MwanaHALISI laibukia MSETO...

Naona kama Wanatapa tapa vile mbona kilichoandikwa kwenye Mseto ni copy & Paste ya kilichoandikiwa kwenye Mwanahalisi Jumatano iliyopita.

Sasa nani anatapatapa? Mwanahalisi au Serikali? Kwa mwananchi ambaye hata hakuwa amesoma Mwanahalisi halafu akataka kulitafuta hawezi lipata tena maana limefungiwa....kumhabarisha ni kuchapisha makala zilizopelekea gazeti la Mwanahalisi kufungiwa...kama ni wewe ungefanya nini katika taaluma yako?
 
nilikuwa nikizungumza na ndugu yangu mmoja jioni hii akanambia kuwa eti gazeti la mwanahalisi limekuja kwa staili mpya mabapo eti kubenea anashusha habari nzito za uchunguzi kupitia gazeti la mseto linalomilikiwa na kampuni ya hali halis publishers na akanitolea mfano leo kuwa eti gazeti hili ambalo huwa ni mahsusi kwa ajili ya michezo headlne yake ilikuwa ni ya siasa na sio michezo.hili likoje jamani/naomba ufafanuzi

ni kweli,jana nimenunua mseto,ameirudia habari yote ya dr Uli
 
Kati ya Radio Imani na Mwanahalisi ni kipi cha hatari zaidi?


Radio Imani na Mwanahalisi nani ameandika taarifa za Usalama wa Taifa.

Au mwenzangu unapouliza kati ya Radio Imani na Mwanahalisi kipi cha hatari una maana gani?
 
mbinu ya kukabili uandishi wa habari kama za kina kubenea kwa kuyafungia magazeti yao haziwezi kuzaa matunda km wao wanavyodhani,hiki si kipindi cha mwaka 47,wakiziba mlango mmoja,mungu atafungua mingine saba zaidi.ni utawala wa kitoto na usio na strategy,madudu matupu
 
R.I.P Mwanahalisi.

Hayo waambie nyinyiemu, kwani ndivyo itakavyokuwa katika miaka michache ijayo, na haki ya Mungu nakuhakikishia, mkiondoka madarakani hamrudi ng'o, mtatokomea nyikani kama vile UNIP na KANU!

Kwa ufahamisho wako, jana gazeti la Mseto liliuza kama njugu, wengi walinunua kwa sympathy kwa Kubenea. Alinidokeza kwamba alipata ushawishi a-print extra copies!

Huwezi kuzuia nguvu ya umma wewe -- hata uki-apply visheria vyenu vya kidikteta -- Gaddafi yu wapi? Hosni yu wapi?

Ila kitu kimoja naamini: Kujikomboa kutoka ukoloni wa weusi ni kazi kubwa kuliko wule wakoloni wa weupe! Lakini mtaondoka tu, nyie siyo miungu!
 
Hatuchoki mpaka kieleweke
go mwanahalisi tuko pamoja na mungu atawalinda na tindikali za serikali
 
Nilisikia wahariri wanataka kuandamana kupinga kufungia Mwanaharisi!vipi walifanikiwa au ndio taarifa za kiintelejensia on system?
 
Serikali ya watu wasiotumia taaluma kufanya mambo. Wao kama wangeta kubenea au mwanahalisi wasiandike habari ya ulimboka kwa sababu wanazojua wao basi wangepiga marufuku makala hiyo au habari za ulimboka kuandikwa.

Sasa kufungia gazeti ni kumzuia muumini kuswali lakini kwa kumnyang'anya kitabu cha sala wakati anaweza kununua kingine na akaendelea kusali
 
Hivi lile Gazeti la Mengi la Kasheshe Bado Lipo Kifungoni? nakumbuka nalo lilifungiwa kwa Muda Usiojulikana....
 
Namshauri ni bora afanye hivyo kuliko kusubiri m;samaha wa serikali ambao hatujui utakuja lini. Towards 1995 marehemu Ben Mtobwa alifanya hivyo wakati gazeti lake la Heko lilipofungiwa kwa muda. Alitumia gazeti lake jingine la Kalulu kuchapa habari ambazo zingechapwa na Heko.
 
La udaku?

Halikuwa na tofauti sana na hili

DARMATESO.jpg
 
Nalimiss kwa kweli Mwanahalisi. Jamaa walikuwa wanashusha vitu ambavyo mara nyingi havipatikani katika magazeti mengi nchini.
 
Back
Top Bottom