Mwanahalisi akifa anakufa na CCM - okoa mwanahalisi ili CCM idumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanahalisi akifa anakufa na CCM - okoa mwanahalisi ili CCM idumu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by salosalo, Aug 4, 2012.

 1. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Serikali ya CCM unajiua na kuua chama bila kujitambua. Naonmba nianze na swali hili: Hivi washauri wa serikali na chama cha CCM mko wapi? Nani kawaloga hata mkaamua kujichimbia kaburi wenyewe ?

  Ushauri wangu wa bure:
  Kama hamjui mmevunja kioo chenu cha kujitazamia,matokeo yake mnatoka nje mkiwa hamjachana nywele, matongotongo usoni, lip-stick hadi puani, sura na nguo vinafanana kwa jinsi vilivyokunjamana. Hamuwezi kujua haya mpaka mrudishe kioo cha kujitazamia kabla hamjatoka nje, ndipo mtaweza kujisafisha mungali ndani kabla ya kuja kupata aibu huku nje.

  Matusi
  Najua utahisi nimekutukana, ila ni kweli nimekutukana. Wewe unamatongotongo machoni, tena nilishau kukwambia kinywa na kwapa vimejaa harufu mbaya na rangi za ajabuajabu. Nywele vururu-vururu. Fanya hima rudi ndani karekebishe haya yote maana ni matusi haya yanayotaja uhalisia wa jinsi ulivyo. Leo nakwambia kwa mara ya mwisho, nenda karudishe kioo chako ili uyaone mauchafu kama haya kabla ya kuja uraiani.

  Safari
  Mimi ninasafiri nje ya nchi kwa muda wa miaka miwili, ntarudi mwaka 2015. Usiporudisha kile kioo chako utakosa hata wa kukusalimia sababu ya uchafu. Maana ni mimi na kioo tu tunaoweza kukwambia ukweli ili urekebishe na kuondoa uozo mwilini mwako, wenzangu na marafiki zako wote hawakwambii badala yake wanakuchekea kinafiki, eti wanakuogopa wakikwambia ukweli utawachukia na kuwaadhibu kama ulivyofanya kwa kioo. Hivi kumbe kioo umekiondoa ukidhani unakiadhibu ee? Ha ha haaaaa!!!(nacheka kidogo), kama ni hivyo umejiadhibu mwenyewe.

  Cha kuanya
  Rudisha kile kioo ili kikuonyeshe uchafu wote ulonao. Utaumia sana kwa kuonyeshwa huo uchafu lakini kwa kadiri utavyokuwa ukiumia ndivyo utakavyokuwa ukijipanga kupambana na matongotongo ili kesho kioo asikuonyeshe tena.
  Kumbuka mimi sirudi hapa mpaka 2015, kama na kioo hutamrudisha nadhani hata mimi nikirudi safarini, ntakukataa maana utakuwa mchafu wakupindukia

  Anayekukamua jipu hadi damu nyekundu , ndiye akutibuye kwelikweli pamoja na kwamba utaumia sana. Mwogope sana yule anayepulizapuliza jibu lako na kukupa pole nyingi bila kukukamua.

  Dedication
  Huu ni ujumbe wako wewe rafiki yangu (SERIKALI) na nashukuru kwa kunisikiliza (MPIGA KURA) ila kama ukiona vema Mshirikishe Baba yako(CCM) maana naambiwa ndiye mshauri wako wa karibu ambaye UKIJAMBA anacheka na UKIJINYEA anacheka na kupiga makofi. Kioo(MWANAHALISI) hakunituma niyaseme haya, ila imenibidi nimshukuru kwa jinsi alivyokutunza bila kumuomba kmbe wewe hujapenda. Nikirudi (MPIGA KURA) toka nje mwaka 2015(UCHAGUZI) tafadhali nikukute safi vinginevyo urafiki wetu basi(SICHAGUI WATOTO WA BABA YAKO WALA BABA MWENYEWE). Kioo, tafadhali nakusihi kama rafiki yangu akikuhitaji tena usiache kukubali kufanya ile kazi ya mwanzo. Nadhani ni ujinga wake unamsumbua.
   
