MwanaHalisi: Serikali hali ngumu - yaagiza kusitisha ajira na kutopandisha vyeo kuelekea 2012

serikali bado haijafilisika! Ukisema imefilisika unakosea. Assets za serikali zina offset liabilities zake. Isitoshe, serikali inauwezo wa kutumia njia nyingi tu ili kupata fedha. Kuchelewa mishahara, kupunguza mishahara, kushuka kwa thamani ya shilingi, ni mambo ya kimkakati yamakusudi ku control uchumi wetu. mfumko wa bei uliopo ni wa muda tu, utapita kwa sababu kwa kiasi kikubwa unasababishwa na bei za vyakula. watu wakivuna, mfumko utashuka sana. japo kuna factors kama nishati etc
 
Serikali ipunguze matumizi kwa kufuta wizara ambazo hazina maana wala tija kwa taifa.
1. Wassira na Wizara yake ya uhusiano (haina tija kabisa)
2. Utawala bora (tayari tuna wizara ya katiba na sheria)
3. Uwezekezaji (tunayo wizara ya viwanda na biashara)
4. Wizara inayosimamia ajira - ifutwe kabisa hakuna kitu pale. Ajira gani wakati vijana wanauza viberiti ubungo mataa tena kwa kufukuzana na city?

Mkuu, siku hizi hata hiyo ajira ya kuuza viberiti ni mgogoro maana siku hizi Tanzania inatuagizia wataalamu wa kichina kufanya shughuli za Machinga.
 
Inashangaza kuona kuna watu wakisikia habari za kufilisika kwa serikali wanazishangilia just for political interests; huu ni ujuha usio na mfano!!! Na ujuha unakua maradufu zaidi pale unapokuta watu wanafanya hivyo just kwa ajili ya wanasiasa kv wao si key players kwenye political filelds!! Mwanasiasa ni mwanasiasa tu; awe CCM, CDM, au CUF!! Ukikaa hapo kutarajia chama kimojawapo kati ya hivyo kitakuondolea umasikini wako basi wewe kalagha baO!!! Pamoja na yote, mimi ni miongoni mwa watu ambao hawaamini kwamba eti serikali imefilisika kwa kuangalia vigezo visivyo na mashiko!!! Kupunguza ajira au kusitisha upandishaji wa vyeo ni mambo ambayo hayaajanza jana wala juzi na wala haitakuwa mwisho!! Na hii si kwa TZ tu, bali duniani kote inafanyika!!!! Kwahiyo, kama usitishaji wa ajira mpya na vyeo ni kufilisika kwa serikali basi nchi hii ilishafilisika miongo kadhaa iliyopita kwani kuna wakati miaka ya nyuma serikali ilishawahi kuacha kuajiri kwa miaka kadhaa!!! Inawezekana kabisa kwamba mapato ya serikali yameyumba kwa sababu zilizo wazi kabisa; hili ni jambo la kawaida popote pale duniani hata katika mazingira ya kawaida kama vile kwenye business world!! Inapotokea hali kama hiyo, ni lazima uangalie nini usitishe, nini uendelee nacho hadi pale system itakapokuwa in equilibrium.
 
1.Inashangaza kuona kuna watu wakisikia habari za kufilisika kwa serikali wanazishangilia just for political interests; huu ni ujuha usio na mfano!!! Na ujuha unakua maradufu zaidi pale unapokuta watu wanafanya hivyo just kwa ajili ya wanasiasa kv wao si key players kwenye political filelds!! Mwanasiasa ni mwanasiasa tu; awe CCM, CDM, au CUF!! 2. Ukikaa hapo kutarajia chama kimojawapo kati ya hivyo kitakuondolea umasikini wako basi wewe kalagha baO!!! Pamoja na yote, mimi ni miongoni mwa watu ambao hawaamini kwamba eti serikali imefilisika kwa kuangalia vigezo visivyo na mashiko!!! Kupunguza ajira au kusitisha upandishaji wa vyeo ni mambo ambayo hayaajanza jana wala juzi na wala haitakuwa mwisho!! 3. Na hii si kwa TZ tu, bali duniani kote inafanyika!!!! Kwahiyo, kama usitishaji wa ajira mpya na vyeo ni kufilisika kwa serikali basi nchi hii ilishafilisika miongo kadhaa iliyopita kwani kuna wakati miaka ya nyuma serikali ilishawahi kuacha kuajiri kwa miaka kadhaa!!! 4. Inawezekana kabisa kwamba mapato ya serikali yameyumba kwa sababu zilizo wazi kabisa; hili ni jambo la kawaida popote pale duniani hata katika mazingira ya kawaida kama vile kwenye business world!! Inapotokea hali kama hiyo, ni lazima uangalie nini usitishe, nini uendelee nacho hadi pale system itakapokuwa in equilibrium.

