Mwambieni Mh, Jenister Muhagama na Abdallah Possy

Mwambieni Mh, Jenister Muhagama na Abdallah Possy

kokakola

Member
Joined
Nov 25, 2015
Posts
30
Reaction score
17
Kwa niaba ya vijana wenzangu wengi naomba nikusumbue kidogo. Naomba ukamuonyeshe hili JIPU ndugu waziri wa kazi vijana na ajira ( Mh, Jenister Muhagama ) na naibu waziri ( Mh, Abdallah Possy )

Pengine wao wanaweza wasiione hii post na kuisoma maana sina uhakika kwamba wapo humu JF.

Tafadhari nenda kamwambie kwamba ule mfumo wa kampuni kuwa ndani ya kampuni bado upo hadi sasa na unatuumiza mno vijana. Mwaka juzi bungeni liliongelewa hili swala. Unakuta kampuni kama Cocacola ambapo ndani yake iliiweka tena kampuni nyingine kwa ajili ya kuwasimamia vibarua. Kampuni hiyo iliyowekwa ilikuwa ni ERO LINK. Kwahiyo kwenye malipo Cocacola alimlipa ERO LINK kisha ERO LINK ndo anakuja kunilipa Mimi kibarua. Shida ni kwamba malipo aliyopewa ERO LINK ili anilipe ni tofauti kabisa na aliyonilipa. Unatakiwa upewe laki tatu si ajabu ukapewa laki na nusu au na sitini. Ukimwambia Cocacola ( HR ) watakuambia mwambie ERO LINK akupe pesa inayostahili maana hiyo anayokulipa sisi hatukukubaliana akulipe hivyo.

Baada ya mjadala bungeni hatimaye waziri wa kazi na ajira wa baraza lililopita ( la raisi mstaafu Jakaya Kikwete ) akaagiza utaratibu huu wa kampuni kuwa ndani ya kampuni nyingine ufe na kampuni zote za mtindo huu ikiwemo ERO LINK ziondoke. Akaagiza wafanyakazi ( vibarua ) wote wawe chini ya kampuni husika.

Kwa hapa kwenye kiwanda cha Cocacola kilichopo Mikocheni Dar es salaam kweli ERO LINK waliondoka ila cha kushangaza baada ya muda mfupi ikaja kampuni nyingine inaitwa CHAGUO SERVICES & CONSULTANTS LTD ambayo ndo ipo hadi muda huu. Hawa nao ni kama ERO LINK tu. Wanatunyonya mno. Kinachotolewa na Cocacola sicho anachotupa chaguo. Ukiumwa utajitibu mwenyewe. Ukienda likizo HUPEWI HATA SENTI. Hakuna motisha wala posho. Arafu ukijifanya kulalamika wanakufukuza kazi mara moja.

Wakija wakaguzi wa Cocacola ( oditors ) ukiwaambia malalamiko yako na ya wengine nakuapia unafukuzwa kazi maana wanasema eti unawachongea. Kwa hiyo vijana hapa tunaburuzwa tu. Tunafanya kazi ngumu mno ambayo kukatwa na chupa ishaanza kuwa kawaida tu. Hata ukipata ajari ya kukanyagwa na folk lift unapewa tu huduma ya kwanza kisha wanakwambia urudi nyumbani kujitibu mwenyewe ukipona ndo utarudi kazini.

Kampuni ya Cocacola yenyewe imeweka bima kwa waajiliwa wao tu. Vibarua au wale walioajiliwa na Chaguo hakuna mwenye bima hata mmoja.

Kwa mujibu wa sheria kama sikosei kibarua anatakiwa afanye kazi kwa kipindi cha miezi sita tu baada ya hapo anatakiwa aajiliwe. Lakini hapa Cocacacola kwanza ltd ( Mikocheni -Dar es salaam ) watu tuna miaka zaidi ya nane bado tu vibarua. Mwambieni Mh waziri kwamba yupo MTU hapa ana miaka 15 kazini na bado hadi leo ni kiabarua.

