Si kitu cha ajabu kwa gazeti la michezo kuta habari nyingine, na si kinyume cha sheria. Mara nyingi magazeti ya akina Shigongo huwa yanaandika habari za siasa, utadhani Uhuru.
isitoshe mwaka 1995 wakati akina Jenerali Ulimwengu walipoanzisha Dimba (la michezo) gazeti hilo lilikuwa linaandika habari za siasa, zakampeni za uchaguzi, hadi pale walipoanzisha Mtanzania, na baadaye RAI.
Lakini ninachohofia hapa ni kwamba katika serikali hizi za kihovyo hovyo inaweza pia kulifungia gazeti hilo kutimiza uchu wake wa kuwaziba wananchi wasijue jinsi serikali yao inavyofanya unyama kwa wananchi wake.
Halafu kitu zaidi kinachonishangaza ni kwamba serikali ilishindwa kabisa kuelezea kivipi Mwanahalisi kilisema uongo katika matoleo yake iliyotaja kukiuka maadili kuhusu sakata la Ulimboka.
Mimi nadhani imefika wakati sasa serikali iwaambie wananchi kuwa sakata la kutekwa ulimboka halikuwapo kabisa na kwamba daktari huyo huenda alipigwa na mke wake nyumbani.
Sijaona serikali kama hii. Lile gazeti la Rupert Murdoch la NEWS OF THE WORLD lilikowa linaandika habari za uongo za kupotosha umma na wahariri wake kudukuu simu za watu wengine hazlikufungwa na serikali ya huko Uingereza, mmiliki wake mwenyewe ndiyo aaliamua kulifunga kuondoa malalmiko.