Vijana hao ni vigumu kufanya dili nzito namna hiyo bila wakubwa kujua. Hio ni dili ya wakubwa funaliAisee inatisha! Ila hawa vijana wadogo saba bana lol maskini tamaa hizii!
Nilishawahi kusema humu kuwa bandari yetu ipo porous, TRA ni kama hawapo na ni kwamba hawapo maksudi hasa kwenye deals zinazohusu wizi wa rasilimali zetu. Niliwahi kuhoji, meno ya Kinana yaliwezaje kupita kuelekea Ng'ambo bila TRA kuhusika??? Kumbe ile haitoshi, hata kwenye kuingiza vitu kumbe tunaobanwa ni wachache tu, wenyewe wanaingiza bila kodi.Hapa kuna tatizo kubwa sana. Hivi hadi waziri awe anakamata vitu kama hivi wahusika kama polisi na wanausalama wengine wanakuwa wako wapi? Kwa hiyo kama waziri asingeenda kuwakamata ndiyo ingekuwa basi tena malori yanapita kinyemela? Huenda kuna kitu zaidi hapo. Ina maana hawakujua hadi waziri ndio aje kukamata au ndiye yale yale nani atamvika paka kengele?
Hongera kamanda Mwakyembe. Ndaga fijo na hayo malori
Hapa Bongo watu wanaendesha hadi magari ya millioni 200 ukijiuliza kwa uchumi gani hujijibu! Hayo ndiyo majawabu; malori 26 yapite kinyemela unadhani hao wahusika wangevuna kiasi gani?
TRA kujitapa kwa kuvuka lengo ni upumbavu kwan wanajiwekea malengo ya chini sana ambayo ni mepesi kuvukwa. Wanawezaje kujigamba wakati wafanya biashara kibao mtaani hawalipi kodi???Jaman ili goal iwe goal ni lazma iwe realistic, huwez ukazema unajiwekea goal kulala kwako ucku then ukifika usiku ukilala kwako unafurahia eti umevuka lengo, huu ni upuuzi.Nchi hii iko hatarini kwani kila taasisi sasa ni wizi tu.TRA wanaojigamba kukusanya kodi na kuvuka Malengo hawasitahili sifa wanazopata kwani ndiyo vinara wa rushwa huku wakijivunia vikodi vidogo vinavyokusanywa kutoka kwa masikini wa nchi hii na kuacha Matajiri wengi hasa wa kutoka Asia wakiendesha biashara na kujitajirisha bila kulipa kodi.Matokeo yake ni kudidimiza ustawi wa Wazawa na kuwaneemesha wageni.
mwakyembe amekuwa polisi siku hizi? Au hajui majukumu yake!
Angalau sasa watanzania tunaweza kufuta ile kauli ya kubezwa na kudharauliwa iliyopata kutolewa na Rais Kagame wa Rwanda kuwa ati tumpe bandari yetu atufundishe namna ya kutenda kazi(kukusanya mapato kikamilifu,kufuta urasimu,kuboresha huduma na kuondoa msongamano).goo goo gooo gooo Malafyale,goo Mwakyembe gooo!!!