Mwanafunzi mjamzito amtaja Paroko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi mjamzito amtaja Paroko

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msharika, May 26, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwanafunzi mjamzito amtaja Paroko

  Katika hali inayoonekana kuwashitua wengi, mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya Sekondari ya Farkwa amemtaja Paroko wa Parokia ya Farkwa, Padri Godian Simpinge, kuwa ndiye aliyempa mimba.

  Tukio hilo lilikuja baada ya wanafunzi wawili wa sekondari hiyo, mmoja wa kidato cha kwanza na mwingine kidato cha tatu kukutwa na ujauzito, kufuatia zoezi la upimaji wa mimba lililoendeshwa na shule hiyo.

  Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mkuu wa shule hiyo, Rajabu Yengela, alisema zoezi hilo lilifanyika Aprili 22 mwaka huu. Alisema mwanafunzi mwingine wa kidato cha nne ambaye naye alihisiwa kuwa na ujauzito alitoroka wakati wa zoezi hilo likiendelea.

  Mwalimu Yengela alisema mwanafunzi wa kitado cha kwanza alikutwa na ujauzito wa miezi sita, huku mwenzake akiwa na miezi minne toka apate ujauzito.

  Mwalimu Yengela alisema, baada ya matokeo hayo, bodi ya shule iliagiza wanafunzi wote waitwe ili waeleze waliohusika kuwapa mimba hizo kisha wachukuliwe hatua.

  Alisema, katika kikao cha bodi, mwanafunzi aliyetoroka wakati wa kupima alipatikana baada ya wazazi wake kubanwa na uongozi wa shule, ambapo alimtaja mwanafunzi mwenzake wa shule ya Sekondari ya Msakwalo (jina tunalo) kuwa ndiye aliyempa ujauzito huo. Lakini yule wa kidato cha kwanza (majina tunayahifadhi) akamtaja Padri Simpinge na kwamba ilikuwa ni wakati alipokuwa akiuza duka la Parokia.

  Mwanafunzi huyo alifafanua kwamba Oktoba mwaka jana alichukuliwa kwenda kuuza duka la Parokia ya Farkwa wakati akisubiri matokeo yake ya darasa la saba.

  Alisema mwezi Novemba, siku na tarehe ambayo haikumbuki, 'Baba' Paroko huyo alimtaka waende wakafanye mahesabu ya mauzo ofisini kwake na walipoingia ndani, Paroko huyo akafunga mlango na kuanza kumpapasa, baadaye akamwangusha chini na kumbaka.

  Alisema Februari aliondoka parokiani hapo na kwenda kuishi na dada yake, lakini wakati wote huo hakujua kuwa ni mjauzito kwa kuwa ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukutana kimwili na mwanaume tangu azaliwe.Kaimu Katibu Tarafa wa Farkwa ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Farkwa, James Mayaka, alisema anashangaa kuona jeshi la polisi wilayani Kondoa likionekana kushindwa kulishughulikia suala hilo licha ya kuwa na vielelezo vyote ikiwemo kadi ya kliniki ya mwanafunzi huyo iliyomtaja paroko huyo kuwa ndiye mwenye ujauzito huo.

  Alisema ofisi yake ilipokea barua kutoka kwa mkuu wa kituo cha polisi cha Kwamtoro ikimtaka atume mgambo kwenda kuwakamata watu wawili, mmoja akijatwa kwa jina moja la Corneli kuwa ni mtuhumiwa namba moja na jina la pili likiwa la Padri Simpinge akitajwa kuwa mtuhumiwa namna mbili katika kosa la kumpa mimba mwanafunzi huyo.

  “Nilimpigia simu kumuuliza mkuu wa kituo, Corneli ni nani na anaingiaje katika kesi hiyo wakati mwanafunzi huyo katika maelezo yake yote amemtaja padri na hata katika kadi ya kliniki amemwandika padri kuwa ndiye mwenye ujauzito, nikajibiwa kuwa ninachotakiwa ni kutekeleza agizo kwa mujibu wa barua hiyo,” alisema mtendaji huyo.

  Alisema wahusika wote hawakupatikana na kwamba padri huyo alikuwa safarini.

  Kwa upande wake, diwani wa kata ya Farkwa, Gabriel Madge, alisema suala hilo baada ya kuona kuwa linasuasua waliamua kumwandikia barua mkuu wa wilaya ya Kondoa, Saidi Bwanamdogo, ili hatua zaidi zichukuliwe.

  Alidai kwamba padri huyo ametuhumiwa siku nyingi kwa kuwarubuni kimapenzi wanafunzi wanaokaa katika bweni lililopo Parokiani hapo, lakini hawakuwahi kupata uthibitisho wa kumchukulia hatua.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Omary Mganga alipoulizwa kuhusina na tukio alisema padri huyo tayari ameshatiwa mikononi mwa polisi na mara baada ya kukamilika kwa upelelezi huo atafikishwa mahakamani.

  CHANZO:
  NIPASHE
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Oh! Mungu wangu.
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Baba Paroko!

