Mwakyembe: Nitaleta Ndege zaidi ya Tano Nchini ikiwa deni la ATCL litalipwa

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,869
2,000
Wadau, wakati Waziri Mwakyembe akijibu hoja za Wabunge walizoibua wakati wa mjadala wa hotuba ya bajeti ya Waziri wa Uchukuzi, hususan wale walioelezea hisia zao kutokana na ATCL kuwa na ndege moja tu, Waziri Mwakyembe amesema kuwa kikwazo kikubwa kwa ATCL kuwa na ndege ni deni linalodaiwa shirika hilo. Amesema kuwa ikiwa wabunge watapigania ili deni hilo lilipwe, yeye yupo tayari kuleta ndege mpya zaidi ya Tano nchini. Amesema kuwa kama wabunge wanamuona ni muongo, wajaribu kushinikiza ulipwaji wa deni hilo ndipo waje kumhukumu.

Hakika kwa hili, kuna kila sababu ya deni hil kulipwa ili shirika letu la ATCL liweze kusimama tena. Sina hakika ya kiasi cha deni hilo ila kama kuna mwenye figure kamili atuwekee ili tuone ukubwa wa deni hilo.
 

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,542
2,000
Kyela kuna Wazee waliahidiwa Nyumba, magari, nk...... kawaulizeni wamepokea nini hadi leo hii.

Pia huwa anaruka hata kile alikisema mapema kwa nyuzi 180*

 
Last edited by a moderator:

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,700
2,000
MWakyembe ni Pimbi, yeye a nashindwa kuweka hoja kwenye baraza la Mawaziri anakuja kuomba msaada Bungeni , nani alimsababishia hayo madeni?
 

kizaizai

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
3,709
2,000
Wanaoweza hawatoiahadi, wanatekeleza bila masharti. Wakajifunze Kenya na Ethiopia.
 

The Name

JF-Expert Member
Jan 30, 2014
812
225
Kwa serkali hii ya ma ccm sidhani kama kuna ndege hapo,kwanza waziri mwenyewe nae ni msaliti tu,alitaka serkali 3 mara akageuka tena yani ndani ya ccm hakuna mkweli hata mmoja
 

Cloud Computing

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
334
195
Kwa hiyo anataka kutuambia kama deni halilipwi basi huu kamwe hatutamiliki ndede zetu, huu ni umaskini mkubwa sana wa fikra kwa viongozi wengi wa nchi hii
 

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,376
2,000
Hakika kwa hili, kuna kila sababu ya deni hil kulipwa ili shirika letu la ATCL liweze kusimama tena. Sina hakika ya kiasi cha deni hilo ila kama kuna mwenye figure kamili atuwekee ili tuone ukubwa wa deni hilo.


Mimi nadhani tuanze na walio tutia kwenye hilo deni na hiyo hasara kwanza ndio tuje kulipa.
Sawa sawaaaa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom