Mwambieni Mh, Jenister Muhagama na Abdallah Possy

Mzee Mengi ni mnafiki sana sijui ata hao wazawa anaopigania maslahi yao akijionyesha kwenye taarifa ya habari itv ni kina nani wakati wazawa ndio awa na anawanyanyasa shenz kabisa.
 
Andika rasmi uitume kwake yeye mwenyewe
 
Kwa niaba ya vijana wenzangu wengi naomba nikusumbue kidogo. Naomba ukamuonyeshe hili JIPU ndugu waziri wa kazi vijana na ajira ( Mh, Jenister Muhagama ) na naibu waziri ( Mh, Abdallah Possy )

Pengine wao wanaweza wasiione hii post na kuisoma maana sina uhakika kwamba wapo humu JF.

Tafadhari nenda kamwambie kwamba ule mfumo wa kampuni kuwa ndani ya kampuni bado upo hadi sasa na unatuumiza mno vijana. Mwaka juzi bungeni liliongelewa hili swala. Unakuta kampuni kama Cocacola ambapo ndani yake iliiweka tena kampuni nyingine kwa ajili ya kuwasimamia vibarua. Kampuni hiyo iliyowekwa ilikuwa ni ERO LINK. Kwahiyo kwenye malipo Cocacola alimlipa ERO LINK kisha ERO LINK ndo anakuja kunilipa Mimi kibarua. Shida ni kwamba malipo aliyopewa ERO LINK ili anilipe ni tofauti kabisa na aliyonilipa. Unatakiwa upewe laki tatu si ajabu ukapewa laki na nusu au na sitini. Ukimwambia Cocacola ( HR ) watakuambia mwambie ERO LINK akupe pesa inayostahili maana hiyo anayokulipa sisi hatukukubaliana akulipe hivyo.

Baada ya mjadala bungeni hatimaye waziri wa kazi na ajira wa baraza lililopita ( la raisi mstaafu Jakaya Kikwete ) akaagiza utaratibu huu wa kampuni kuwa ndani ya kampuni nyingine ufe na kampuni zote za mtindo huu ikiwemo ERO LINK ziondoke. Akaagiza wafanyakazi ( vibarua ) wote wawe chini ya kampuni husika.

Kwa hapa kwenye kiwanda cha Cocacola kilichopo Mikocheni Dar es salaam kweli ERO LINK waliondoka ila cha kushangaza baada ya muda mfupi ikaja kampuni nyingine inaitwa CHAGUO SERVICES & CONSULTANTS LTD ambayo ndo ipo hadi muda huu. Hawa nao ni kama ERO LINK tu. Wanatunyonya mno. Kinachotolewa na Cocacola sicho anachotupa chaguo. Ukiumwa utajitibu mwenyewe. Ukienda likizo HUPEWI HATA SENTI. Hakuna motisha wala posho. Arafu ukijifanya kulalamika wanakufukuza kazi mara moja.

Wakija wakaguzi wa Cocacola ( oditors ) ukiwaambia malalamiko yako na ya wengine nakuapia unafukuzwa kazi maana wanasema eti unawachongea. Kwa hiyo vijana hapa tunaburuzwa tu. Tunafanya kazi ngumu mno ambayo kukatwa na chupa ishaanza kuwa kawaida tu. Hata ukipata ajari ya kukanyagwa na folk lift unapewa tu huduma ya kwanza kisha wanakwambia urudi nyumbani kujitibu mwenyewe ukipona ndo utarudi kazini.

Kampuni ya Cocacola yenyewe imeweka bima kwa waajiliwa wao tu. Vibarua au wale walioajiliwa na Chaguo hakuna mwenye bima hata mmoja.

Kwa mujibu wa sheria kama sikosei kibarua anatakiwa afanye kazi kwa kipindi cha miezi sita tu baada ya hapo anatakiwa aajiliwe. Lakini hapa Cocacacola kwanza ltd ( Mikocheni -Dar es salaam ) watu tuna miaka zaidi ya nane bado tu vibarua. Mwambieni Mh waziri kwamba yupo MTU hapa ana miaka 15 kazini na bado hadi leo ni kiabarua.

Kuna boss Fulani wa Cocacola aliwahi kutuambia kwamba kampuni ya Cocacola iliiweka kampuni ya Chaguo au ero link pamoja na Ik kipindi cha nyuma ili tu kuikwepa hiyo sheria ya mtu kuajiriwa baada ya miezi sita. Kwahiyo kibarua ukienda Cocacola (HR) kulalamika watakuambia sisi wewe HATUKUJUI, sisi tunaijua kampuni ya Chaguo na ndiyo tulioiajiri. Daah inauma sana jamani.

Mwambieni muheshimiwa waziri kwamba kampuni kama ERO LINK , Chaguo na nyinginezo nyingi ni MAJIPU. Mwambieni ayakamue kwa kuziondoa kabisa.

Tafadharini sana jamani. Mfikishieni hayo muheshimiwa waziri Jenister Muhagama na naibu wake Abdallah Possy. Lakini hata muheshimiwa waziri mkuu natamani pia angeliona hili.

