Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Wana-JF:
Nimeona ni vyema niwawekeeni hii sehemu ya mwisho ya stori katika Mwanahalisi la leo kuhusu sakata la Dr Slaa, Mahimbo, na Josephine. Ningekuwa na muda ningeweza kui-key in yote, lakini sehemu hii kidogo inadokeza mwanga wa kile kilichotokea nyuma ya mapazia. Asanteni.
..Kwa mujibu wa mtoa taarifa wa gazeti hili, Mahimbo ametafutwa na CCm kwa udi na uvumba kwa maelekezo ka Katibu Mkuu Yusuf Makamba, ili kukamilisha mradi wao dhidi ya Dr Slaa.
Mengine sasa utafute mwenyewe na kuthibitisha; lakini naambiwa kuwa CCM wamemtafuta, kumpa gari, kumkodishia hoteli na mumhkakikishia kulipa gharama za wakili, ilimradi ijulikane amempeleka Dk Slaa mahakamani, kimeeleza chanzo chetu.Mwandishi huyu aliwasiliana na Mahimbo kupata maelezo ya upande wake na yafuatayo ni sehemu ya majadiliano kati yao.
Mwandishi: Tuna taarifa kwamba ulikutana na Yusuf Makamba wiki iliyopita na akaupa maelekezo juu ya haya unayofanya.
Mahimbo: Hayo mambo siyajui.
Mwandishi: Mbona kuna madai kuwa ulitengana na mkeo miaka mitatu iliyopita; kwa nini unaibuka leo?
Mahimbo: Hayo muulizeni yeye.
Mwandishi: Makamba amekupa gari na amegharamia ukae hotelini
Mahimbo: Sijui (akata simu)
Naye Josephine ambaye anakata mbuga na wapambanaji wa Chadema alipoulizwa juu ya sakata hilo amesema: najua kinachoendelea. Haya yote yameibuliwa na wapinzani wa kisiasa wa Dk Slaa. Nawafahamu hata kwa majina.
Josephine anakiri kuwa alikuwa ameoana na Mahimbo lakini hawako pamoja kwa miaka mitatu sasa.
Amesema kwa ufupi, kwa njia ya simu kutoka Singida, kuwa kama wewe ni mwanamme na unakaa miaka mitatu bila kumuona mkeo, na katika kipindi chote hicho huchukui hatua, basi wewe una matatizo.
Juhudi za kumpata Makamba kujibu maswali kadhaa hazikufanuikiwa. Alikuwa aulizwe iwapo ni yeye anayesimamia mradi wa kuchafua Dk Slaa.
Alikuwa aulizwe pia juu ya tuhuma kuwa ni kupitia kwake, gazeti moja lilipata fedha za kuchapisha toleo moja lenye taarifa zinazohusu Dr Slaa na kugawiwa bure.
Swali jingine lililolenga Makamba lilihusu wafadhili wengine wa mradi huu ambako taarifa zinamtaja Rostam Aziz na Abdulrahman Kinana, mwenyekiti wa Kampeni ya mgombea wa CCM.
Si Rostam wala Kinana aliyepatikana kuzungumzia ushirika wao.
Hata hivyo, MwanaHalisi linaweza kuthibitisha kuwa mmoja wa wahariri wa gazeti lililochapisha tuhuma dhidi Dk Slaa, alikutana na Makamba, makao makuu madogo ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam siku mbili kabla ya gazeti kuchapishwa.
Taarifa zinasema miongoni mwa makubaliano kati ya mhariri na Makamba, ni kugharamia uchapishaji na baadhi ya gharama za uendeshaji wa gazeti.