salosalo
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 596
- 278
Serikali ya CCM unajiua na kuua chama bila kujitambua. Naonmba nianze na swali hili: Hivi washauri wa serikali na chama cha CCM mko wapi? Nani kawaloga hata mkaamua kujichimbia kaburi wenyewe ?
Ushauri wangu wa bure:
Kama hamjui mmevunja kioo chenu cha kujitazamia,matokeo yake mnatoka nje mkiwa hamjachana nywele, matongotongo usoni, lip-stick hadi puani, sura na nguo vinafanana kwa jinsi vilivyokunjamana. Hamuwezi kujua haya mpaka mrudishe kioo cha kujitazamia kabla hamjatoka nje, ndipo mtaweza kujisafisha mungali ndani kabla ya kuja kupata aibu huku nje.
Matusi
Najua utahisi nimekutukana, ila ni kweli nimekutukana. Wewe unamatongotongo machoni, tena nilishau kukwambia kinywa na kwapa vimejaa harufu mbaya na rangi za ajabuajabu. Nywele vururu-vururu. Fanya hima rudi ndani karekebishe haya yote maana ni matusi haya yanayotaja uhalisia wa jinsi ulivyo. Leo nakwambia kwa mara ya mwisho, nenda karudishe kioo chako ili uyaone mauchafu kama haya kabla ya kuja uraiani.
Safari
Mimi ninasafiri nje ya nchi kwa muda wa miaka miwili, ntarudi mwaka 2015. Usiporudisha kile kioo chako utakosa hata wa kukusalimia sababu ya uchafu. Maana ni mimi na kioo tu tunaoweza kukwambia ukweli ili urekebishe na kuondoa uozo mwilini mwako, wenzangu na marafiki zako wote hawakwambii badala yake wanakuchekea kinafiki, eti wanakuogopa wakikwambia ukweli utawachukia na kuwaadhibu kama ulivyofanya kwa kioo. Hivi kumbe kioo umekiondoa ukidhani unakiadhibu ee? Ha ha haaaaa!!!(nacheka kidogo), kama ni hivyo umejiadhibu mwenyewe.
Cha kuanya
Rudisha kile kioo ili kikuonyeshe uchafu wote ulonao. Utaumia sana kwa kuonyeshwa huo uchafu lakini kwa kadiri utavyokuwa ukiumia ndivyo utakavyokuwa ukijipanga kupambana na matongotongo ili kesho kioo asikuonyeshe tena.
Kumbuka mimi sirudi hapa mpaka 2015, kama na kioo hutamrudisha nadhani hata mimi nikirudi safarini, ntakukataa maana utakuwa mchafu wakupindukia
Anayekukamua jipu hadi damu nyekundu , ndiye akutibuye kwelikweli pamoja na kwamba utaumia sana. Mwogope sana yule anayepulizapuliza jibu lako na kukupa pole nyingi bila kukukamua.
Dedication
Huu ni ujumbe wako wewe rafiki yangu (SERIKALI) na nashukuru kwa kunisikiliza (MPIGA KURA) ila kama ukiona vema Mshirikishe Baba yako(CCM) maana naambiwa ndiye mshauri wako wa karibu ambaye UKIJAMBA anacheka na UKIJINYEA anacheka na kupiga makofi. Kioo(MWANAHALISI) hakunituma niyaseme haya, ila imenibidi nimshukuru kwa jinsi alivyokutunza bila kumuomba kmbe wewe hujapenda. Nikirudi (MPIGA KURA) toka nje mwaka 2015(UCHAGUZI) tafadhali nikukute safi vinginevyo urafiki wetu basi(SICHAGUI WATOTO WA BABA YAKO WALA BABA MWENYEWE). Kioo, tafadhali nakusihi kama rafiki yangu akikuhitaji tena usiache kukubali kufanya ile kazi ya mwanzo. Nadhani ni ujinga wake unamsumbua.