#Hapa kazi tu# Sawa, lakini unyonyaji na ujanja ujanja wa baadhi ya kampuni unatuumiza mno vijana.

Jiajiri ndo suluhisho
 
Hiyo ni kawaida sana mkuu,hapo coca cola wame outsourced kazi zingine,hivyo Chaguo ni kama contractor,chamsingi Chaguo inatakiwa ibanwe na serikali hili ifuate masharti na sheria za ajira nchini.Hawa jamaa walitumia vizuri sana udhaifu wa serikali ya kikwete kuwanyonya watu,ikishindikana pelekeni mgogoro wa kimslahi CMA, Labour court au kwa wizara husika.
 
Mkuu huu utaratibu uko duniani kote na tena nchi zilizoendelea za Ulaya ndio mtindo wa maisha. Mimi nilipokuwa nasoma nimefanya kazi sehemu mbalimbali kwa kupelekwa na hizi kampuni za uwakala. Mwenye kampuni ya Coca Cola hawezi kulaumiwa hata kidogo. Mimi nadhani tatizo lipo kwenye mkataba kati ya kibarua na hizi kampuni za uwakala i.e. labda Tanzania hao mawakala wanawapa mshahara mdogo sana. Unapoajiriwa na kampuni za uwakala usianze kuangalia kampuni mama inamlipa nini au wale wafanyakazi wa kampuni mama wanalipwa nini kwani utapata vidonda vya tumbo haraka. Cha msingi na cha kusisitiza ni hizi kampuni za uwakala kuwalipa hao vibarua kulingana na viwango vya serikali.

Mod, can you serve use with a like button? Pia hiyo inaongeza tija zaidi, imagine kampuni ingekuwa moja, mpaka wainzi, usafi wingine kupamba tu! Hizo ni outsourced kwa faida mbili, moja kampuni hiyo ndogo inapewa uwezo wa kutoa ajira za kutosha, pili, kulipa kodi stahiki. Al Muhimu ni kujadili vizuri mikataba na kuhakikisha wanalipwa kama walivyo ahuidi
 
Poleni sana ingawa upo nchi nyingi duniani huu mfumo, ni employment agency hao ambao wanasubiri waombwe wafanyakazi nao hupeleka kwa maelewano ya bei kwa kila kazi.

Hiyo inamfanya mwenye kiwanda akwepe vitu vingi ambapo mfanyakazi angepata kama angeajiriwa moja kwa moja kama overtime, likizo, bima, mshahara wa juu nk.

Hii inamfanya employment agency apate hela nyingi zaidi akiwa amekaa ofisini tu na kusubiri vijana wanaohangaika kupata mshahara mzuri kwenye kampuni kubwa kubwa.

Inasikitisha kweli na ndio maana hawa agents wanashika nafasi ya tatu kwa biashara inayolipa duniani baada ya estate agents.
Tatizo sheria ya kazi inaruhusu nadhani ukisoma kifungu kama sikosei cha 22
 
Mod, can you serve use with a like button? Pia hiyo inaongeza tija zaidi, imagine kampuni ingekuwa moja, mpaka wainzi, usafi wingine kupamba tu! Hizo ni outsourced kwa faida mbili, moja kampuni hiyo ndogo inapewa uwezo wa kutoa ajira za kutosha, pili, kulipa kodi stahiki. Al Muhimu ni kujadili vizuri mikataba na kuhakikisha wanalipwa kama walivyo ahuidi
Hizi kampuni ni za kinyonyaji tu. Zimeshanyonya sana watu.Bora ziondolewe tu kabisa. Kisha wafanyakazi wawe chini ya kampuni husika.
 
Ni kweli ndugu, hiyo ni moja ya njia ya kusaidia, ingine ni kuhakikisha hao wanatekeleza matakwa ya mikataba yao, huwa wanaandika kiwango ambacho wanamlipa kila mfanyakazi lakini wanafanya kinyume.
 
Kwa niaba ya vijana wenzangu wengi naomba nikusumbue kidogo. Naomba ukamuonyeshe hili JIPU ndugu waziri wa kazi vijana na ajira ( Mh, Jenister Muhagama ) na naibu waziri ( Mh, Abdallah Possy )

Pengine wao wanaweza wasiione hii post na kuisoma maana sina uhakika kwamba wapo humu JF.

Tafadhari nenda kamwambie kwamba ule mfumo wa kampuni kuwa ndani ya kampuni bado upo hadi sasa na unatuumiza mno vijana. Mwaka juzi bungeni liliongelewa hili swala. Unakuta kampuni kama Cocacola ambapo ndani yake iliiweka tena kampuni nyingine kwa ajili ya kuwasimamia vibarua. Kampuni hiyo iliyowekwa ilikuwa ni ERO LINK. Kwahiyo kwenye malipo Cocacola alimlipa ERO LINK kisha ERO LINK ndo anakuja kunilipa Mimi kibarua. Shida ni kwamba malipo aliyopewa ERO LINK ili anilipe ni tofauti kabisa na aliyonilipa. Unatakiwa upewe laki tatu si ajabu ukapewa laki na nusu au na sitini. Ukimwambia Cocacola ( HR ) watakuambia mwambie ERO LINK akupe pesa inayostahili maana hiyo anayokulipa sisi hatukukubaliana akulipe hivyo.

