Mwanafunzi achinjwa kama kuku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi achinjwa kama kuku

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  HOFU imetenda kwenye Shule ya Msingi Living stone ya mchepuo wa Kiingereza, wilayani Njombe, baada ya mwanafunzi Doris Lutego (12), aliyetekwa ndani ya bweni wiki iliyopita kukutwa ameuawa kwa kuchinjwa kama kuku, mwili wake kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.
  Mauaji ya mwanafunzi huyo yametokea siku chache baada ya polisi kutoa taarifa ya kutoweka kwa mwanafunzi huyo, kutokana na watu wasiojulikana kumteka ndani ya bweni.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, alisema mwili huo uliokotwa Juni 13, mwaka huu majira ya asubuhi, kichwa kilikutwa kimetupwa Mtaa wa Nzerengete, huku kikiwa kimewekwa kwenye mkoba wa daftari wa mwanafunzi huyo.
  Mangala alisema kiwiliwili chake kilikutwa kimewekwa kwenye genge la biashara lililopo karibu na makazi ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kambarage, kilomita 10 kutoka eneo la shule hiyo.
  Awali, ilidaiwa mwanafunzi huyo alitekwa na watu wasiojulikana akiwa amelala baada ya kuvamia bweni la wasichana Juni 12, mwaka huu majira ya usiku na kutoweka naye, huku wakiacha jino na damu kwenye bweni.
  Kutokana na uchunguzi wa polisi, watu watatu wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
  Alitaja wanaoshikiliwa kuwa, wote ni wakazi wa Njombe, mkoani Iringa.
  Mangala alisema polisi inafanya uchunguzi wa kina kujua sababu za mauaji hayo ya kinyama, hasa yakishusisha mwanafunzi ambaye uchunguzi wa mwili wa marehemu unaonyesha kabla ya kuuawa, alipigwa na kitu kizito kichwani.
  Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sara Dumba, alisikitishwa na hali hiyo ambayo imesababisha hofu kwa wanafunzi wa shule hiyo na kwamba, wananchi wanapaswa kutulia wakati polisi wakiendelea na msako kubaini wahusika.
  "Serikali imesikitishwa na mauji haya ya kinyama, ninachoomba wananchi wawe watulivu kwa wakati huu polisi wanafanya uchunguzi kubaini wahusika ili hatua za kisheria zichukuliwe," alisema Dumba.
  Baadhi ya wananchi walitaka serikali kuhakikisha usalama wa shule zote ambazo zimekuwa zikiweka bwenini wanafunzi, ili kuepusha matukio ya mauaji.
  Augustino Wikesi, alisema kama shule hizo zingekuwa na ulinzi wa kutosha, mwanafunzi huyo asigetekwa usiku.

   
 2. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,538
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  binadamu kwa sasa tumegeuka wanyama wa mwituni? kwanini jaamani?hivi inakuwaje mtu amkate mwenzake shingo kama kuku
  ama kweli siku za mwisho zimefika r.i.p marehemu
   
 3. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,581
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  ni zaidi ya kusikitisha kwani umri huu sidhani kama anaweza kuwa na na visasi na mtu yoyote, hao wauaji wanyongwe tu na hakuna hukumu njingine itawafaa, nahisi hao wametumwa tu na ukiangalia unaweza kuta kuna mgogoro wa uhalali/umiliki wa wazazi juu ya huyo binti. RIP Doris
   
 4. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  This is too much.....Maisha ya Doris yalikuwa na maana kubwa kwa wazazi wake, ndugu zake na taifa kwa ujumla....
  ...chanzo cha mauaji haya kikijulikana tujuzane, japo hakuna sababu yoyote ya maana ya kupoteza maisha ya binti huyu....damu ya doris si tu inalia mbele za MUNGU kwa ajili ya wauaji wake lakini pia inaleta laana ktk taifa

  mix with yours

   
 5. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  inasikitisha sana, wakikamatwa wakabidhiwe kwa wananchi nao wawamalize. hawafai kukaa jela hao
   
 6. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,467
  Likes Received: 3,732
  Trophy Points: 280
  Masikini mtoto Doris
  Mungu ailaze roho ya marehemu peponi...Amina
   
 7. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Habari hii imenisikitisha sana... Heading yake kwenye gazeti mojawapo la leo SIJAIPENDA KABISA...
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  wameandikaje??binadamu tumekua kama wanyama!
   
 9. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,088
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli kama wauwaji wanakamatwa wanastahili mauaji mbele za umati,ni ajabu mtoto wa hivi kuuawa kimafia namna hii

  May Lord rest her soul in peace!
   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  taratibu mambo yanayotokea nchi za mbali yanaanza kutokea nyumbani kwetu. i miss them days,when i played inncocently, laughing and jumping kama kitoto cha ndama, worrying abt nothing! maskini watoto wangu...:A S 12:
   
 11. pangalashaba

  pangalashaba JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 1,089
  Likes Received: 885
  Trophy Points: 280
  r.i.p dorris. unaweza ukakuta bifu ni mzazi/wazazi na watu wengine. either wamedhulumiana au wameleteana fitina kazini.
   
 12. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  R.I.P. Doris,huenda ni visasi vya wazazi.Huu ni unyama wa hali ya juu sana.
   
 13. I

  IGO Member

  #13
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapana mkuu hata wanyama hawana hiyo tabia,nao hawatuelewi.
   
 14. M

  Morris john New Member

  #14
  Jun 15, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha na kutia simanzi kubwa sana ktk taifa letu Tanzania. Hayo majamaa nayo yauliwe hvyo2 kwn aliye ua kwa upanga naye auawe vivyo hivyo. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMINA!!!
   
 15. A

  Aine JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Jamani! Mungu atusamehe. Kwanza mtoto mwenyewe ana miaka 12! yaani hapo sioni kama kawakosea nini mtoto mdogo wa umri huo. RIP Doris na poleni wafiwa wote
   
 16. S

  Samkyjr JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haki za binadamu wanapinga binadamu kunyongwa lakini kwa mauaji ya namna hii jamani!!!
   
 17. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,122
  Likes Received: 6,606
  Trophy Points: 280
  Nimeumia sana, mtoto malaika kwani kakosa nini jamani, hamna hata huruma. EE MUNGU mlipie kwa kuwa ulisema ".............. kisasi ni juu yangu .........."
   
 18. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  da tunakoenda watanzania ni kubaya sana mana uyo mtoto jamani ana kosa gani? ngoja tusubiri vyombo vya dola vifanye kazi yake labda tutaja pata ukweli wa jambo lenyewe
   
 19. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Duhhhh!!!!!!!!! Bila shk hiyo viza tu.
   
 20. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  This is sad news.
   
Loading...