 2. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Duh!!!!!!!!!!!!
   
 3. S

  Singo JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,073
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  nimependa hiyo fani na maudhui, ujumbe umefika.
   
 4. d

  dizo Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wataisoma kimyakimya.
   
 5. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Na kama wanabishana na ukweli huu, naomba wanipe ukweli wao
   
 6. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Dah, Basi hii ni zamani zile nikiwa nasoma fasihi nikiwa o'level ndo nilifundishwa Fasihi simulizi na andishi huko Lute camp-Tukuyu zote zikiwa na fani na maudhui ila baadaye nili-opt PCM.
   
 7. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,583
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Salosalo,
  Habari...!
  Kama umesoma Lutengano,then you MUST know the meaning of my NAME!!!
  Kwa kutumia uhalisia wa jina langu nimeamua kumpa LIKE mtoa mada...ujumbe wake ni murua sana.
   
 8. Gwamahala

  Gwamahala JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 3,583
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Wasipofuata huu ushauri,come 2015 hawatakuwa na wa KUMLAUMU!
  Umenena yaliyo KWELI tupu.
   
 9. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Umeona ee!!
  Huku nilipo ili watu wapate ushauri kama huu ni lazima walipie kuonana na mimi ndipo walipie ushauri nitakao wapa lakini hawa nimewapa bure bila kujali
   
 10. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Ni kweli nilishakuwepo Lute, Jina lako lina maana zifuatazo:- Gwamahala au Gifted au Mwenye akili au Bright au kwa wenye taaluma ya ualimu kama mimi basi ktk yale makundi ya Gold, Silver na Iron kwa wanafunzi, basi Gwamahala maana yake ni Gold. Hapo je umeamini?
   
 11. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Heri Mwanahalisi na CCM yake wafe pamoja ili tuokoe Tanzania kuliko wote kuishi ingawa ndoa yao ya siri haijajulikana.
   
 12. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Bora kuteseka kwa kuujua ukweli kuliko kufurahi huku ukidhihakiwa
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  CCM ni sikio la kufa...
   
 14. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Wow! Mtiririko umetulia,ni wao tu kukubaliana na ukweli!
   
 15. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Salosalo yupo wima kabisa, tatizo ni hawa wanaoambiwa. wametia pamba masikio hawasikii na hawaoneshi dalili za kutaka kusikia. hawa dawa yao ni kuwalazimisha wasikie, halafu wawajibike, vinginevyo tuwatoeni hawa. inatia hasira nchi za wenzetu ambao hata rasilimali tunawazidi halafu, wao wana nafuu ya maisha kimaendeleo kuliko sisi. lazima tupate mbadala wa hii serikali, ili mambo yaende sawa.
   
 16. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  atendaye makusudi hata umwambie vp ataendelea kufanya makusudi tu. ccm wanafanya makusudi hawataki kubadilika si kwamba hawajui wanachofanya
   
 17. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #17
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Ningekuwa karibu na nao ningewazibua vibao vya sikio kila mmoja ili wazibuke. Maana tumewapa kutuendesha wanalala kabla hatujafika, wanatutafutia kifo hawa
   
 18. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #18
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Kabisa mkuu, wanatakiwa wafanye kama jina lako linavyosomeka
   
 19. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #19
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Basi mimi hunishindi kwa jinsi ninavyopata kichwa moto kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa. Ila nakusihi twende wote Ughaibuni ili turudi wote 2015
   
 20. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #20
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Si ndio maana wanasema ni upepo wa kisiasa. Mbinu walizokuwa wakizitumia kutudanganya zimepitwa na wakati mkuu. Wanatakiwa wabadilike sana. Si kwamba tunaichukia CCM bali tunachukia namna yao ya utendaji na hapo ndipo tutakapotafuta utendaji mpya popote pale
   
Loading...