Mwakyembe na ufisadi mabehewa feki

Kosa la kwanza la Magufuli alilolifanya ktk uteuzi wake ni kuwaingiza hawa mabwana wawili ktk cabinet yake; Dr. Harrison Mwakyembe na Prof. Sospeter Muhongo.

Hakika kivuli cha tuhuma za hawa mabwana kitamwandama na hatutashangaa na haitakuwa ajabu kuona akipangua baraza lake la mawaziri si muda mrefu, else ajiandae yeye mwenyewe kuwa JIPU KUU!

Lol, ama kweli CCM ni ile ile, kamwe ni ngumu sana ikabadilika!!
 
mkuu mbona hayo maelezo unayoyatoa mwakyembe mwenyewe kashindwa kuyatoa ili kujitetea bungeni
 
Ni kuongeza elimu ya uraia kwa wananchi waweze kujua na kuzitambua haki zao,ili unapofanyika uchaguzi wasidanganywe kwa kupewa khanga,tshirts,na kofia bali wawachague wabunge watakao kuwa tayari kutetea maslahi ya wao na taifa kwa ujumla

Hii haitwezekana mpaka pale jamii itakapo pewa uwezo wa kujitegemea Kiuchumi.Kama mwanachi wa kawaida hatapewa uwezo wa kujikimu kimaisha RUSHWA nyakati za uchaguzi hazitaisha.

Labda kuwe na Tume huru ya uchaguzi ambayo itakuwa na sheria kali,pale mgombea atakaposhikwa kutoa rushwa basi iwe mwisho wake wa kugombea.

Ona hata issue ya UMEYA,Diwani amechaguliwa bado anapokea RUSHWA huoni kwamba ni shida hapo???Rushwa hata kwa wale maofisa wanosimamia uchaguzi wengi wao watakuwa walipokea rushwa toka kwa wagombea walioshindwa ili wawashindishe,na sehemu nyingine ilifahamika mapema zaidi,nyingine haikufahamika mapema
 
Kweli mkuu na hili ni donda ndugu ambalo kupona kwake itachukua miaka
 
Ccm hata aje malaika haiwezi kubadilika na jp ajiandae kuingia kwenye orodha ile ile ya kutoheshimika baada ya kustaafu
 

Jibu hoja acha blah blah zako ... wewe kama baba kiongozi wa familia watt wako wakipoto kimaadili nani aulizwe ???
 
3 problems I have noticed about Tz politics, 1.talking 2.talking 3.talking and then nothing happens, aliyeshiba ataendelea kushiba na mwenye njaa atabaki na njaa yake
Tatizo kubwa Mwakyembe ni rafiki mkubwa wa magu itakuwa vigumu kumwajibisha na hiki ndicho kitakuwa kipimo ingawa sasa Membe akina Nape na January wapo busy kubuni mbinu ya kumlinda asitumbuliwe jipu kwa nguvu na Ukawa.
 
Kkikwete anamjua vizuri Mwakyembe anajua kuwa ndiye alinunua mabehewa mabovu hata kule bandarini alipandikiza ukabila mwingi dili nyingi za wizi wa kontena na ukwepaji kodi zilipigwa wakati Mwakyembe akiwa Waziri wa uchukuzi.
 
Hiyo ni minotice tu ya maadili ya viongozi ambayo katibu Mkuu alikuwa anawasomea wateule wa JPM. Ambapo hao wateule walikuwa wanasikia sikio la kushoto wanatolea sikio la kulia, hakuna hata mmoja ambaye angekataa ulaji. #ccmNiIleile
 
Wewe Umekariri Lowasa mpaka unakaribia kusema hata akipita panya nyumbani kwa Mwakyembe atakuwa katumwa na Lowasa, acha kuishi kwa kukariri, hiyo reports yako ilichakachuliwa na Mwakyembe mwenyewe kila kitu kinajulikana kuwa Mwakyembe aliingilia mchakato wote wa Ununuzi mabehewa na alipewa rushwa wenzako wajanja wanajua mchezo wote hata wale ambao kawabebesha zigo wanasema Ukweli kuwa walifanya manunuzi kwa shinikizo la Mwakyembe usipende kumhusisha Lowasa na madili Binafsi ya Mwakyembe utajikuta unakariri hata mende waliopo chooni kwa Mwakyembe wamepelekwa na Lowasa.
 
Nina uhakika 100% umebanwa na ma.vi,nakushauri nenda ukanye kwanza ndio uje uchangie mada.
 
Hoja ya mabehewa fake Mwakyembe ameitolea ufafanuzi jana bungeni.
Ufafanuzi upi? Ule haukuwa ufafanuzi bali ulikuwa ujanja ujanja tu hakuna ufafanuzi kwenye dili hilo inajulikana kuwa Mwakyembe alipiga dili hata akikwepa vipi Safari hii atanasa tu.
 
Mwakyembe awajibishwe tu hapa hakuna habari za kulindana, tunawaomba wabunge wetu wakweli hasa hasa wa upinzani waifanye hiyo kazi maana wabunge wa ccm wao kazi yao ni kulinda maslahi na ustawi wa ccm


Sijui kama atafanyiwa chochote!
 
K
Nina uhakika 100% umebanwa na ma.vi,nakushauri nenda ukanye kwanza ndio uje uchangie mada.
weli hicho kijamaa kitakuwa kinaumwa Tumbo maana kimekariri kuwa Lowasa yupo nyuma ya Mwakyembe kila alipo, hilo ni Tatizo kubwa kuishi kwa kukariri kuwa Mwakyembe ni Mungu hana dhambi na kila kinachomkuta kinafanywa na Lowasa.
 
K

weli hicho kijamaa kitakuwa kinaumwa Tumbo maana kimekariri kuwa Lowasa yupo nyuma ya Mwakyembe kila alipo, hilo ni Tatizo kubwa kuishi kwa kukariri kuwa Mwakyembe ni Mungu hana dhambi na kila kinachomkuta kinafanywa na Lowasa.
Ni muendelezo wa uzuzu tu unaofanywa na wana ccm kudhani kwamba viongozi wao ni malaika wakati matendo yao yaenda kabisa kinyume
 
Team Membe acheni kukariri kuwa kila dhambi za Mwakyembe huibuliwa na Lowasa kumbuka Kikwete alimtoa wizara ya uchukuzi baada ya kubaini kuwa Mwakyembe ni mwizi na fisadi mkubwa.
 
Sijui kama atafanyiwa chochote!
Ni vigumu kuwajibishwa ila kinachotakiwa ni kwa wabunge wa upinzani kuhakikisha wanatimiza wajibu wao na kama serikali itaendelea kiziba masikio wananchi tunaona na tunajua jinsi ya kuwaadhibu
 
Ni muendelezo wa uzuzu tu unaofanywa na wana ccm kudhani kwamba viongozi wao ni malaika wakati matendo yao yaenda kabisa kinyume
ccm ni ile ile na wateuliwa wao ni wale wale huenda hili likafunikwa kijanja na kuishia kuwakandamiza wale wa chini ambao hawakufaidi chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…