"Mwanadamu wa kawaida" huwezi kuelewa

TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
1,820
2,000
Mara nyingi nimekua nikiona watu wanaoleta mada ambazo wanadhani ni ngumu kueleweka (hasa jukwaa hili) hua wanapenda kutumia misemo kama "Kwa akili ya kawaida huwezi kuelewa" au "mtu wa kawaida hatanielewa" au utasikia "swala hili liko nje ya upeo wa akili za mwanadamu" (hasa mambo ya dini) n.k.

Mimi siku zote nimekua nikijiuliza "kama swala liko nje ya upeo wa akili ya mwanadamu, au haliwezi kueleweka kwa akili ya mwanadamu, huyo anaeliwasilisha yeye hua ametumia akili ya wapi kuweza kulielewa?"
 
Chimunguru

JF-Expert Member
May 3, 2009
10,583
2,000
Jitahidi kusoma vitabu, makala mbali mbali ili kupanua ufahamu wako. Mfano tunaamini kwamba sisi ndio binadamu wa kwanza kuishi hapa duniani. Lkn ukiwa mdadisi na kusoma vitabu na makala mbali mbali utakuja gundua kwamba kabla yetu kulikuwa na jamii iliyoendelea sana ilikwepo kabla yetu. Ndio hao waliojenga majumba makubwa makubwa ambayo tofali lake moja ni km behewa la treni. Hii jamii ya watu wakubwa Giants ilikuja teketetezwa wakati wa great floods au Gharika kuu. Nenda Mexico, Misri, Lebanon Syria, Iraq, India Japan utakuta hizo Megalithic structures zilizobakia.
Kwenye haya majengo utakuta picha zimechorwa za astronauts wa kale na ndiyo tecnolojia wana anga wa sasa wanatumia. Hayo majengo yalijengwa kwa mawe na si tofali km zetu hizi. Jiwe limekatwa vizuri kama wewe unavyoweza chonga kinyago cha mbao. Jiwe kubwa kama behewa la treni limetobolewa katikati, na kuchongwa vizuri. Technolojia hiyo bado hatuna.
Kwa hiyo kwa akili ya kukaririshwa tu vitabu vyetu hivi huwezi fikiria nje ya box
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
21,549
2,000
Mara nyingi nimekua nikiona watu wanaoleta mada ambazo wanadhani ni ngumu kueleweka (hasa jukwaa hili) hua wanapenda kutumia misemo kama "Kwa akili ya kawaida huwezi kuelewa" au "mtu wa kawaida hatanielewa" au utasikia "swala hili liko nje ya upeo wa akili za mwanadamu" (hasa mambo ya dini) n.k.

Mimi siku zote nimekua nikijiuliza "kama swala liko nje ya upeo wa akili ya mwanadamu, au haliwezi kueleweka kwa akili ya mwanadamu, huyo anaeliwasilisha yeye hua ametumia akili ya wapi kuweza kulielewa?"

Mara nyingi hao ni watu wanaojiona kwamba ni bora kuliko wengine Tu ndu Lisu type, lkn ni Wagonjwa wa akili, wengi wanaishi kwenye Dunia yao na wamepoteza uhalisia wa kinachoendelea Duniani.
 
Jurjani

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
18,618
2,000
Hahah kweli asee,.ndio maana wengine tukiona hayo maneno "kwa akili ya kawaida huwezi" tunapita kimyakimya tuu hatutaki kabisaa kujichosha,.muda mchache mambo mengi ya kufanya..
Inaonekana wewe ni muoga sana wa kufikiri mambo kiundani.

Unajua kuna lugha za kifani na lugha za kawaida.

Nakuja ....
 
Mother Confessor

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
17,108
2,000
Inaonekana wewe ni muoga sana wa kufikiri mambo kiundani.

Unajua kuna lugha za kifani na lugha za kawaida.

Nakuja ....
Ningekuwa muoga wa kufikiri kiasi hicho ningeweza kuvuka hata barabara kweli....?

Nimewaza kwa sauti tuu,.
 
mkorinto

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
17,407
2,000
Mabadiliko yoyote yale yalifanywa na watu ambao waliacha kufikiri kwa mazoea(akili za kawaida).

Kisa tu unaona jua linanyanyuka mashariki,kutua magharibi basi unahitimisha kwa akili za mazoea,jua linazunguka dunia.

Ukija kuambiwa tofauti na kuchanwa kwamba kwa akili za kawaida huwezi elewa unashangaa,how!!!
 
TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
1,820
2,000
Mimi nadhani wanamaanisha wasioelewa ni wale wenye uvivu tu wa kufikilia na kuchanganua mambo, Hii hali yao huwa ni uvivu na tabia ya kupuuzia lolote linaloonekana mbele yao. Huyu ndio Mwanadamu wa kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa mkuu mtu anapoleta mada na anaweka kabisa angalizo kwamba kitu hiki kwa akili ya binadamu wa kawaida hamuwezi kuelewa, wakati binadamu wote tuna tumia akili hii hii ya binadamu, anakua ana maana gani?
 
TheChoji

JF-Expert Member
Apr 14, 2009
1,820
2,000
Mabadiliko yoyote yale yalifanywa na watu ambao waliacha kufikiri kwa mazoea(akili za kawaida).

Kisa tu unaona jua linanyanyuka mashariki,kutua magharibi basi unahitimisha kwa akili za mazoea,jua linazunguka dunia.

Ukija kuambiwa tofauti na kuchanwa kwamba kwa akili za kawaida huwezi elewa unashangaa,how!!!
Kwahiyo ukielewa kitu unakua hujatumia akili ya kawaida?
 
Jurjani

JF-Expert Member
Apr 6, 2018
18,618
2,000
Mara nyingi nimekua nikiona watu wanaoleta mada ambazo wanadhani ni ngumu kueleweka (hasa jukwaa hili) hua wanapenda kutumia misemo kama "Kwa akili ya kawaida huwezi kuelewa" au "mtu wa kawaida hatanielewa" au utasikia "swala hili liko nje ya upeo wa akili za mwanadamu" (hasa mambo ya dini) n.k.

Mimi siku zote nimekua nikijiuliza "kama swala liko nje ya upeo wa akili ya mwanadamu, au haliwezi kueleweka kwa akili ya mwanadamu, huyo anaeliwasilisha yeye hua ametumia akili ya wapi kuweza kulielewa?"
Ningekuwa muoga wa kufikiri kiasi hicho ningeweza kuvuka hata barabara kweli....?

Nimewaza kwa sauti tuu,.
Kuvuka bara bara ni jambo la kimaumbile tu bibie kama ilivyo kwa mtoto hawezi kufundishwa kunyonyw au kuweka tonge mdomoni.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom