Mwanafunzi aliyempinga Mugabe akamatwa

Mwanafunzi aliyempinga Mugabe akamatwa

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu amechukuliwa na watu wasiojulikana, baada ya kuonyesha bango lililokuwa na maandishi ya kumtaka rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ajiuzulu
Bwana Mugabe alikuwa akiongoza hafla ya kufuzu kwa wanafunzi wa chuo kiku cha Sayansi na Teknolojia cha Bulawayo kilicho kusini mwa Zimbabwe wakati kundi la wanafunzi lilifanya maamdamano.

Advance Musoke aliakuwa mmoja wa wanafunzi 14 waliokuwa wakifuzu walioiunu mabango kupinga ukosefu wa ajira. Haijulikani ikiwa Rais Mugabe aliona mabango hayo.

Makomborero Haruzivishe, ambaye ni kiongozi wa wanafunzi aliiambia bbc kuwa wanaume wasiojulikana walimchukua bwana Musoke huku wengine wakifanikiwa kutoroka.

Maandamano ya kumpinga rais Mugabe na sera zake yamekuwa mengi wakati nchi inakabiliwa na hali mbaya ya uchumi.

Chanzo: BBC
 
Watu wa kitengo ktk kulinda waharifu sugu wa Afrika waliosababisha matatizo makubwa
 
Back
Top Bottom