MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Katika siku ya wafanyakazi May 1995, rais mstaafu na mwenyekiti mstaafu wa CCM Mwl. Julius K. Nyerere ndiyo alikuwa mgeni rasmi. Alitoa hotuba ndefu kidogo iliyo jaa maono na muongozo.
Lakini mimi kuna sehemu moja tu ya hiyo hotuba ndiyo ilinikuna kupita zote. Mwl. alisema kwamba wakati yeye anaingia madarakani na wenzake walikua hawana model ya kufuata. Kila kitu kili takiwa kujengwa kuanzia juu kwenda chini yani "trial & error".
Akaendelea kusema kwamba anakubali serikali yake ilikuwa na mabaya yake lakini pia ilikuwa na mazuri yake. Akasema serikali ya Mwinyi ilipaswa kuchukua yale mazuri na kuyaacha yale mabaya. Hali kadhalika akasema nao serikali ya Mkapa inatakiwa kuchukua yale mazuri ya kipindi cha Mwinyi na kuyaacha mabaya.
Haya maneno yalinigusa sana kwa sababu ni maneno rahisi lakini magumu kuelewa. Leo hii inashangaza serikali yetu inafanya kinyume na kuchukua mabaya yote ya serikali zilizopita na kuyaacha mazuri. Inasikitisha kwamba baada ya miaka hamsini ya uhuru tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele.
Je ni mazuri yapi ya serikali za Nyerere, Mwinyi na Mkapa yalitakiwa kuendelezwa?
[video=youtube;iokLuPXv33]http://www.youtube.com/watch?v=iokLuPXv33[/video]