1. Kwa kweli suala la nchi kufilisika siyo habari njema ya kushangiliwa kwa sababu hali zetu kimaisha zinazidi kudidimia. Lakini hata hivyo mtu aking'ang'ania jambo halafu likamshinda anajishababishia kicheko yeye mwenyewe. tuna serkali na chama tawala ng'ang'anizi ambao kiutendaji walishashindwa siku nyingi tu.

2. Chama tawala na serkali yake vina wajibu usiokwepeka wa kuwaendeleza na kuwatoa kwenye umaskini wananchi wake, hili haliwezi kupingika ni wajibu wao na ni lazima wafanye hivyo. Nchi zinatumia hela nyingi wakati wa kampeni za uchaguzi, wagombea wanaeleza sera zao na jinsi watakavyo waletea wananchi maendeleo na kuondoa umaskini. Kama huu sio wajibu wao je kuna haja gani ya kuwepo serkali au rais? Je tunahitaji raisi ili awe anafungua tamasha na mikutano? au kuhutubia kwenye sherehe na kutokea kwenye vyombo vya habari? Msanii? Kwenye hali ya kawaida wananchi wanapata nafasi ya kumchagua mgombea au chama chenye sera nzuri, lakini kwa bahati mbaya sisi tanganyika tunachakachuliwa, matokeo yake tunapata viongozi na chama majizi ambayo hayaamini wala hayana uwezo wa kuleta maendeleo ya nchi bali ya kutunisha matumbo yao binafsi. Serkali ni kama mfugaji mwenye jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa mifugo yake lakini uamuzi wa kunywa au la unabaki wa mifugo yenyewe. Serkali inawajibu wa kuweka sera, miundo mbinu na taasisi za kuleta maendeleo kwa wananchi wake na kuwasaidia wale ambao kwa sababu mbalimbali wanashindwa kujiendeleza na siyo kujilimbikizia mali

3.Hii habari ya kushindwa na kutafuta visingizio inachefua sana. Unaugua maralia badala ya kupima damu unasema umelogwa matokeo yake utakufa kwa maralia. Huko duniani kote hakutuhusu shida zao siyo zetu wala shibe au njaa yao haituhusu. Kama wewe ni dereva uko kwenye msafara na magari yote yaliyokutangulia yakagongana, je hutachukua tahadhali ili usiingie kwenye ajali hiyo? au utaendelea kuendesha na kugongesha gari lako kwa vile kila gari limegonga? Kuna tatizo gani kama tanganyika uchumi wake hautateteleka kama nchi zingine? Dhana kwamba uchumi ni mbaya dunia nzima hivyo ni haki tanganyika pia iwe na ubovu wa uchumi ni dhana potofu. Hali ya uchumi inapokuwa mbaya nchi zinachukua tahadhali na kuweka mikakati ya kukabiliana na hiyo hali.

4. Sababu zinazoyumbisha mapato ya serkali kwa kweli zipo wazi mfano ufisadi, kushindwa kukusanya kodi, uongozi wa kujuana hivyo kupunguza uwajibikaji, serkali legelege inayoongwa hadi suti, viongozi wajinga wasiojua wafanye nini, jamii ya watu wapumbavu nk nk
 
serikali bado haijafilisika! Ukisema imefilisika unakosea. Assets za serikali zina offset liabilities zake. Isitoshe, serikali inauwezo wa kutumia njia nyingi tu ili kupata fedha. Kuchelewa mishahara, kupunguza mishahara, kushuka kwa thamani ya shilingi, ni mambo ya kimkakati yamakusudi ku control uchumi wetu. mfumko wa bei uliopo ni wa muda tu, utapita kwa sababu kwa kiasi kikubwa unasababishwa na bei za vyakula. watu wakivuna, mfumko utashuka sana. japo kuna factors kama nishati etc

Hujasikia mikoa ya kusini mahindi yanaoza kwa kukusa sehemu ya kuhifadhia? Sawa wewe unasuburi mavuno yapi ili bei za chakula zishuke?
 
Uarabuni wametorosha fedha na wanyama yaani hii nchi sasa hv ni kwishen kabisa

Nasema fedha zetu zilizokwishatoroshewa Uarabuni kamwe hakiwezi kutukwepesha UCHUMI UTAPIAMLO kihivi licha ya wataalam wetu kujihangaisha sana hivi sasa.

Nakuambieni hamna kilichobaki pale, taabu kweli kweli mwakani lakini cha ajabu hela kinunulia vyombo vya FFU zenyewe zimepatikana badala ya kuchagua njia yenye bajeti ndogo; wananchi kujiundia mpya katiba.
 
Hujasikia mikoa ya kusini mahindi yanaoza kwa kukusa sehemu ya kuhifadhia? Sawa wewe unasuburi mavuno yapi ili bei za chakula zishuke?

Sio kosa lake huyo, achana nae huyo, hajui asemalo!!
 
Back
Top Bottom