"Mwanadamu wa kawaida" huwezi kuelewa

Hapana mkuu. Asilimia kubwa ya kile tunachoita akili hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine hivyo watu watofautiana kwenye uwezo kufikiri toka utotoni.
Lakini uko sahihi kwamba watu wengi wana kiwango cha kawaida cha akili(average intelligence) na tofauti ipo kwenye kuindeleza akili au kuongezea uwezo wa mtu wa kufikiri kwa kujifunza. Zingatia pia kuwa wale wanazaliwa na kiwango cha juu cha akili wana uwezekano mkubwa zaidi wa kuendeleza akili zao.
Mimi nafikiri tukubaliane kwamba binadamu wote tuna akili za kawaida. Labda tofauti inakuja pale ambapo mtu umeamua kuinoa akili yako kwenye eneo fulani kwahiyo unakua unajua zaidi kuhusu eneo hilo, ila sio kwamba una akili isiyo ya kawaida.
 
Chief ngoja nikupe ufafanuzi juu ya kauli hii au kauli hizo.

Katika kuwasilisha mambo lugha huwa jambo la msingi sana. Lugha imegawanyika katika sehemu kuu mbili,kuna lugha ya kifani na lugha ya kawaida ya mazungumzo tunayo zungumza,mathalani leo hii huwezi kutumia lugha ya kifasihi ya ndani kwa mwananchi anae hitaji lugha nyepesi sana. Haoa watu wa fasihi huwa wanasema mtu lazima uzungumze jambo kulingana na hadhira ikoje.

Sasa swali la msingi ni wakati gani jambo huwa gumu kueleweka ? Kabla ya hapo,akili ya mwanadamu iko tayari kupokea chochote endapo kikiwekwa katika hali nyepesi na kueleweka.

Sababu za mada au jambo kutokueleweka.
1. Lugha,hii ni sababu ya msingi sana ambayo wawasilishaji wa mada wanatakiwa kulizingatia,yaani muwasilishaji mada anatakiwa aangalie mahitaji ya hadhira.

2. Ufasaha wa muwasilishaji,hili pia ni jambo la msingi. Wawasilishaji wametofautiana vipawa na namna ya uwasilishaji jambo,hili si jambo geni. Leo unaweza kuelezewa maana ya "Elimu" na msomi fulani usielewe na ukaelezewa maana ya "Elimu" na msomi mwingine ukaelewa na wala usihitaji kupewa mifano.

3. Umakini wa msikilizaji,kuna watu wengine huwa wakielezewa jambo wao wanafanya mengine na mfano wake,huwa tunasema hivi mshika mawili moja hushika njia.

4. Kutokuwa na ufahamu wa jambo linalowasilishwa. Hapa inaingia kwa muwasilishaji na hadhira.

Angalizo : Akili ya mwandamu ni hii hii ambayo wewe ubayo na mimi ninayo,tofauti zetu ni katika juhudi na kufikiria sana,yaani matumizi ya akili.

Nipo ....
Well Explanation. Zurri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jitahidi kusoma vitabu, makala mbali mbali ili kupanua ufahamu wako. Mfano tunaamini kwamba sisi ndio binadamu wa kwanza kuishi hapa duniani. Lkn ukiwa mdadisi na kusoma vitabu na makala mbali mbali utakuja gundua kwamba kabla yetu kulikuwa na jamii iliyoendelea sana ilikwepo kabla yetu. Ndio hao waliojenga majumba makubwa makubwa ambayo tofali lake moja ni km behewa la treni. Hii jamii ya watu wakubwa Giants ilikuja teketetezwa wakati wa great floods au Gharika kuu. Nenda Mexico, Misri, Lebanon Syria, Iraq, India Japan utakuta hizo Megalithic structures zilizobakia.
Kwenye haya majengo utakuta picha zimechorwa za astronauts wa kale na ndiyo tecnolojia wana anga wa sasa wanatumia. Hayo majengo yalijengwa kwa mawe na si tofali km zetu hizi. Jiwe limekatwa vizuri kama wewe unavyoweza chonga kinyago cha mbao. Jiwe kubwa kama behewa la treni limetobolewa katikati, na kuchongwa vizuri. Technolojia hiyo bado hatuna.
Kwa hiyo kwa akili ya kukaririshwa tu vitabu vyetu hivi huwezi fikiria nje ya box
URE TOTALLY WRONGLY
 
URE TOTALLY WRONGLY
Angalia hizo Megalithic structures nani anaweza beba tena kujengea nyumba kwa Mwanadamu wa kawaida?
FB_IMG_1550494000746.jpg
FB_IMG_1550493992772.jpg
 
Angalia hizo Megalithic structures nani anaweza beba tena kujengea nyumba kwa Mwanadamu wa kawaida?View attachment 1025662View attachment 1025664
Kosa kubwa mnalodanganya watu wa siku hizi

Ni,kuona binadamu wa kale walikuwa hawana ujuzi na maarifa
Na hizi Ni propaganda za watu zenye agenda ya Siri katika kukamilisha ya kwao

Hizi mnazoziita technology au science ni copy&paste ya Zama za watu wa kale

WATU WA KALE WALIKUWA NA AKILI NA UJUZI MWINGI KULIKO WA SASA.

Endeleeni kukalilishwa,wakati hata hao kina
Eistein,Netwon, Pythagoras etc
walifanya ku copy&ku paste
 
Back
Top Bottom