Mwakyembe na polisi wadaka watano wakitaka kuvusha malori 26 kinyemela bandarini

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225
113.jpg

Waziri wa Uchukuzi Dk. Harisson Mwakyembe akizungumza na waadishi wa habari
Bandarini jijini Dar es salaam leo jioni wakati akitoa taarifa ya
kukamatwa kwa watumishi wa Bandari wanaodaiwa kutaka kutoa malori 26
kinyemela bandarini, watu watano wamekamatwa katika sakata hilo.

25.jpg

Dk.
Harrison Mwakyembe akiongea na maafisa mbalimbali wa Polisi na Bandari
baada ya kukagua magari hayo yaliyotaka kutolewa kinyemela bandarini
hapo.

62.jpg

Dk.
Mwakyembe akikagua Malori yanayodaiwa kutaka kutolewa kinyemela na
kampuni ya Dhandho, Malori matano kati ya 26 yalipewa baraka na Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) yatolewe.

34.jpg

Mmoja wa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Andrew Masaga (kulia)
anayedaiwa kuhusika kula njama ya kutoa malori hayo akijitetea mbele ya
Waziri (hayupo pichani) katika sakata hilo leo jinoni. Kushoto ni Mkuu
wa Polisi Bandarini Afande FM Misilimu
44.jpg

Ofisa Utawala wa kampuni ya Dhandho Antipasi Otieno (kulia) akitoa maelezo mbele ya waziri Dk. Harrison Mwakyembe

52.jpg

Mtumishi
wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Gladness Mangelele akitoa maelezo
mbele ya Waziri Dk. Mwakyembe baada ya kuhusishwa katika sakata hilo
ambapo alidai alikuwa hajui chochote kwani alikuwa akitekeleza majukumu
yake ya kawaida katika idara yake.

71.jpg

Marystella Minja akitoa maelezo yake mbele ya Waziri Dk Harrison Mwakyembe baada ya kutuhumiwa katika sakata hilo.

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,866
2,000
Hapa kuna tatizo kubwa sana. Hivi hadi waziri awe anakamata vitu kama hivi wahusika kama polisi na wanausalama wengine wanakuwa wako wapi? Kwa hiyo kama waziri asingeenda kuwakamata ndiyo ingekuwa basi tena malori yanapita kinyemela? Huenda kuna kitu zaidi hapo. Ina maana hawakujua hadi waziri ndio aje kukamata au ndiye yale yale nani atamvika paka kengele?

Hongera kamanda Mwakyembe. Ndaga fijo na hayo malori

Hapa Bongo watu wanaendesha hadi magari ya millioni 200 ukijiuliza kwa uchumi gani hujijibu! Hayo ndiyo majawabu; malori 26 yapite kinyemela unadhani hao wahusika wangevuna kiasi gani?
 
arinaswi

Senior Member
Sep 25, 2010
183
170
Jamani huyo mdada ni mdogo wangu jamani!!! Kumbe ndio kazi zenyewe anazofanya hizi!!! Alipoacha kazi Barclays hatukujua kama alikuwa anataka mambo ya kupata utajiri kwa urahisi tena kwa haraka haraka!! Pole sana Tanzania!! Tunafisidiwa kila upande, hata wavuja jasho wenzetu wanapopata mwanya wanatutenda!
 
Tatu

JF-Expert Member
Oct 6, 2006
1,079
1,225
Wizi wote huu ukiweza kudhibitiwa, Tanzania inaweza kukusanya mapato mengi sana ya kutosheleza mishahara mizuri kwa wafanyakazi wake na maendeleo kwenye huduma za jamii. Manyang'au wachache na viongozi dhaifu na wabinafsi ndio wanakwamisha hii nchi.

Hongera Mr. Mwakyembe.
 
Mkatavimeo

JF-Expert Member
Jan 3, 2011
2,152
2,000
Marystella Minja ana uhusiano na akina Andrew Minja na David Minja? Naona kafanana nao kiaina.
 
kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,171
2,000
kila taasisi za serikali ni matatizo, mpaka TRA wanajihusisha kuihujumu nchi yetu, mbali na kulipwa mishahara mikubwa. Polisi nayo imeoza, ndiyo maana inaitwa ni kichaka na genge la wahalifu. Nani ametuloga watanzania jamani?
 
BROO

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
360
195
Aisee inatisha! Ila hawa vijana wadogo saba bana lol maskini tamaa hizii!
 
figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
18,668
2,000
dhandho na manilax huwa yanabeba mizigo ya serikalini na mizigo ya jeshi mara nyingi. wahindi nawachukia kwa kukwepa kodi tu. inabidi wajirekebishe bana. mia
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225
kila taasisi za serikali ni matatizo, mpaka TRA wanajihusisha kuihujumu nchi yetu, mbali na kulipwa mishahara mikubwa. Polisi nayo imeoza, ndiyo maana inaitwa ni kichaka na genge la wahalifu. Nani ametuloga watanzania jamani?

UONGOZI wa CCM UMETULOGA... WALIANZA SISI wananchi tukafuata... UFISADI

Mara Walikuja na RUKSA... Wakaua NGUZO 5 za UONGOZI; Wakaja na Kusaini DEALS za MADINI Uchwara na Kuuza VIWANDA na MAJUMBA yote ya SERIKALI kwa HAO wao WACHACHE... Sasa Ukiiangalia CCM kila MTU ana DEALs hadi watoto wa VIONGOZI wa CCM... Kweli Mwananchi hataweza kufuata UCHWARA HUO?
 
Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,998
2,000
Hapa kuna tatizo kubwa sana. Hivi hadi waziri awe anakamata vitu kama hivi wahusika kama polisi na wanausalama wengine wanakuwa wako wapi? Kwa hiyo kama waziri asingeenda kuwakamata ndiyo ingekuwa basi tena malori yanapita kinyemela? Huenda kuna kitu zaidi hapo. Ina maana hawakujua hadi waziri ndio aje kukamata au ndiye yale yale nani atamvika paka kengele?

Hongera kamanda Mwakyembe. Ndaga fijo na hayo malori

Hapa Bongo watu wanaendesha hadi magari ya millioni 200 ukijiuliza kwa uchumi gani hujijibu! Hayo ndiyo majawabu; malori 26 yapite kinyemela unadhani hao wahusika wangevuna kiasi gani?
Hii inaonyesha kuwa mfumo mzima umeoza kwa wizi na rushwa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom