Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau, wakati Waziri Mwakyembe akijibu hoja za Wabunge walizoibua wakati wa mjadala wa hotuba ya bajeti ya Waziri wa Uchukuzi, hususan wale walioelezea hisia zao kutokana na ATCL kuwa na ndege moja tu, Waziri Mwakyembe amesema kuwa kikwazo kikubwa kwa ATCL kuwa na ndege ni deni linalodaiwa shirika hilo. Amesema kuwa ikiwa wabunge watapigania ili deni hilo lilipwe, yeye yupo tayari kuleta ndege mpya zaidi ya Tano nchini. Amesema kuwa kama wabunge wanamuona ni muongo, wajaribu kushinikiza ulipwaji wa deni hilo ndipo waje kumhukumu.
Hakika kwa hili, kuna kila sababu ya deni hil kulipwa ili shirika letu la ATCL liweze kusimama tena. Sina hakika ya kiasi cha deni hilo ila kama kuna mwenye figure kamili atuwekee ili tuone ukubwa wa deni hilo.