Mwakyembe: Maisha yangu yapo hatarini

Mwakyembe: Maisha yangu yapo hatarini

Status
Not open for further replies.
Huyu Mwakyembe ukweli wake ni kutiliwa shaka...

Amefanya nini hadi aone kuwa usalama wake upo hatarini????!

Na ni akina nani hao wanaotishia usalama wake???!!!

Mtu huyu aliwahi kutoa madai kama hayo miaka ya nyuma, na akadai kuwa ametoa taarifa kwa IGP akiambatanisha na alivyoviita vielelezo/ushahidi.

Sasa kama anaona hilo lipo, yeye ni mwanasheria hivyo anaelewa taratibu. Zaidi ya yote yeye yupo katika kundi la watawala, sasa analalamikia wananchi ili iweje??

Awataje kwa uwazi hao wanaomtishia, pia aseme sababu ni nini.

Vinginevyo naomba wananchi tuamini kwamba huyu mtu anatafuta huruma yetu, hasa baada ya yeye kubaini kuwa wananchi tumepoteza imani naye kutokana na matendo yake ya hovyo dhidi ya umma.
Kama aliwahi kukana PhD yake hamna namna tumpuuze tu
 
Kuna kitu kinakuja kikubwa,na watanzania tulivyo litatubeba sana
 
Jamani huyu kiongozi wa serikali ya ccm anatuchanganya.
Wao ndo wanamajeshi yote mpaka ya ziada wasiojua hata askari wake,kama yule aliyemuonyesha nape bastola !
Sasa kiongozi huyu akilalamikia usalama wake,wakati anatu
mia nguvu na akilizake zote kulinda ccm,ataeleweka kweli ?
Hapa kuna jambo kubwa sana analotafuta huyu waziri.mzee usitafute watu wachangie ili muwapeleke kisutu.huna lolote ni kakomedi kako na wewe ueanzisha.
Dada yang Joyce, usiichoshe akili yako kwa ajili ya mtu huyu.

Black & white ya bwana huyu ni hii:

Ametoa madai hayo kwa sababu ameshabaini kuwa umma wa Watanzania haupo naye hivyo ameshadharauliwa na amechukiwa sana.

Na hiyo ni kutokana na vitendo vyake vya kinafiki na uzandiki kwa kuusaliti na kuupuza umma.

Hivyo anataka kupata huruma ya wananchi kwa kuamini kuwa akizua hilo alilozua watu watamuonea huruma kama kipindi kile alichodai kupewa sumu.

Ambacho hajiku ni kwamba, wananchi wana akili ya kupambanua mambo na kwamba sio wajinga kama anavyofikiria.

Asituumize Vichwa.
 
" Kwenye serikali yangu, sitaweka wazee.. maana wazee ndo wametufikisha hapa tulipo"..... kuna muda ni bora kunyamaza kuliko kutoa speech
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema maisha yake yapo hatarini, amesema "pamoja na kuwa hawezi kulinganisha miaka saba iliyopita na sasa lakini bado maisha yangu hayako salama."

Akizungmza na Gazeti la MWANAHALISI, Dk Mwakyembe amesema "Siwezi kuwa salama siwezi kuwa naweza kutumia uhuru wangu wa kwenda kokote nikakota au wakati wowote ninaotaka.

"kwamba naweza kutumia uhuru wangu huo kama unavyotakiwa na katiba bado nina hofu ya maisha yangu ingawa siyo kama ilivyokuwa miaka ya mitano iliyopita " ameeleza DK Mwakyembe.

DK Mwakyembe alikuwa ni mmoja wa watu waliotajwa kwenye orodha ya wanaotishiwa maisha.
wengine wanaotajwa kwenye orodhra hiyo ni pamoja na Dr Willibrod Slaa.

kauli ya Dk Mwakyembe imekuja siku tano baada ya watu wasiojulikana kumteka na kumtesa mwanamuziki Ibrahim Musa (Roma Mkatoliki).

Dk Mwakyembe aliwahi kuripoti Februari Mwaka 2011 kuwepo kwa hatari ya kutokomeza maisha yake.

MWANAHALISI
Sasa Serikali Yenyewe inaogopa na Mwananchi wa Kaida atasemaje Sasa au Maisha Yake yapo hatarini kivipi c zaidi ya Mwakyembe Sasa?
 
Tusidharau kauli kama hizi kwani mwanzo wa ngoma ni lele na tukumbuke yalishamkuta huyu huyu na akapigania roho yake hakuna aliyejua kama atapona.......huyu ni mtu mkubwa Serikalini hawezi kueleza hovyo hovyo tu jambo kama hili, kifupi hakuna aliye salama kwa sasa.
 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema maisha yake yapo hatarini, amesema "pamoja na kuwa hawezi kulinganisha miaka saba iliyopita na sasa lakini bado maisha yangu hayako salama."

Akizungmza na Gazeti la MWANAHALISI, Dk Mwakyembe amesema "Siwezi kuwa salama siwezi kuwa naweza kutumia uhuru wangu wa kwenda kokote nikakota au wakati wowote ninaotaka.

"kwamba naweza kutumia uhuru wangu huo kama unavyotakiwa na katiba bado nina hofu ya maisha yangu ingawa siyo kama ilivyokuwa miaka ya mitano iliyopita " ameeleza DK Mwakyembe.

DK Mwakyembe alikuwa ni mmoja wa watu waliotajwa kwenye orodha ya wanaotishiwa maisha.
wengine wanaotajwa kwenye orodhra hiyo ni pamoja na Dr Willibrod Slaa.

kauli ya Dk Mwakyembe imekuja siku tano baada ya watu wasiojulikana kumteka na kumtesa mwanamuziki Ibrahim Musa (Roma Mkatoliki).

Dk Mwakyembe aliwahi kuripoti Februari Mwaka 2011 kuwepo kwa hatari ya kutokomeza maisha yake.

MWANAHALISI
He trying to attract sympathy when all that he has from the people is hate caused by his hypocrisy
 
560c093c1129e325306998fcb13ba97b.jpg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom