Mwakyembe, Sitta 'walisafisha' nini Bandarini?

kwa kuwa inaonekana hatujajua sisi wana jf ni nani wa kulaumiwa hebu tuvute subira na hii hatua inayochukuliwa sasa tuone matokeo tuyahukumu matokea. vinginevyo tutakuwa waganga wa kienyeji kutabiri uongo
 
Mwakyembe alichafua kwa kupandikiza ukabla kuwaajiri ndugu zake watupu huku akishiriki kuiba sana, Mzee sita na yeye aliiba zaidi huku akihujumu Reli na kuwafanya Wamiliki wa maroli mladi wa kuchukua pesa kwa kisingizio kuwa akifufua Reli na treni za mizigo watazuiwa kupakia mizigo.kila mmoja alikuwa mwizi kwa syle yake lakini mwisho wa siku wote hawakuisaidia bandari chochote.

Utakuwa una minyoo wewe
 
Tulikuwa tunampa hongera na sifa nyingi humu Mwakyembe tukisema 'aliisafisha bandari' na ni 'mchapakazi' na wengine wakiomba ateuliwe kuwa Waziri mkuu ili alete Hiyo kasi na uchapakazi lakini tunakumbuka Sitta alipom replace na yeye Sitta akala 'ujiko' wa kuisafisha bandari na kuondoa madudu.

Kumbe in reality hakuna walichokifanya au walichokifanya hakikuwa na manufaa sasa tena sasa tunashingilia Magufuli na Majaliwa 'kuisafisha 'bandari na kuondoa madudu.

Maswali ya kujiuliza Sitta na Mwakyembe 'tuliwasifia' kwa nini hasa? Na kinachofanyika sasa tuna uhakika ndo soluhisho la kudumu? Kama sifa tulizowapa Mwakyembe na Sitta huko nyuma zilikuwa za makosa na hizi sifa tunazo mwaga sasa je? Hivi haiwezekani nchi hii mambo yakaenda bila kiongozi 'kutikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' na 'akamwagiwa' sifa tele?

Nchi zote zenye efficiency viongozi wao huwa 'wanatikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' Kama hapa kwetu?

The Boss, unatumika vibaya sana na hujui unachotumika nacho. Waambie hao wanaokutuma, waangalie haja za kukutuma nazo. Hivi unafikiri bila kazi ya TPA wakiwa chini ya Mwakyembe wasingetunza kumbukumbu taarifa zingepatikana wapi? Sasa kwa kukusaidia tu mchezo ulikuwa kama ifuatavyo, waliwatumia watu wa IT wa TRA kuondoa yale maconteiner kwenye system yao. Kwahiyo audit zote zilipita bila tatizo. Ila ukiangalia kwenye list ya TPA utagundua makontena ni mengi lakin kule TRA hayajalipiwa. Sasa huyo Mwakyembe anaingiliana vipi na TRA? Mtasumbuka sana na Mwakyembe maana amewashika pa baya mmeshindwa hata kupumua kwa ufisadi wenu. Swali la mwisho je mmemsikia mkurugenzi wa TPA kuhusishwa kwenye suala hili?
 
Kweli humu ndani kuna watu wanatakiwa kupimwa akili hivi jambo la Tra na Bandari wapi na wapi mpk Ahusishwe Mwakyembe na Sitta? Wakupuuzwa tu hawa
 
Tulikuwa tunampa hongera na sifa nyingi humu Mwakyembe tukisema 'aliisafisha bandari' na ni 'mchapakazi' na wengine wakiomba ateuliwe kuwa Waziri mkuu ili alete Hiyo kasi na uchapakazi lakini tunakumbuka Sitta alipom replace na yeye Sitta akala 'ujiko' wa kuisafisha bandari na kuondoa madudu.

Kumbe in reality hakuna walichokifanya au walichokifanya hakikuwa na manufaa sasa tena sasa tunashingilia Magufuli na Majaliwa 'kuisafisha 'bandari na kuondoa madudu.

Maswali ya kujiuliza Sitta na Mwakyembe 'tuliwasifia' kwa nini hasa? Na kinachofanyika sasa tuna uhakika ndo soluhisho la kudumu? Kama sifa tulizowapa Mwakyembe na Sitta huko nyuma zilikuwa za makosa na hizi sifa tunazo mwaga sasa je? Hivi haiwezekani nchi hii mambo yakaenda bila kiongozi 'kutikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' na 'akamwagiwa' sifa tele?

Nchi zote zenye efficiency viongozi wao huwa 'wanatikisa' na 'kutingisha' na 'kusafisha' Kama hapa kwetu?

Mtoa post naona umejitoa fahamu, hivi kukwepa kodi kunahusiana vipi na wizara iliyoongozwa na mwakyembe? Hata waziri mkuu jana kwenye majumuisho yake kaisifia bandari kwa kuwa na taarifa sahihi ambazo zimesaidia kujua ni makontena mangapi yameingia na kwenda icd ambako yametoka bila kilipiwa kodi hadi kupelekea kusimamishwa kazi kwa mtendaji mkuu wa Tra na wenzake saba kupisha uchunguzi na wengine watano kushikiliwa na jeshi la polisi kuanzia jana, sasa kuwahusisha mwakyembe na Sita kwenye sekta ambayo sio yao ni nini maana yake au ndio siasa zenu za maji taka? Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
 
TRA wanahusika direct na ulinzi wa kontena?
au zilipotolewa kuna forged documents?
walinzi wa gate no 5 ni waajiriwa wa TRA?

