MwanaHalisi: Serikali hali ngumu - yaagiza kusitisha ajira na kutopandisha vyeo kuelekea 2012 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MwanaHalisi: Serikali hali ngumu - yaagiza kusitisha ajira na kutopandisha vyeo kuelekea 2012

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Dec 21, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  [FONT=&amp] Wadau;[/FONT]


  [FONT=&amp]Serikali yetu inayoongozwa na magamba sasa imedhihirika rasmi kwamba imefilisika. Mwanahalisi leo imeandika kwamba serikali iko hoi kifedha na imetoa nakala ya barua kutoka menejiment ya utumishi wa Umma ambayo ni taasisi chini ya Ofisi ya rais kwenda kwa makatibu Wakuu wote ikiwaagiza kwamba kutokana na ufinyu wa mapato ya serikali, ajira mpya zipunguzwe kwa asilimia 50. Upandishwaji vyeo nao upunguzwe kwa asilimia hiyo hiyo.[/FONT]

  [FONT=&amp]CCM KAZI KWISHA!!! WAMESHINDWA KABISA KUSIMAMIA NCHI! [/FONT]
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na bado! Ndo maana wanakazania Kafulila asamehwe bcoz hawana hela za by-elections?
  Na jee iwapo serikali ya magamba itakazania kuona akina Lema na wabunge wengine wa CDM wenye kesi za uchaguzi wakishindwa kesi hizo?
   
 3. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,035
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Ni kweli Taasisis zote za serikali, Wizara na Halmashauri zimeshaagizwa kupunguza bajeti ya Mishahara by January 2012 wapeleke bajeti mpya isiyojumuisha ajira mpya na kupanda vyeo.
   
 4. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  weka habari ndugu, wengine tuko jimboni kwa Tundu Lissu, magazeti huku 'mbado'.
   
 5. Mbayuwa2

  Mbayuwa2 Member

  #5
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaman wana JF. kama mwajiri wetu kafulisika? Mishahara yetu je!
   
 6. mfarisayo

  mfarisayo JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 5,035
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Na bado madaraja yamebokoka pande zote za nchi
   
 7. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Serikali kufirisika sipendi kabisa kuamini kauli hiyo: Ni namna tu kwa walioko juu waweze kuchukua chao mapema kwani 2015 imekaribika: iweje serikali ifirisike wakati wataalamu wa kupiga usingizi MJENGONI wanajiongezea posho!!!!!!!, Raisi ajaye anakazi kubwa ya kuziba mapengo kwani atakuta Hazina haina kitu kabisa.
   
 8. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Sisi tunapiga kazi kwa wazungu mpaka saa hizi tumeisha tia kibindoni maelfu ya shilingi. sijui tutafika mwaka mpya na pesa?
   
 9. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mficha mauti, ugonjwa humuumbua!

  Zitto alisema siku nyingi tu kuwa hamna kitu mule, kipara akabisha. Sasa mambo hadharani, tukae mkao wa kukimbia. Ukimbizi wa kiuchumi utakuwa mpya kwa watakaotupokea. Mi nilifikiri wangekata bajeti ya Land Cruiser V8, badala yake wanakata ajira mpya, mweh!

  Waongeze bajeti ya FFU manake mwakani tutaandamana mfano wake hakuna
   
 10. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  nchi zote zinazoendelea bajeti yake kama 3/4 yote ina enda kwenye matumizi ya utawala..
   
 11. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,151
  Likes Received: 2,112
  Trophy Points: 280
  na kwa wale wenye kawaida ya kusherehekea sikukuu, nwapeni pole kwani mishahara hakuna na mwezi utapita hivhivi
   
 12. Kinyengeli

  Kinyengeli JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2011
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tanesco wao mishahara tangu jana poa kabisa!! Hv wao sio serikali?
   
 13. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,155
  Likes Received: 3,346
  Trophy Points: 280
  Nimeshanunua nakala ya gazeti, i cant wait kuisoma.
   
 14. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Si tuliambiwa ni Uchumi imara? Kumbe ni Uchumi Uchwara wa Ndullu na Mkullo.
   
 15. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Masikini JK. Kama ni kweli angalia cha kufanya.

  AM sure rais ajaye atakua makini hali hii (kama ni kweli) isitokee.
   
 16. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kweli nimeamini Kusoma kwingi hakuna maana. Huyo bwana naona ni bure kabisa.
   
 17. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #17
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  Alichokikimbilia mule jumba jeupe ndio atakijua sasa!!!!historia haitamsahau huyu mjomba!!aibu kubwa sana anaturudisha enzi zile za ankal yake nae nchi ilienda mrama kama sasa!!
   
 18. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #18
  Dec 21, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Serikali imefilisika kiuchumi
  Viongozi wa Serikali wamefilisika kichwani hamna kitu
   
 19. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #19
  Dec 21, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,509
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Nasubiri FF atuletee zile figure zake za uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi chini ya uongozi wa JK!!
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Dec 21, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Serikali ipunguze matumizi kwa kufuta wizara ambazo hazina maana wala tija kwa taifa.
  1. Wassira na Wizara yake ya uhusiano (haina tija kabisa)
  2. Utawala bora (tayari tuna wizara ya katiba na sheria)
  3. Uwezekezaji (tunayo wizara ya viwanda na biashara)
  4. Wizara inayosimamia ajira - ifutwe kabisa hakuna kitu pale. Ajira gani wakati vijana wanauza viberiti ubungo mataa tena kwa kufukuzana na city?
   
Loading...