Mwananchi wa chini
JF-Expert Member
- Jul 23, 2013
- 227
- 599
...................Na Mzee Yahya Msangi........................................
Mwaka 1997 nilikuwa mwanafunzimwaka wa pili chuo kikuu cha Ireland (University College Dublin). Nilikuwa mwanafunzi ngazi ya Masters kipindi hicho. Nikisomea Satellite Remote Sensing and Geographical Information Systems for Environmental Resource Management. Tuliuwa watanzania wawili mwenzangu nadhani sasa ni Senior Lecturer Open University Dar Es Salaam.
Ireland ni nchi rasmi ya kikatoliki kwa mujibu wa katiba yao. Lakini chokochoko za kuruhusu ushoga, utoaji mimba, ndoa za jinsi moja na uchafu mwingine zilikuwepo. Pale chuoni UCD palikuwa na chama cha mashoga. Mkifika wanafunzi wapya wanapitapita kujaribu kufanya usajili wa wanachama wapya! Hakika wanafunzi wengi wa kiafrika hawakutaka hata kuwasikiliza. Sikumbuki kuona mwanafunzi wa kiafrika aliojiunga nao.
Sasa kulikuwa na mazoea chuoni pale kuwaalika wakuu wa nchi kuja kuhutubia jumuia ya chuo kikuu. Kulikuwa na ka utamaduni kwa 'kuwachemsha' wakuu wa nchi kutoka Afrika. Ni mkuu mmoja tu niliona aliheshimiwa na kila mmoja. Huyu ni Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Hatukusumbuka sana kumpamba. Mimi nilikuwa Katibu wa Chama cha Watanzania wasomao UK na Republic of Ireland. Sikusumbuka sana kumpamba kwani wazungu wenye walisambaza matangazo kuwa the PRIDE OF AFRICA IS COMING!
Ikaja zamu ya Jongwe wa Zimbabwe. Naye alikuwa anaheshimika sana Ireland ila kipindi kaalikwa kukatokea kituko nchini mwake. Raisi wa Zimbabwe Reverend Canan akatuhumiwa kumlawiti mlinzi wake. Mugabe akalaani kitendo kile na kusema adhabu stahiki ni kifo. Hili likaamsha hasira ya mashoga wote UK na Ireland na Ulaya nzima! Wakajaa Dublin kumkabili Jongwe. Tokea airport wakamshikia mabango! Alipofika chuoni kuhutubia mabango yakajaa ya kumshtumu, kumdhihaki na hata kutmtukana. Mvunja haki za binadamu! Tukadhani jongwe atanyong'onyea! Tukamkaribisha kwanza kwenye klabu yetu ya wanafunzi wa Afrika. Tukaongea naye sana na kumpa tathmini yetu ya hali ilivyo. Chuo kikampangia aongelee kuhusu Mahusiano ya Kijamii na Uhuru!
Ndipo mkutano ukaanza. Ukumbini wamejaa tele mashoga toka pembe zote za ulaya. Wamevaa uniform zao za pink na bandama za rainbow. Jongwe akahutubia vyema na tukamshangilia sana! Ukaja muda wa maswali. Nafasi ya kwanza wakapewa mashoga. Kiongozi akamuuliza jongwe aeleze msimamo wake kuhusu mahusiano ya watu wa jinsi moja! Tuliona sura ya jongwe ilivyobadilika! Alighadhabika sana. Bila kupepesa macho akamjibu yule shoga: nadhani unataka kujua naukubali au naukataa ushoga nikwambie hivi ushoga hata mungu aliukataa na nikipata nafasi ya kumhukumu shoga nitampa adhabu moja tu - ya kifo! Alishangiliwa mno na waatoliki wa Ireland na sie waafrika. Kivumbi ikawa mashoga. Walitaka wasogee mbele ili wamshughulikie! Ulinzi ulikuwa mkali mno wakashindwa! Mugabe kwa jinsi alivyoudhika alikataa kuendelea kujibu maswali akaomba aondoke! Tulishangilia mno! JONGWEE, JONGWEEEE naye akitupungia mkono akaondoka zake ukumbini.
Jioni yake ilikuwa aondoke na AIR ZIMBABWE yake. Wakati wa kuondoka ndege ikaleta hitilafu ikabidi irudi kutua. Uwanjani pale mashoga walikuwepo! Waliposikia ndege imeshindwa kuondoka wakadai ni wa kuwa aliwatukana!
Raisi Magufuli kuwa kama JONGWE!