kazi ngumu na anachoka kama punda mbeba mizigo jangwani, inabidi akirudi apike, afue n.k maana alishamfumania mumewe na mdada wa kazi. Tena mume akamkanya eti kama hatatimiza majukumu yake, ataoa dada wa kazi. Aibu ya kuolelewa dada kazi bora akomae na kufua majeans.

Majukumu ya mke ni nini? Nani alisema mke anaolewa akasake mali barabarani? Hili ni tendo la hovyo zaidi kwenye ndoa ingawa laonekana kuwa ni jema. Mke amepaswa kulindwa, unaanza kumruhusu akashinde ofisini au mtaani kwenye ujasiriamali akichangamana na wanaume wengine? Hii inaondoa kabisa maana ya ndoa.

Mwanamume halisi akitazama house girl anatekeleza majukumu yote ya nyumbani yampasayo mke hushangaa ilikuwaje akaacha kumwoa huyu? Thamani yake huvuka mipaka ya 'house girl'kwani amekamilika kwa kuwa na sifa za mke wa ndoa, anafua nguo za baba na watoto, anaogesha watoto, anapika chakula cha familia, anampokea baba arudipo, anamwandalia maji ya kuoga, anaongea na baba kwa lugha ya unyenyekevu na utii wa hali ya juu. Kwenye ndoa majukumu haya yanapaswa kutekelezwa na nani?

Kimsingi mwanamume anapooa anahitaji feminine energy sio masculine energy. Ukioa mwanamke anayetekeleza majukumu ya mwanamume utakuwa umeia masculine energy, mtakuwa mafahari wawili ndani ya zizi moja. Hivi ndivyo zilivyo ndoa za kisasa kiasi cha kupelekea mabubujiko ya talaka. Hakikisha unaoa mwanamke sio mwanamume mwenye mwonekano wa mwanamke.
Halafu kuna wakina sie – Wasimbe.

Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa shida zote hizi zinakuja kwa sababu tumekataa kabisa kubadilisha taasisi ya ndoa, mfumo na matarajio ya wanandoa. Mpaka leo tunataka kuishi, kama wahenga walivyoishi kwenye zama za mawe za kale. Tunakwama. Ndoa zinakosa maana.

Sababu ni kukataa kuifuata sheria ya Mungu. Sasa baada ya kujipangia taratibu za kidunia za ndoa kisha mambo kutushinda tunarudi kumnyooshea kidole Mwenyezi Mungu badala ya kujirudi na kuifuata sheria yake.

Itaendelea...

luchelele mzunguko
 
Back
Top Bottom