Hizo container zilikuwa zimetoka mikononi mwa tpa na port changes ililipwa ndio maana waziri mkuu kasema walioruhusu container kutoka walikuwa wanajirudia kwa maana ya Tra, usipende kupika maneno Boss siasa za maji taka hazina nafasi kwa sasa, mwakyembe alifanya kazi yake kwa weredi ndio maana mpaka leo tpa hujasikia upotevu wa container
 
Achana naye huyo. Kila kitu cha Magufuli so far amebeza. Sijui alitaka Rais afanyeje! Au ili mradi ni wa CCM haoni jema.

Jimama jiongeze kidogo
ukisoma thread utagundua nazungumzia zaidi utawala wa JK
Mwakyembe na Sitta ndio watendaji waliopata sifa
nahoji sifa zao zaidi....wapi nimebeza Magufuli zaidi ya kuuliza tu what if?
 
Wakala wa Meli/bandari inabidi arudishwe tuondokane na aibu wanayotuchapia hawa matajiri katika kusafirisha mizigo.
 
Hata hii inaweza kuwa kiini macho tu. Maana mfumo wa chama cha mapinduzi ni wakubebana. Ukweli ukibainika basi kila kitu kiwekwe wazi wapelekwe mahakamani nawachukuliwe hatua kweli siyo kuwabeba tena
 
Binafsi nahisi ni movies mbili tofauti na sterling wake ni tofauti kabisa. Ila tatizo linabaki wa watazamaji, ni movie ipi inatuletea ukweli kama ulivyo?

Bado nina mashaka na utendaji wa serikali zetu!

Lazima uwe na shaka
sidhani kama nchi ambayo umewahi kuishi ughaibuni umewahi ona au kusikia waziri anaenda
'kutikisa' na kutingisha' au 'kusafisha' bandarini au airport ili huduma ziende..
kwa vyovyote vile kuna kitu wenzetu wanakifanya ambacho sisi hatukifanyi
na hatutaki kujifunza....

Sinema za 'kutingisha' na 'kusafisha' mbele ya camera za TV...zinatupanda vichwani...
 
thread ina maswali ya msingi, umeharibu ulipoanza kumtetea bade.

Unaweza changia kwa kipande unachokubaliana nacho
Bade harudi tena....unaweza changia ili madudu haya yasijirudie
 
The Boss hoja yako haijaeleweka vizuri. wao wanadhani unabeza utendaji kazi wa Magufuli kumbe unahoji kama hatua zilizochukuliwa ni endelevu kitaasisi au ni sifa za muda mfupi za mtu? Watu badala ya kujadili maudhui yanayojenga hoja yako, wao wanajadili mtiririko wa uandishi wa hoja yenyewe.

Pia umetoa hoja ya msingi sana. Hivi nchi kama Marekani, Japani, nchi za Scandinavia,Ulaya na nyinginezo zilizoendelea za Asia zikiongozwa na Uchina, nchi zao ziliendelea kwa viongozi wao kufanya mbwembwe hizi zinazofanywa na viongozi wetu?

Mkuu ahsante kwa kunielewa....
maswali hayo very valid...na wapo wana JF wanaishi nchi hizo wanaopita hapa
lakini hizi mbwembwe zina 'mvuto' zaidi kwao
 
Mwakyembe alichafua kwa kupandikiza ukabla kuwaajiri ndugu zake watupu huku akishiriki kuiba sana, Mzee sita na yeye aliiba zaidi huku akihujumu Reli na kuwafanya Wamiliki wa maroli mladi wa kuchukua pesa kwa kisingizio kuwa akifufua Reli na treni za mizigo watazuiwa kupakia mizigo.kila mmoja alikuwa mwizi kwa syle yake lakini mwisho wa siku wote hawakuisaidia bandari chochote.

Usilopoke kama umelewa viroba unaweza kutuambia hao ndugu zake mwakyembe aliowaajiri huko bandarini ni akina nani au unaandika ili nawe uonekane umeandika tu
 
The Boss, unatumika vibaya sana na hujui unachotumika nacho. Waambie hao wanaokutuma, waangalie haja za kukutuma nazo. Hivi unafikiri bila kazi ya TPA wakiwa chini ya Mwakyembe wasingetunza kumbukumbu taarifa zingepatikana wapi? Sasa kwa kukusaidia tu mchezo ulikuwa kama ifuatavyo, waliwatumia watu wa IT wa TRA kuondoa yale maconteiner kwenye system yao. Kwahiyo audit zote zilipita bila tatizo. Ila ukiangalia kwenye list ya TPA utagundua makontena ni mengi lakin kule TRA hayajalipiwa. Sasa huyo Mwakyembe anaingiliana vipi na TRA? Mtasumbuka sana na Mwakyembe maana amewashika pa baya mmeshindwa hata kupumua kwa ufisadi wenu. Swali la mwisho je mmemsikia mkurugenzi wa TPA kuhusishwa kwenye suala hili?

Soma michango ya wengine kabla hujachangia
watu tele wametaja jinsi Bandari walivyohusika
hao walinzi wa gate no 5 sio watumishi wa TRA...
 
Back
Top Bottom