Pole sana mkuu Azikiwe,
Mi niko huku ughaibuni maeneo ya Asia, usafiri wa pikipiki ni moja ya usafiri unaotumiwa na karibu kila nchi na kwa kila mwananchi huku, kuna piki piki nyingi sana huku, lakini ajali za mara kwa mara kama Dar hazipo. Watu wanaheshimiana, wanajaliana lakini kwetu bwana madereva wenye magari ndo wenye barabara. Na mwenye gari akiwa nalo kubwa zaidi ndo mwenye bara bara haswa, i hate this basi tu!. Hii inatokana na mfumo mbovu wa utozwaji faini ya makosa barabarani, leseni nazo zinatolewa kiholela kama wauza michicha.
Nachotaka kusema hapa ni kuwa, kuna haja ya kuangalia upya mifumo na sheria za nenda kwa usalama barabarani ili watu tuheshimiane na tuweze kuwa na amani barabarani.
Once again, Get well soon brother!! hakika mungu yupo, utapona mkuu.