Mwalimu Nyerere aliipenda nchi siyo CCM

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,223
35,149
Kama ilivyokuwa kwa Mwalimu Nyerere mapenzi yake yalikuwa kwa nchi siyo CCM.

Ukipenda nchi utakuwa mzalendo kwa dhati yako. Huwezi kutumwa kufanya ujambazi, ubakaji, utekaji, utesaji, wizi, udhwalimu nk, nawe ukakubali na hata kuja kujitetea mahakamani kuwa ulikuwa mtumwa tu.

Kwa hakika hii ni bila kujali ni nani anayekutuma!

Ukipenda nchi yako huwezi kushabikia vitendo hivyo, anayevitenda wala anayeviagiza kutelekezwa.

Ama kwa hakika mtu huyo kama kweli anatuma watu kufanya hayo atakuwa ni mwovu sana.

Yupo kwenye rekodi mwalimu akiliweka wazi hilo - "CCM siyo mama yake." Moto wake mzee ruksa anaufahamu hata kama leo kumbukumbu za Chatto hana.



Mengine kwamba kuna wenzetu hata walilazimika kutokomea kusikojulikana wakiwa na maumivu makali:

IMG_20211016_132442_593.jpg


kisa na mkawa, hatimaye Sabaya amegota na kwamba rasmi ni mfungwa mwenye "numero", hayo sasa ndiyo lile kipaji lenyewe kama alivyonena Julius.

Ujinga jikiteni kwenye elimu. Huu mwingine ni sawa na ufupi na urefu tu. Hauna dawa 😁😁!

Tupendeni nchi kama wajibu, si vyama wala watu.

Tukapate kuwakemea wote kama wanakotaka kutupeleka siko.
 
Kwa hiyo tukitumwa na wakubwa tuwe tunakataa? Tatizo njaa Sasa; ndo inatutesa tusipofanya wanavyotaka wanakata pumzi ya pesa.
 
Kwa hiyo tukitumwa na wakubwa tuwe tunakataa? Tatizo njaa Sasa ndo inatutesa tusipofanya wanavyotaka wanakata pumzi ya pesa.


Sent using Jamii Forums mobile app

Una maana hii "squalor" yote kuanzia Sabaya, Kingai hadi Idugunde tatizo ni pesa tu za matumbo yao hadi ubinadamu umewatoka, ila inatenda na kushabikia udhwalimu kama misukule "proper" tu?

Kama jibu ni ndiyo, basi Nyerere aligongelea na nyundo. Hapo ni kama urefu na ufupi tu 😁😁.
 
Kwa nini Nyerere alivyokuwa madarakani hakurusu vyama vingi, upinzani, na demokrasia?

Alikiri yalikuwa ni makosa. Akakomaa vikarudi.

Kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa.

Bado haikutoshi tu?

IMG_20211015_144814_546.jpg
 
Mwalimu Nyerere ndie alieimilikisha nchi kwa chama halafu leo unatwambia aliipenda nchi?
 
Mwalimu Nyerere ndie alieimilikisha nchi kwa chama halafu leo unatwambia aliipenda nchi?

Nchi imetekwa nyara. Nyerere haikumilikisha nchi kwa hao ndezi.

Angekuwapo angesha wafurusha hawa.

Mwulize Mwinyi.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom