Mwakyembe na polisi wadaka watano wakitaka kuvusha malori 26 kinyemela bandarini

Hao maafisa wafuatilieni na wanavyomiliki wanatakiwa wafilisiwe na wa start from zero again.... mimi sikubari hao madada hawawezi kuwa wezi wanatumiwa tu vigogo ndio wezi kwani wanaacha haya yanaendelea tu na hao wenye uwezo wa kutoa punguzo wamepata wapi ridhaa ya kusamehe kodi? ndio kina mramba wengine hawa
 
kwani wizi ni ajabu kutokea bandarini? kwa taarifa ni kwamba HAKUNA transaction inayokamilika bila kuchakachuliwa pale long room na wafanyakazi wa TRA kodi ya serikali huishia mifukoni mwao
 
Aisee inatisha! Ila hawa vijana wadogo saba bana lol maskini tamaa hizii!
Vijana hao ni vigumu kufanya dili nzito namna hiyo bila wakubwa kujua. Hio ni dili ya wakubwa funali
 
Nchi hii iko hatarini kwani kila taasisi sasa ni wizi tu.TRA wanaojigamba kukusanya kodi na kuvuka Malengo hawasitahili sifa wanazopata kwani ndiyo vinara wa rushwa huku wakijivunia vikodi vidogo vinavyokusanywa kutoka kwa masikini wa nchi hii na kuacha Matajiri wengi hasa wa kutoka Asia wakiendesha biashara na kujitajirisha bila kulipa kodi.Matokeo yake ni kudidimiza ustawi wa Wazawa na kuwaneemesha wageni.
 
Jamani serikalini watu wanaiba jamani nimepata mshituko yani wenzetu wanapata billion300 sisi bilion27 kwa mwezi, jamani hii ni bandari tu tunapoteza mabillion je secta nyingine??? JAMANI TUMUOMBEE MWAKIEMBE HUYU NI WAZIRI WA MFANO WA KUIGWA SANA ANASTAILI PONGEZI NA ULINZI SANA
 
Hapa kuna tatizo kubwa sana. Hivi hadi waziri awe anakamata vitu kama hivi wahusika kama polisi na wanausalama wengine wanakuwa wako wapi? Kwa hiyo kama waziri asingeenda kuwakamata ndiyo ingekuwa basi tena malori yanapita kinyemela? Huenda kuna kitu zaidi hapo. Ina maana hawakujua hadi waziri ndio aje kukamata au ndiye yale yale nani atamvika paka kengele?

Hongera kamanda Mwakyembe. Ndaga fijo na hayo malori

Hapa Bongo watu wanaendesha hadi magari ya millioni 200 ukijiuliza kwa uchumi gani hujijibu! Hayo ndiyo majawabu; malori 26 yapite kinyemela unadhani hao wahusika wangevuna kiasi gani?
Nilishawahi kusema humu kuwa bandari yetu ipo porous, TRA ni kama hawapo na ni kwamba hawapo maksudi hasa kwenye deals zinazohusu wizi wa rasilimali zetu. Niliwahi kuhoji, meno ya Kinana yaliwezaje kupita kuelekea Ng'ambo bila TRA kuhusika??? Kumbe ile haitoshi, hata kwenye kuingiza vitu kumbe tunaobanwa ni wachache tu, wenyewe wanaingiza bila kodi.

Sasa tunawezaje kusubiri maendeleo wakati kodi haikusanywi??? Mimi ningetegemea bandarin kuwe na ulinzi mkali sana unaohusisha pia vifaa vya kisasa, lakin inaonekana pale hamna hata ulinzi. Naomba Pale Polisi waondolewe na ulinzi huo ufanywe na kampuni binafsi na kuwepo vifaa vya kunasa sauti na taswira pia ili iwe rahisi kunyoosheana vidole.
 
