Mwalimu bora wa Physics aliyewahi kunifundisha

Mwalimu bora wa Physics aliyewahi kunifundisha

Habarini wakuu wa jf.
Leo nimemkubuka Mwalimu wangu na kwa wengine ambae ni bora kabisa katika kizazi hiki na kijacho.

Huyu si mwingini ni Ngaola au ukipenda muite Moddy Physics/ Commissioner

Daah sitakusahau Baba, wewe ndie mwalimu wangu bora kabisa wa muda wote nilitesekaga sana kwenye Physics ila kwako nilipata unafuu mkubwa.

Marafiki zangu kipindi nipo A'Level na O'level walinibatiza jina la 'ZE YOUNG COMMISSIONER'
maana nilizipatia sana zile mbwembwe zako kama 'Let's stop here at this particula junction and if God wishes we shall meet 2moro"

Na jinsi ulivyokuwa unaguna yaani "mmhhhhhhh! mhhhhhh!"

Daah, sikuacha maarifa uliyonipatia nikae nayo peke yangu, ila nimeweza kuwafundisha vijana wengi wengi sana na nimepata sifa nyingi ila moyoni najua bila wewe nisingekuwa hivi.

Am so happy I'm medical personeel ila I love physics because of you na kwa sababu hukunikaririsha.

UISHI MAISHA MAREFU,COMMISSIONER
Usiwaze dogo.... Nashukuru saana na tutakuwa pamoja daima...
 
Kwa sie tech boys, G. R A Titcomb ndio mwisho wa habari kwa O Level.

A Level UP na Nelkon. Sikuwahi kusikia tuition wala nani, ila pongezi ziende kwa Mr. Msami (P Diddy) A'Level na Luhwago (Kaka) O'Level.
 
Unadhani mgote ni mchezo mamaeee.. Mechanics kisubtopic kimoja notes kana Nelkon yote
Hahaha mgote kasolve maswali mengi ya rojer na nelkon so ukimpiga yeye vizuri ukamuelewa hakuna swali lolote litakupiga chenga. Ila all in all physics ya advance ukikomaa b hukosi
 
Nakuona moody Physics ukijipigia upatu......inshort jamaa ni mweupe(shallow),mzurumat hamalizi topics,Kazi kutongoza vitoto vya kike wanaomuelewa wengi ni PCB ambao Physics huwasumbua.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Moody kawa msaada mkubwa wanafunzi kuhusu physics hasa ukanda wa pwani, Dar na mikoa ya jirani. Jamaa ni anafundisha sio mchezo.
Sikuwahi kusoma tuition yake ila aliwahi kuja kufundisha shuleni kwetu kwa muda so watu tulipata muda wa kusaidiwa topics nyingi, ni mwalimu mzuri kweli kweli, shida yake ni kwenye uandaaji wa vitini tu ndio kaachwa mbali na kina Mgote napo ni kwa vile wao wanachimba sana mpaka vingine out of syllabus.
 
Moody mweupe tu wanaojua Physics Vzr ndo watanielewa
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Moody kawa msaada mkubwa wanafunzi kuhusu physics hasa ukanda wa pwani, Dar na mikoa ya jirani. Jamaa ni anafundisha sio mchezo.
Sikuwahi kusoma tuition yake ila aliwahi kuja kufundisha shuleni kwetu kwa muda so watu tulipata muda wa kusaidiwa topics nyingi, ni mwalimu mzuri kweli kweli, shida yake ni kwenye uandaaji wa vitini tu ndio kaachwa mbali na kina Mgote napo ni kwa vile wao wanachimba sana mpaka vingine out of syllabus.
 
Atleast mtiga yuko Vzr na huyu chipukizi eng challange anajitahid ila sio wapuuzi Ally abdallah,mgote na huyo taktaka mood
 
Ticha wangu book-keeping n commerce...Mr.kunga a.k.a Tall boy...

Mr.mwanza wa mathematics...

Walimu wangu Bora kabisa
 
Wakuu Muddy ana patikana wapi kuna mdogo wangu wangu yuko advance phiysics Ina mzingua sana na yupo PCM dogo yupo Dar
 
Warembo wa PCB physics inawasumbua sana kidogo hawa watoto wa pcm wanajitahidi

Wazee wa PAGUMU hapo ndo tulikuwa tunateleza sema geography ndo nilikuwa inatulawiti sana ila physics na maths tuliinyoosha sana

Karibu jukwaa LA elimu muddy physics naona umeamua ujiandikie Uzi
 
PGM niliosoma nao wote ni waalimu, sijui kwanini.
 
Mudy labda physics ya O level yuko njema Huko advance sidhani kama yupo poa
 
My best physics teacher ni MR MWAKITALIMA alikuwa mwalimu IYUNGA TECHNICAL

akiaanza fundisha unapata kama mkanda wa filamu kichwani unatembea juu ya hio mada .

Maswali yanaibuka kichwani na unajijibu mwenyewe bila kuuliza .

Too bad wakaenda kumpa u headmaster so Iyunga wakazulumiwa kichwa kile

Na mkewe aisee kemia ilala kichwani
 
Back
Top Bottom