  Hata kondoo wako tena wanafunzi hauwaonei hata huruma?? Lol!
   
 4. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Dah! Hii imekaa vibaya. Inanikumbusha ya Nanihiii Kimaro.
   
 5. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2009
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mapadri wengi wamezidi kufanya uzinifu na watoto wadogo kwa kuwa hao ni rahisi kuwarubuni. Umefika wakati sasa wa kanisa kuacha kukaa kimya na kuwafukuza upadre. Mapadre wanaitwa baba, ni baba gani analala na mwanae!! Haya si ndiyo machukizo yaliyotajwa katika Biblia takatifu?

  Kuna suala la kuwaruhusu kuoa; hili sidhani kama ni suluhu kwani wengi wao wana vimada zaidi ya mmoja hivyo labda waruhusiwe kuoa zaidi ya mke mmoja. Maaskofu wao wanafanya nini? Waepusheni kondoo wa Bwana na chui waliovaa ngozi ya Mchungaji.

  Nashauri kanisa lisikimbilie kuwa na idadi kubwa ya mapadre bila kuangalia wito; wengi siku hizi wanakwenda katika upadre kama ajira tena ya maisha. Umefika wakati wa kuzingatia umri kama kigezo kimojawapo. Kijana wa miaka 28 unampa upadre na gari na fedha chungu nzima toka kwa wafadhili; unategemea azifanyie nini? Comeon Bishops, wakeup, kondoo wanazidi kupotea. Jiulize, ni wangapi wanakwenda kwa padre kuungama dhambi zao? Mnadhani sababu ni nini?

  Ni kwa sababu hawa mapadre tunagongana nao mitaani.
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Oooh no!!! Eeeh!! Sijui inakuwaje hapo....nguvu ya ziada itatumika kutupia hi taka chini ya uvungu kabla mambo hayajaharibika. Ohh!!!
  Tunarudi pale pale, tuache kuishi double standard life vinginevyo haya mambo tunayodhani tunafanya kwa siri yataendelea kutuadhiri
   
 7. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  At least this time its a girl...lol.. (dont get me wrong, anatakiwa ale mvua 30 akawaeleze ma nyampara kuhusu huyo mungu wake aone nayeye watakavyo mla ndogo.. MOFO!) Its a shame.
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  ooooh...
  Siamini hili...
  How comes Baba Padri doing a filthy thing like this?
  Hivi ndo kupagawa au? Naombea iwe proved beyond doubt kwamba si yeye...
   
 9. IronBroom

  IronBroom JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 524
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ''wote ni wezi ni kwa vile hatujakamatwa''.Aliwahi kusema Padre mmoja katika moja ya mahubiri yake yenye mvuto kwa wengi.Padre huyo alikuwa akihubiri katika seminari aliyosoma huyu mtuhumiwa wa ubakaji(acording to maelezo ya mwanafunzi) na kusababisha ujauzito kwa mwanafunzi(according to uongozi wa shule na mwanafunzi aliyepewa huo ujauzito).

  It is possible hasa katika jimbo hilo katoliki la Dodoma.I know Priests ambao walifikia hatua ya kuishi kabisa na wanawake( na kuzaa nao watoto)...one ended up committing suicide baada ya kusimamishwa kutoa huduma za kipadre. Wengine (wengi) wanao watoto...na inafahamika... Thanks to God Huyu Askofu 'mpya' anajitahidi sana kuwaadabisha kadiri anavyopata taarifa na evidence. I hope katika hili pia ataendelea na msimamo wake huohuo.

  MY PRAYER:HAKI ITENDEKE.
   
 10. M

  Maskini Mimi Member

  #10
  May 26, 2009
  Joined: Jun 25, 2008
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa maporoko kwa nini wasiruhusiwe wawe na wake so as to avoid kutia mimba watoto wetu.

  Akamatwe halafu ajzwe chupa huyo ....... ndiyo atajua raha ya kuwaharibu watoto wetu!
   
 11. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  eti baba padre..lol.. hawa watu wanafiki tuu. Sio yeye sasa mtoto adanganye ili nini.. DNA test, alafu baba padre anaenda kuwa anty Faza ukonga.. lazima awe mchuchu... wa manyampara.. wale 'small'... watu wanafiki wanatuharibia watoto.. tena skuizi wanaona wakike wameshaguswa guswa.. wanaharibu mkapa wakiume... sasa nini nini usichoamini hapo? Its a real shame, mi naombea huyo mtoto a-recover ki saikolojia na huyo faza akaliwe ndogo jela huko for 30 years. Amen
   
 12. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hawa maparoko kazi yao ni kula wale "kondoo walio nona tu". Japo wenye wake na wasio na wake lao ni moja, lakini bora waruhusiwe kuoa tu, japo wapunguze kidogo ili hata wake za waumini wapate mahali pa kupumulia. HAWACHOKI KUWA-UNGAMISHA WAUMINI WAO KWA KUWAPIGISHA GOTI.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...