Mwakyembe: Maisha yangu yapo hatarini

Mwakyembe: Maisha yangu yapo hatarini

Status
Not open for further replies.
Mwakyembe bila shaka ile sumu aliyolishwa haijaisha mwilini na ndio maana anasema maisha yake yako hatarini!! Usanii wake ndio utamponza kwani wakati ule anaugulia alisema kuwa angewataja hadharani wale waliomfanyizia lakini kama alivyofanya kwenye ripoti ya Richamond hakufanya hivyo. Ni vigumu sana kumuamini huyu bwana anapotoa tamko lolote lile.
 
Watu wanaojificha nyuma ya keybodi MNA shida sana. Nani anajua mwakiembe ana vichekesho zaidi yako?
Sasa kama alikana andiko lake si ndio vichekesho vyenyewe? Au kwenda kwenye press wakati aliyetekwa ni mwingine si ndio vichekesho vyenyewe? Au kutishia kuzui TLS kufanya uchaguzi wake si ndio komedi yenyewe?
 


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema maisha yake yapo hatarini, amesema "pamoja na kuwa hawezi kulinganisha miaka saba iliyopita na sasa lakini bado maisha yangu hayako salama."

Akizungmza na Gazeti la MWANAHALISI, Dk Mwakyembe amesema "Siwezi kuwa salama siwezi kuwa naweza kutumia uhuru wangu wa kwenda kokote nikakota au wakati wowote ninaotaka.

"kwamba naweza kutumia uhuru wangu huo kama unavyotakiwa na katiba bado nina hofu ya maisha yangu ingawa siyo kama ilivyokuwa miaka ya mitano iliyopita " ameeleza DK Mwakyembe.

DK Mwakyembe alikuwa ni mmoja wa watu waliotajwa kwenye orodha ya wanaotishiwa maisha.
wengine wanaotajwa kwenye orodhra hiyo ni pamoja na Dr Willibrod Slaa.

kauli ya Dk Mwakyembe imekuja siku tano baada ya watu wasiojulikana kumteka na kumtesa mwanamuziki Ibrahim Musa (Roma Mkatoliki).

Dk Mwakyembe aliwahi kuripoti Februari Mwaka 2011 kuwepo kwa hatari ya kutokomeza maisha yake.

MWANAHALISI
 
Mpuuzeni huyu mwoga wa kufa, mara usalama wa taifa, mara vodacom mara caspian, mara el shabaab mara wakabaji mara waganga...
Tumuulize ripoti ya kamati aliyounda mtangulizi wake kaifanyia kazi? Au ndo huyo mtuhumiwa anamtishia maisha?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom