Mwakyembe na polisi wadaka watano wakitaka kuvusha malori 26 kinyemela bandarini

Naona ni mwendo wa DAGAA tuu ila MAPAPA yale makubwamakubwa hayaguswi,,,Njama tu hizo yaan hapo lazima kuna kigogo anahusika ila hao ndo CHAMBO au KAFARA,,,,,ukitaka utajiri wa kush2kiza uwe mfanyakazi wa TPA au TANAPA yaan ni miez6 unakula kuku kwa Mrija!,,,mazafanta wezi wote

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Hayo magari yangefanikiwa kutoka tu documents zake zingechanwa,usingezipata TRA wala TPA Kisha wangedai yameibiwa bandarini.Hiyo ni michezo ya kila siku bandarini,uliza mwaka jana MAKATAPILA mangapi yameibiwa,yanapitia wapi wakati mageti ya kutokea ni matatu tu, MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MINGU MBARIKI mwakyembe
 
Chadema bhana sasa mlitaka slaa ndio alipue bomu la ufisadi bandariini? Kwani na yeye amekuwa polisi au mpelelezi? Akili zenu ni fupi kama mkia wa mbuzi! Tatizo ni mfumo kristo wamejazana bandarini kazi kuiba na kudidimiza uchhumi wa nchi angalia waliokamatwa leo wote ni kina CDU
 

LOL... HATARI na Lazima WAKUBWA watatajwa... Malori zaidi ya 20? na hakuna KIGOGO aliyehusika? kama ni HIVYO nchi yetu IMEANGAMIA VIOFISA VIDOGO haviwezi kuashiria TRICK kubwa kama HIYO
Dhando ni Muziki mnene huo... unatisha
 
Mbona magari yenyewe ni ya zamani? Registrations ni za hapa UK mfano R reg ni 1995!!!! Wataweza kulipia huo ushuru???? Yameishachoka sana na sijui yaliruhusiwa vipi kutoka UK maana sio rahisi kuruhusu magari kama haya kupita
nawe acha kuongea bila kutafiti. unaweza kuonyesha sheria inayozuia trucks za 1995 kuingia Tanzania? au hata kutembea ndani ya UK?
 
Hapa kuna tatizo kubwa sana. Hivi hadi waziri awe anakamata vitu kama hivi wahusika kama polisi na wanausalama wengine wanakuwa wako wapi? Kwa hiyo kama waziri asingeenda kuwakamata ndiyo ingekuwa basi tena malori yanapita kinyemela? Huenda kuna kitu zaidi hapo. Ina maana hawakujua hadi waziri ndio aje kukamata au ndiye yale yale nani atamvika paka kengele?

Hongera kamanda Mwakyembe. Ndaga fijo na hayo malori

Hapa Bongo watu wanaendesha hadi magari ya millioni 200 ukijiuliza kwa uchumi gani hujijibu! Hayo ndiyo majawabu; malori 26 yapite kinyemela unadhani hao wahusika wangevuna kiasi gani?


Mkuu mpaka ukiona waziri kaja hapo, kazi ilishafanywa na wahusika kwa muda mrefu tu hadi kuzaa matunda hayo. Mara zote wahalifu wanafikiri ahead kufanikisha jambo lao na ujue ni wahalifu ndio wanapanga namna na wakati gani wa kufanya uhalifu tena bila kuwataarifu law enforcers kama police ndio maana wanakutwa by suprise mara nyingi. Lakini kwa hili watu wamefanya kazi ya hatari tena wakihusiswa hat baadhi ya wafanyakazi wa hiyo kampuni jizi.
 
Mwakyembe si Polisi, si sehemu ya auditor wa CAG wala si mwajiriwa wa TAKUKURU, kawakamata. ila watu na taaluma zao walizosomea eti wanasema ni vigumu sana kukamata mambo kama haya. Wangekuwa TARUKURUKU wangedai chao na mchezo ungeishia palepale. TZ zaidi ya tuijuavyo
 
mwakyembe amekuwa polisi siku hizi? au hajui majukumu yake!
Mkuu Mchaka Mchaka Mbona unazungumza maneno ya Pumba wewe?Ulitaka Mheshimiwa Waziri H. Mwakyembe akae ofisini kwake anapunga upepo wa feni kwa ajili ya joto kali sana la Dar? Alichofanya

Mheshimiwa Waziri

H.Mwakyembe kingelifaa kuiga na Mawaziri wenzake wote sio kupunga upepo Ofisini huku mafisadi wanaharibu uchumi wa

nchi. Nchi ina Polisi lakini hawafanyi kazi zao nchi ina wapelelzi lakini hawafanyi kazi zao ni kula Rushwa nchi inanuka kwa

wizi na kula rushwa Hongera Mheshimiwa Waziri H.Mwakyembe Mwenyeezi Mungu akulinde na hao Mafisadi wa nchi yetu

Ameen. Wallah ninaapa kwa Mwenyeezi Mungu Rais wetu Mzee J.Kikwete angelipata Ma-Waziri 10 katika Serikali yake

wana uchungu na Mali ya Umma kama alivyo Mheshimiwa Waziri H.Mwakyembe basi nchi yetu ingelikuwa na Maendeleo

lakini wapi? Ma-Waziri wake wote Mheshimiwa Rais wetu J.Kikwete Mawaziri wote wake ni feki na wengi wao ni

Mafisadi Ee Mola iokowe nchi yetu na Viongozi Mafisadi ameen.
 
Last edited by a moderator:
tulipofika ni pabaya sana jamani,kupata kazi sehemu kama hizi kwa mtu wa kawaida tu lazima utoe rushwa tena ya maana.otherwise uwe mtoto wa fulani kwa sababu ya wizi kama huo,nchi inanuka kila kona hakuna unafuu idara zote duh sijui kama tutafika kweli.
 
"....................nipe bandari nitakulisha wewe na watu wako wote kwa hiyo bandari"
 
Sokomoko mwizi ni mwizi tu hana dini hata majina mengine huenda sio halisi. Tunaomba Dr uwabambe na mabosi wa hao vijana kwani wao ndio walisuka dili zima hawa wadogo ni watekelezaji tu.
 
Hongera Dr. Tunakuomba uwabambe na mabosi wa hao vijana kwani wao ndio waliosuka dili hawa vijana ni watekelezaji tu. kwani hata EPA ilikuwa hivyohivyo wale wa BOT walikuwa wanatekeleza ya wakubwa ingawa walijua iko nje ya maadili yao ya kazi.
 
Wazee wa bandari siku hizi siwasikii kabisa yaani kama vile hawapo,zamani nilizoea kusikia papaa fulani mzee wa bandari siku kimyaa!!!!!
 
Back
Top Bottom