Nchi hii iko hatarini kwani kila taasisi sasa ni wizi tu.TRA wanaojigamba kukusanya kodi na kuvuka Malengo hawasitahili sifa wanazopata kwani ndiyo vinara wa rushwa huku wakijivunia vikodi vidogo vinavyokusanywa kutoka kwa masikini wa nchi hii na kuacha Matajiri wengi hasa wa kutoka Asia wakiendesha biashara na kujitajirisha bila kulipa kodi.Matokeo yake ni kudidimiza ustawi wa Wazawa na kuwaneemesha wageni.
TRA kujitapa kwa kuvuka lengo ni upumbavu kwan wanajiwekea malengo ya chini sana ambayo ni mepesi kuvukwa. Wanawezaje kujigamba wakati wafanya biashara kibao mtaani hawalipi kodi???Jaman ili goal iwe goal ni lazma iwe realistic, huwez ukazema unajiwekea goal kulala kwako ucku then ukifika usiku ukilala kwako unafurahia eti umevuka lengo, huu ni upuuzi.

Kila kona sasa hiv kuna wizi, kinana kavusha meno bila kulipa kodi ya yale meno, Haw nao walikuwa wamekwepa kodi, huko mipakan ndo usiseme, wafanya biashara wakubwa nao hawalipi kodi stahili achilia mbali wafanyabiashara ndg ndg, wafugaji na wakulima wanafanya biashara kubwa sana hatujawaona wakitozwa kodi za maana hivi ktk mazingira haya ambayo hata kuinstitute matumizi ya risiti tu wameshindwa, wanawezaje kujigamba kuwa wamevuka lengo??? Labda wanavukaga malengo ya kutuibia kiasi flan cha pesa kwa mwaka. Katu hawajawahi kuvuka lengo kwenye kukusanya kodi, TRA ina underperform! Nyerere alipata kusema Serikali Corrupt haiwezi kukusanya kodi!! Kweli nayaona aisee.
 
heko dr. mwakyembe. piga mzigo tuko nyuma yako. saidianeni huko ukwepaj wa kodi ufikie mwisho. weken mikakat hlo tatzo liwe historia. kuna watu hawajui mambo kama haya ya ukwepaj kodi na ufisad ndo yanafanya nchi ionekane ya ovyo na mwisho yanaangusha nchi
 
du! mi napita tuu, inatia moyo nikiangalia hatua za mh mwakyembe maana ni kitu tofauti sana na yale ya jana. wachina wana msemo eti safari ya kilometa 1000 huanza kwa kuchukua hatua moja. Mimi ninachohofia ni jinsi hii muvi "starring" mwakyembe itakavyoisha, sijui kama mabaharia wataamua kumuua kiaina kama yule jaji sikumbuki jina lake aliuwawa miaka ya nyuma sana ajali ya gari ya kutatanisha au wamtoe kafara ili kutoa onyo kwa wanaomfuata huyu shujaa mwakyembe. haya ni maji marefu, wanaofahamu hawasemi wanaosema wanauwawa, hapa sijui ni nani atanusurikia.
 
Angalau sasa watanzania tunaweza kufuta ile kauli ya kubezwa na kudharauliwa iliyopata kutolewa na Rais Kagame wa Rwanda kuwa ati tumpe bandari yetu atufundishe namna ya kutenda kazi(kukusanya mapato kikamilifu,kufuta urasimu,kuboresha huduma na kuondoa msongamano).goo goo gooo gooo Malafyale,goo Mwakyembe gooo!!!
 
Angalau sasa watanzania tunaweza kufuta ile kauli ya kubezwa na kudharauliwa iliyopata kutolewa na Rais Kagame wa Rwanda kuwa ati tumpe bandari yetu atufundishe namna ya kutenda kazi(kukusanya mapato kikamilifu,kufuta urasimu,kuboresha huduma na kuondoa msongamano).goo goo gooo gooo Malafyale,goo Mwakyembe gooo!!!

wanajf waliofukuzwa bandarini kwa habar zilizopo wengi ni wachaga.hawa jamaa siwaelewi wanapenda mshiko regardles halali ama sio halali.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom