Mwalimu Nyerere hakuona kazi kujiuzulu

Mwalimu Nyerere hakuona kazi kujiuzulu

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
10,884
Reaction score
18,824
1. Mwaka 1955 alijiuzulu ualimu Pugu sekondari baada ya kuambiwa achague siasa au ualimu
2. Kama mwaka 1958 hivi alijiuzulu ubunge baada ya kuona hamna anachofanya, mapendekezo yake yote yanatupiliwa mbali.
3. Mwaka 1962 alijiuzulu uwaziri mkuu
4. Akamaliza na kujiuzulu/kung'atuka urais.

Au alikuwa na ugonjwa wa kujiuzulu?
 
Kung'atuka urais ilikua lazima penda asipende.
Si kweli labda hausikilizi hotuba zake ,kuna moja alisema kila akitaka kujiuzulu wasaidizi wake walikuwa wanamwambia endelea mwalimu ila akaja kugundua wale wasaidizi walikuwa wanamwambia vile kutokana na maslahi yao binafsi.

Nyerere hakuwa FISADI na kama angekuwa FISADI angekuwa na utajiri kuzidi hata aliokuwa nao MOBUTU SESSESEKO KUKU WAZABANGA hadi anajiuzulu alikuwa na nyumba za kawaida pale msasani zile kama za wakazi wa bagamoyo...Nyerere amejengewa nyumba mwaka 1999 tena alikuwa haitaki.
 
Nisichokipinga kuhusu Julius ni kwamba hakuwa fisadi mla rushwa. Alijaribu kuishi maisha bila ufisadi bila rushwa akafanikiwa. Bila nyumba Kali, bila maisha ghali akaishi duniani vyema.
Kwenye kun'gatuka kwake kiukweli hakukuja hivihivi anguko la baba yetu Soviet Union lilikuwa sababu namba moja ya anguko la Jk.
Rip father.
 
Si kweli labda hausikilizi hotuba zake ,kuna moja alisema kila akitaka kujiuzulu wasaidizi wake walikuwa wanamwambia endelea mwalimu ila akaja kugundua wale wasaidizi walikuwa wanamwambia vile kutokana na maslahi yao binafsi.

Nyerere hakuwa FISADI na kama angekuwa FISADI angekuwa na utajiri kuzidi hata aliokuwa nao MOBUTU SESSESEKO KUKU WAZABANGA hadi anajiuzulu alikuwa na nyumba za kawaida pale msasani zile kama za wakazi wa bagamoyo...Nyerere amejengewa nyumba mwaka 1999 tena alikuwa haitaki.
Wewe chimba zaidi ujue ukweli
 
Nyerere hakuwa fisadi wa pesa, ila alikuwa fisadi wa madaraka. Kwa katiba hii aliyotuachia inathibiyisha Hilo.

Mzee alikuwa na katamaa Fulani hv, ata kukaa mdarakani miaka 20+ inaonesha tamaa zake. Ni mfano wa viongozi waliokuwa na maneno mengi bila vitendo.

Back
Top Bottom