Kuna boss Fulani wa Cocacola aliwahi kutuambia kwamba kampuni ya Cocacola iliiweka kampuni ya Chaguo au ero link pamoja na Ik kipindi cha nyuma ili tu kuikwepa hiyo sheria ya mtu kuajiriwa baada ya miezi sita. Kwahiyo kibarua ukienda Cocacola (HR) kulalamika watakuambia sisi wewe HATUKUJUI, sisi tunaijua kampuni ya Chaguo na ndiyo tulioiajiri. Daah inauma sana jamani.

Mwambieni muheshimiwa waziri kwamba kampuni kama ERO LINK , Chaguo na nyinginezo nyingi ni MAJIPU. Mwambieni ayakamue kwa kuziondoa kabisa.

Tafadharini sana jamani. Mfikishieni hayo muheshimiwa waziri Jenister Muhagama na naibu wake Abdallah Possy. Lakini hata muheshimiwa waziri mkuu natamani pia angeliona hili.

#Hapa kazi tu# Sawa, lakini unyonyaji na ujanja ujanja wa baadhi ya kampuni unatuumiza mno vijana.
 
Nimeupenda huu utaratibu wa kila eneo kuonyesha wapi jipu lilipo na vile linasumbua, ili kuwapa urahisi watumbuaji wajue mahali pa kuanzia!
 
hii ishu inasikitisha sana hasa kwa kampuni ambayo tunaambiwa inamilikiwa na mzawa....sipati picha ingekuaje kama mmiliki wa kampuni hiyo angekua ni mwenye asili ya kiasia..
Double standards....
 
Dah, hii ni Aibu kwa yule anayejiita mzawa kuconspire kuwaumiza wananchi wanyonge, Tunamuomba mheshimiwa Waziri Mhagama akomae na dhulma hii ili wananchi wa kipato cha chini wasidhulumiwe nguvu na jasho lao.
 
Hii kampuni ya Coca Cola ni ya nani mmiliki wake?
 
Poleni sana ingawa upo nchi nyingi duniani huu mfumo, ni employment agency hao ambao wanasubiri waombwe wafanyakazi nao hupeleka kwa maelewano ya bei kwa kila kazi.

Hiyo inamfanya mwenye kiwanda akwepe vitu vingi ambapo mfanyakazi angepata kama angeajiriwa moja kwa moja kama overtime, likizo, bima, mshahara wa juu nk.

Hii inamfanya employment agency apate hela nyingi zaidi akiwa amekaa ofisini tu na kusubiri vijana wanaohangaika kupata mshahara mzuri kwenye kampuni kubwa kubwa.

Inasikitisha kweli na ndio maana hawa agents wanashika nafasi ya tatu kwa biashara inayolipa duniani baada ya estate agents.
 
Mvaa suruali za ugoko kila mada ye anaichukulia kidini au kikabila.

✅ Huo mchezo upo sana hakuna kiongozi wizarani ambaye hajui,wanajua sana na wapo kwenye payroll zao,kampuni ndani ya kampuni ni jipu na Michezo yote ipo engineered na HR nao wana % zao.
 
Daah hili km JIPU basi ni la KWAPA au kwenye mfereji wa Makalio
 
Mvaa suruali za ugoko kila mada ye anaichukulia kidini au kikabila.

