Best Daddy
JF-Expert Member
- Apr 2, 2019
- 769
- 1,292
Natumaini wote ni wazima wa afya, ila kama mwenye matatizo kiafya basi Mwenyezi Mungu(Allah) au kwa imani yako ikusaidie upone.
Basi, kuelekea kwenye Uzinduzi wa michuano mikubwa zaidi ya Vilabu barani Africa (AFL) kumekuwa na hisia tofauti tofauti katika mechi hiyo ya Uzinduzi ambayo itaikutanisha Miamba ya Afrika Masharikia (Simba) vs Al Ahly (Vigogo wa Afrika)
Katika mlengo wa Soka, hizi hisia tofauti zimetokana na baadhi ya mashabiki wa Simba na wale wapenda Soka kufurahishwa na si tu uwepo wa Simba katika mashindanio hayo, bali kuwa sehemu ya uzinduzi wa mashindano hayo ambayo yatahudhuriwa na viongozi wakubwa kutoka FIFA na wale wa CAF.
Lakini, kuna kundi la pili la mashabiki na viongozi lisilo furahishwa na hili, wazi limeonesha chuki kubwa ya uwepo wa Simba, pia kupewa thamani kubwa ya kuwa sehemu ya uzinduzi wa Mashindano hayo. Hili kundi linatumia nguvu kubwa sana kuichafua Simba, kudhihaki mashindano na ajenda nyingi ili kushusha thamani ya hili linalofanyika. Sio jambo zuri hasa kwa watu wenye akili timamu. Tuishie hapo, hii sio mada ya leo.
Ila nimekuja kutoa lai kwa Wanasimba ya kuwa ipo siku Yanga atapita katika njia anazozipita Simba au atapata mafanikio kama ya Simba, aisee hapatakalika hapa Tanzania.
Simba ni Timu pekee kutoka Tanzania imecheza fainaliya CAF Champions League(ikifahamika hivyo kwa sasa) mwaka 1974, ila naona mashabiki hawana shida na historia hiyo, Maisha yanaendelea.
Simba imecheza Fainali 1993 ila historia hii ilikufa, hadi pale Yanga alipofika fainali msimu ulipopita, Japo historia ipo ila mtaani wao wanajinasibu kama ndiyo timu pekee kufika Fainali. Wanasimba wamekubali, Maisha yanaendelea.
Simba ni timu peke iliyopo katika 10 bora ya Vilabu Afrika, ila tunaulizwa inatusaidia nini? Tumekubali maisha yanaendelea.
Tuna wachezaji, ambao wenye skills na bora Tanzania lakini hatupigi kelele na kuwapa majina ya ukuu wao, Mfano Chama, Sakho. ila wao wamepata mchezaji angalau anaweza kutuliza mpira na Skills kidogo, Pacome, Tayari anaitwa Zidane(Zizou).
Simba ni timu pekee imepata nafasi ya Kucheza na Sevilla, ikaweza kufunga goli nne, ila hata haikuwa issue. Maisha yanaendelea.
Leo Simba imepata nafasi ya Kushiriki AFL, timu pekee Tanzania ila bado kwa wanaSimba kama sio issue, hata furaha yako haiumizi watu wengine. Maisha yanaendelea. Assume Yanga ingepata nafasi hii?
Ukitoa Viongozi wakubwa watakao hudhuria , Ila umepata nafasi ya kushuhudiwa na Arsene Wenger, kwako hata sio issue. Tunakumbuka alikuja hapa Pisto Mosimane alionekama kama ni Kocha bora duniani( Kocha ka dunia).
Sijui ni ukomavu katika soka, akili nyingi au dharau zetu, ila assume haya mafanikio yangekua Yanga? Kumbe hayo ni mafanikio ya kipekee.
Japo inaweza chukua muda mrefu sana au isitokee, Ila Siku ikitokea Yanga amepata mafanikio ya kipekee ambayo Simba hajawahi fikia, Tanzania haitakua sehemu ya amani tena kwa Mashabiki wa Simba.
Tafadhari cheka kwa uhuru wakati bado meno yapo.