Mwanafunzi aliyesema "muhogo"

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Darasani kwetu alikuwepo mwanafunzi ambaye kwa kweli alikuwa mkali sana kwa masomo mengine yote isipokuwa Kemia. Ilipofika somo la Kemia yeye ndiyo ulikuwa muda wake wa kulala darasani. Siku moja mwalimu wa Kemia alikuwa anafundisha mambo ya chemical reactions na chemical equations. Baada ya kuzungumza kwakirefu aliuliza swali ambalo jawabu lake kwa kweli lilikuwa ni rahisi tu - Water (H2O).

Alimuuliza Chris; Chris alikuwa amelala na mtu wa nyuma yake alimshtua na yeye alisimama mara moja akizinduka toka usingizini. Hakujua kilichoulizwa na wala hakujua jawabu. Na kwa vile ndiye aliyekuwa smartest kid in the class aliangaza pembeni kuangalia kama kuna mtu angemsevu.

Mjanja mmoja akamnong'oneza..

"sema muhogo"

Kijana yule bila kufikiria lolote na akiwa na macho makavu kama kuku wa kukopa alirudia.

"Muhogo!!"

Darasa zima lilipuka kwa kicheko.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom