Mwanafunzi askari chuo cha anga cha JWTZ ajiua

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,534
Mwanafunzi wa Chuo cha Anga (Skua) cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilichopo Kange jijini Tanga, Philip Fred (28) amejiua kwa kujipiga risasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paul aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kwamba tukio hilo ni la jana saa 1.15 usiku katika chuo hicho kilichopo kata ya Maweni nje kidogo ya jiji.

Alisema askari mwenye cheo cha Koplo mwenye namba MT 81627 alijiua wakati akiwa katika eneo la lindo chuoni hapo.

“Kimsingi chanzo cha kifo cha askari jeshi huyo bado hakijajulikana na imefahamika kwamba alikuwa ni mwanafunzi wa ‘Level one’ chuoni hapo na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa Bombo”, alisema Kamanda.

Chanzo: Mpekuzi

Jamani, ukimwona mtu ambaye mara nyingi anapenda kuwa peke yake mfuatilie kwa makini kwani anaweza kuwa na stress ambayo inaweza kumsababisha kujiua au kuua wenzake. Hata mtu ambaye ghafla anaanza kucheka sana aangaliwe pia kwa makini ni lazima patakuwa na jambo nyuma ya kicheko hicho.
 
poleni wafiwa vijana sijui wana shetani gani wanachukua maamuzi magumu kirahisi rahisi tuu bila hata kuwajali wazazi watakua katika hali gani ya mshtuko..mbaya sana hii
 
Jamani, ukimwona mtu ambaye mara nyingi anapenda kuwa peke yake mfuatilie kwa makini kwani anaweza kuwa na stress ambayo inaweza kumsababisha kujiua au kuua wenzake. Hata mtu ambaye ghafla anaanza kucheka sana aangaliwe pia kwa makini ni lazima patakuwa na jambo nyuma ya kicheko hicho.

Unamfata ukiwa na bullet proof?
 
Jamani, ukimwona mtu ambaye mara nyingi anapenda kuwa peke yake mfuatilie kwa makini kwani anaweza kuwa na stress ambayo inaweza kumsababisha kujiua au kuua wenzake. Hata mtu ambaye ghafla anaanza kucheka sana aangaliwe pia kwa makini ni lazima patakuwa na jambo nyuma ya kicheko hicho.
Kweli ndugu..Na pia tujifunze kutoa ushauri ulio bora kwa mtu aliyekata tamaa kabisaa.Maana sisi pia huwa chanzo cha haya mambo.Una mjambo umekukaa kooni unamfuta mtu wa karibu umjuze ili tu utue ulilo nalo.Unapewa majibu ambayo hupelekea kuanguka zaidi.
 
Umesema kweli kabisa. Hata kama hatakujibu ovyo anakwenda kuwatangazia watu wengine. Mbaya sana.
 
Inan
Umesema kweli kabisa. Hata kama hatakujibu ovyo anakwenda kuwatangazia watu wengine. Mbaya sana.
Inanikumbusha jamaa aliaachwa ghafla na hao ndugu zetu hawa.Muda ukapita haonekani,kati yetu akashtuka na kwenda kumcheki ndani.Kichwa chake kilipotea kabisa akawa yupo yupo tu.Sasa akaja kichaa mmoja kati yetu akamcheka saana jamaa saaana.Kati yetu mmoja wetu alimtimua jamaa huyo aliyekuwa akicheka,na taratibu akaanza kuingia ndani ya tatizo la jamaa kama pia liliwahi kumkuta.Walizungumza mengi sana na kila mwanaume (Vijana) walikuwa karibu na jamaa,kutoa magumu zaidi ya jamaa.Baada ya muda jamaa akaanza kurudi taratibu,.Akiwa chini ya kutazamwa kwa muda wa siku 3 hivi.Mpaka sasa yu hai na anashukuru tu hiyo siku.Sasa mfikirie yule aliyeanza kucheka hovyo hovyo.Matatizo yapo mengi sana hapa duniani.Ukiona kwako dogo kwa mwenzio ni zito kwa kuwa hatufanani kifrikra hata kidogo ila tu tunakubaliana na kuamua pamoja.
 
Back
Top Bottom