Mwakyembe, mburuze mahakamani Lowassa kesi ya Richmond

Mwakyembe, mburuze mahakamani Lowassa kesi ya Richmond

Itakuwa vizuri ili tujue embe mbichi na mbivu ni zipi!!!!
Mwakyembe kashika wizara ya sheria ambako kuna wanasheria wa serikali na waendesha mashtaka nguli waliobobea katika fani za sheria na wenye weledi mkubwa.

Mwakyembe wafurahishe na uwatendee haki watanzania,Kutana na wanasheria wako wizarani hapo mburuzeni Lowassa MAHAKAMANI kesi ya RICHMOND na angalieni na maeneo mengine aliyotupiga watanzania kwa kutuibia.

Chonde chonde Mwakyembe tusaidie watanzania.Wanasheria msaidieni Mwakyembe.Naamini wanasheria watakaoikalia vizuri hiyo kesi si ajabu wakaja kuwa marais baada ya Magufuli kumaliza awamu zake.
 
Hakuna degree isiyo kuwa na ajira kinachosumbua n miundo mbinu mibovu ambayo unakutwa imewekwa na government...... Kama school of law hainaajira basi ifutwe!!!!!!!

School of law haiwezi kufutwa kwa ajili ya mtu asiye na ajira.Wanaosoma School of law wengine wanasomeshwa na kampuni zao.Mfano mtu unakuta ana chuo au kampuni hana mwanasheria.Anaaamua kupeleka mwanae au ndugu yake akasome School of law aje awe mwanasheria wa kampuni au chuo chake.

Kampuni pia za wanasheria husomesha ndugu zao wakiona kazi za sheria zinaongezeka.Tatizo ni wewe kusoma bila kujua ukimaliza unaenda wapi unabaki kubwatukia serikali.Ni sawa na kusomea udereva. Si kila anayesomea udereva anataka kazi ya udereva mwingine anasoma akaendeshe gari yake.Huwezi sema wewe unayesomea udereva ili uajiriwe kwa kuwa ajira za udereva hazipo serikalini basi kozi za udereva zifutwe vyuoni.Ni mawazo finyu.
 
aliyekuwa waziri wa nishati na madini kipindi hicho ndo mwizi mwenyewd
 
Mwakyembe ni mjanja mjanja sana ni mchapa kazi lakini hapo hapo huwa ni mwizi balaa sanjari na mnafiki mkubwa na mbinu mbalimbali za kimataifa ndiyo maana wakati mwingine hupata Wananchi wanaomwona na shujaa na mwadilifu , lakini kiundani Mwakyembe ni mwizi mkubwa.


Ndio formula ya ufisadi ilivyo .
Ukiona kiongozi ni mchapa kazi sana katika mfumo wa kibepari basi ujue huyo ananafasi kubwa ya kukumbatiwa na matajiri kwa kupewa offer na zawadi nyingi za kumtuliza.
Mafisafi na matajiri hawawezi wakamfuata kiongozi legelege kwa mamilioni.

Hata majambazi yakitaka kushirikiana na mapolisi wanatafuta wale wenye uwezo wa kuwakamata na kutibua dili zao.
 
Sijui Hidaya labda nimekosea Jina lako anyway mwanzisha Uzi, sijafahamu ulikuwa Na umri gani Na Elimu gani kipindi kile 2008 Mheshimiwa Sana Former PM Edward Ngoyai Lowassa Kwa hiyari yake mwenyewe alipoamua kujiuzulu uwaziri mkuu on Richmond Secandal pale bungeni.
Sio kama mawaziri we2 wa Leo wanao ngan'ngania mpaka 2uandamame regardless wamekumbwa Na scandal kubwa namna gani.2umeona Escrow.EPA.operations 2komeza.nk

Kesho yake mara Baada ya Mh.Lowassa kujiuzulu Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Na Amiri Jeshi Mkuu by zen Ndg J M K alihojiwa Na waandishi wa Habari Na kuuwambia uma Na dunia Kwa ujumla kwamba waziri wake mkuu "HAHUSIKI NA WIZI WA AINA yoyote" Bali kilicho 2okea ni "AJALI YA KISIASA" 2 AND CAN HAPPEN 2 ANYONE in Politics as collective responsibility" sasa we Hidaya hizo chonde chonde unapingana Na Rais wako? We unajua sana kuliko yeye?

Huyu m2 uanyesema afunguliwe Kesi awekwe ndani ili Mwakyembe awafurahishe watanzania ni watanzania wapi Hao wanaofurahishwa? Je Hidaya anafahamu Kuwa kwa mujibu wa jaji babu lubuva huyo Ndg ameaminiwa Na watanzania Over 6 mil. Nje ya wale mil.kumi Na-v waliopiga kura. Minus 8 mil. Iliyosemekama hawakumchagua? Swali; Hidaya wapi unaweza kuzi2unza hasira za Hao watanzania mil.6 waliomuamini kuumpa nchi awaongoze? Au ukimya umekuduwaza akili? Use your common sense kabla hujaandika ama kuanzisha Uzi.




Muulize tu dili za mabilioni ya ESCROW zilipigwa na watu wa ukanda fulani. Na leo huo ukanda ndio uliotoa mawaziri 10. Kuna nini hapo kama sio mtandao uliokua umejificha.
Mwakyembe kwanza atafute wale waliokuwa wamempiga ----- mpaka akanyonyolewa nywele baada ya kusema atamtaja mmiliki wa Richmond na nchi itikisike.

Na pia aunde tume ichunguze chanzo cha ugonjwa wa Lowasa na Mrema nini!!. Mana Lowasa alijiuzulu akiwa askari wa mwavuli lakini ghafla hali yake ikabadilika.
 
Back
Top Bottom