✅ Huo mchezo upo sana hakuna kiongozi wizarani ambaye hajui,wanajua sana na wapo kwenye payroll zao,kampuni ndani ya kampuni ni jipu na Michezo yote ipo engineered na HR nao wana % zao.
Mkuu huu utaratibu uko duniani kote na tena nchi zilizoendelea za Ulaya ndio mtindo wa maisha. Mimi nilipokuwa nasoma nimefanya kazi sehemu mbalimbali kwa kupelekwa na hizi kampuni za uwakala. Mwenye kampuni ya Coca Cola hawezi kulaumiwa hata kidogo. Mimi nadhani tatizo lipo kwenye mkataba kati ya kibarua na hizi kampuni za uwakala i.e. labda Tanzania hao mawakala wanawapa mshahara mdogo sana. Unapoajiriwa na kampuni za uwakala usianze kuangalia kampuni mama inamlipa nini au wale wafanyakazi wa kampuni mama wanalipwa nini kwani utapata vidonda vya tumbo haraka. Cha msingi na cha kusisitiza ni hizi kampuni za uwakala kuwalipa hao vibarua kulingana na viwango vya serikali.
 
Kijana utaratibu huu ni zao la mfumo Wa uchumi wa kibepari, unatumika na umekubalika sehemu nyingi dunani. Ni njia moja wapo inayotumika na waajiri kupambana na migogoro na madai ya wafanyakazi.
Siasa ya Ujamaa ilizlisha wafanyakazi waliokua wanadai sana haki lakini hawatimizi wajibu wao. wanalipwa hata bila kuzalisha. kazi ya kufanywa na mtu mmoja wanaajiliwa 10. matumizi yanakuwa makubwa pasipo uzalishaji Wa tija.

Mtindo huu umeokoa pesa nyingi serikalini zilizokuwa zikiibiwa kwa wahudumu na manunuzi hewa. Haiwaajili tena wafanya usafi wame - lease kampuni, wapishi majeshini ni kampuni
inalipwa waajiliwa wanakula kwa kuponi.
 
Poleni sana ingawa upo nchi nyingi duniani huu mfumo, ni employment agency hao ambao wanasubiri waombwe wafanyakazi nao hupeleka kwa maelewano ya bei kwa kila kazi.

Hiyo inamfanya mwenye kiwanda akwepe vitu vingi ambapo mfanyakazi angepata kama angeajiriwa moja kwa moja kama overtime, likizo, bima, mshahara wa juu nk.

Hii inamfanya employment agency apate hela nyingi zaidi akiwa amekaa ofisini tu na kusubiri vijana wanaohangaika kupata mshahara mzuri kwenye kampuni kubwa kubwa.

Inasikitisha kweli na ndio maana hawa agents wanashika nafasi ya tatu kwa biashara inayolipa duniani baada ya estate agents.

N'kuu umeongea point chana. Mama Muhagama angefanya tu kuchaidia vijana
 
Nashauri anzisheni chama cha wafanyakazi vibarua wa cocacola ili mpambane na huyo dalali wa ajira vinginevyo sauti ya mmoja haifiki kokote. Kukaa miaka 15ya kazi huku ukiendelea kunyonywa na wewe mwenyewe ukiwa unatambua kuwa unanyonywa ni wendawazimu
 
Kuzikomesha kwa mazingira ya sasa ni vigumu

Mfumo huu upo sio tu private sector lakini hata taasisi binafsi unapoamua kuchukua kampuni binafsi kusimamia baadhi ya majukumu ndani ya taasisi nyingine. Hapa zinaingia kampuni kama hizo na zile za ulinzi, usafi, huduma za kisheria n.k.

Inasaidia kuipunguzia taasisi inayoajiri taasisi nyingine mzigo wa usimamizi wa kundi la wafanyakazi na badala yake yenyewe inabaki na kazi tu ya kusimamia mkataba husika....

Mfumo huu ukisimamiwa vizuri humpunguzia mteja (kampuni inayoajiri kampuni nyingine) kazi nyingi na jukumu kubwa la usimamizi na huwa na manufaa/matokeo mazuri sana
 
Reginald Mengi, kila siku unajifanya kulia lia una uchungu unafanya mzalendo kumbe kampuni yako inafanya ushenzi huu kwa Watanzania siku ukipewa kitalu cha gesi itakuwaje.
 
Back
Top Bottom