Baada ya mjadala bungeni hatimaye waziri wa kazi na ajira wa baraza lililopita ( la raisi mstaafu Jakaya Kikwete ) akaagiza utaratibu huu wa kampuni kuwa ndani ya kampuni nyingine ufe na kampuni zote za mtindo huu ikiwemo ERO LINK ziondoke. Akaagiza wafanyakazi ( vibarua ) wote wawe chini ya kampuni husika.

Kwa hapa kwenye kiwanda cha Cocacola kilichopo Mikocheni Dar es salaam kweli ERO LINK waliondoka ila cha kushangaza baada ya muda mfupi ikaja kampuni nyingine inaitwa CHAGUO SERVICES & CONSULTANTS LTD ambayo ndo ipo hadi muda huu. Hawa nao ni kama ERO LINK tu. Wanatunyonya mno. Kinachotolewa na Cocacola sicho anachotupa chaguo. Ukiumwa utajitibu mwenyewe. Ukienda likizo HUPEWI HATA SENTI. Hakuna motisha wala posho. Arafu ukijifanya kulalamika wanakufukuza kazi mara moja.

Wakija wakaguzi wa Cocacola ( oditors ) ukiwaambia malalamiko yako na ya wengine nakuapia unafukuzwa kazi maana wanasema eti unawachongea. Kwa hiyo vijana hapa tunaburuzwa tu. Tunafanya kazi ngumu mno ambayo kukatwa na chupa ishaanza kuwa kawaida tu. Hata ukipata ajari ya kukanyagwa na folk lift unapewa tu huduma ya kwanza kisha wanakwambia urudi nyumbani kujitibu mwenyewe ukipona ndo utarudi kazini.

Kampuni ya Cocacola yenyewe imeweka bima kwa waajiliwa wao tu. Vibarua au wale walioajiliwa na Chaguo hakuna mwenye bima hata mmoja.

Kwa mujibu wa sheria kama sikosei kibarua anatakiwa afanye kazi kwa kipindi cha miezi sita tu baada ya hapo anatakiwa aajiliwe. Lakini hapa Cocacacola kwanza ltd ( Mikocheni -Dar es salaam ) watu tuna miaka zaidi ya nane bado tu vibarua. Mwambieni Mh waziri kwamba yupo MTU hapa ana miaka 15 kazini na bado hadi leo ni kiabarua.

Kuna boss Fulani wa Cocacola aliwahi kutuambia kwamba kampuni ya Cocacola iliiweka kampuni ya Chaguo au ero link pamoja na Ik kipindi cha nyuma ili tu kuikwepa hiyo sheria ya mtu kuajiriwa baada ya miezi sita. Kwahiyo kibarua ukienda Cocacola (HR) kulalamika watakuambia sisi wewe HATUKUJUI, sisi tunaijua kampuni ya Chaguo na ndiyo tulioiajiri. Daah inauma sana jamani.

Mwambieni muheshimiwa waziri kwamba kampuni kama ERO LINK , Chaguo na nyinginezo nyingi ni MAJIPU. Mwambieni ayakamue kwa kuziondoa kabisa.

Tafadharini sana jamani. Mfikishieni hayo muheshimiwa waziri Jenister Muhagama na naibu wake Abdallah Possy. Lakini hata muheshimiwa waziri mkuu natamani pia angeliona hili.

#Hapa kazi tu# Sawa, lakini unyonyaji na ujanja ujanja wa baadhi ya kampuni unatuumiza mno vijana.

Imefika wajiandae
 
Ni kweli ndugu, hiyo ni moja ya njia ya kusaidia, ingine ni kuhakikisha hao wanatekeleza matakwa ya mikataba yao, huwa wanaandika kiwango ambacho wanamlipa kila mfanyakazi lakini wanafanya kinyume.
Dash! Yaani ni kweli kabisaaa. Ulijuaje wewe lakini.Mi niliwahi kuwa na ero link. Aisee ni balaaa hizi kampuni hazina huruma kabisa na vijana.
 
Hili ni jipu linalotakiwa kutumbuliwa mapema iwezekanavyo sawa na hizi kampuni za simu zinaingiza fedha nyingi lakini kwa uzembe wa wizara husika inawaachia wana subcontract uajiri. Mfano kazi za Customer services hapa tanzania ni ngumu kwani ni rahisi kwa muhusika kufa masikio hasa wale wanaoshinda na ma earphone masaa 8 bado bacterial infections toka sikio la agent mmoja kwenda mwingine,hearing loss etc lakini unakuta spanco sasa wamejibadilisha jina wako jengo la quality plaza na erolink mygoli wanalipa mshahara kiduchu bila hata bima ya afya.
Tupige vita vibarua kwani kodi stahili ya paye haipatikani hapo.
 
Kwakweli serikali iliangalie hili swala. Watu tunanyonywa mno vibarua
 
Back
Top Bottom