comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema maisha yake yapo hatarini, amesema "pamoja na kuwa hawezi kulinganisha miaka saba iliyopita na sasa lakini bado maisha yangu hayako salama."
Akizungmza na Gazeti la MWANAHALISI, Dk Mwakyembe amesema "Siwezi kuwa salama siwezi kuwa naweza kutumia uhuru wangu wa kwenda kokote nikakota au wakati wowote ninaotaka.
"kwamba naweza kutumia uhuru wangu huo kama unavyotakiwa na katiba bado nina hofu ya maisha yangu ingawa siyo kama ilivyokuwa miaka ya mitano iliyopita " ameeleza DK Mwakyembe.
DK Mwakyembe alikuwa ni mmoja wa watu waliotajwa kwenye orodha ya wanaotishiwa maisha.
wengine wanaotajwa kwenye orodhra hiyo ni pamoja na Dr Willibrod Slaa.
kauli ya Dk Mwakyembe imekuja siku tano baada ya watu wasiojulikana kumteka na kumtesa mwanamuziki Ibrahim Musa (Roma Mkatoliki).
Dk Mwakyembe aliwahi kuripoti Februari Mwaka 2011 kuwepo kwa hatari ya kutokomeza maisha yake.
MWANAHALISI
========
Hii Habari imekanushwa.
Kwa habari zaidi soma=>Wizara ya Habari yakanusha habari ya gazeti la MwanaHalisi kuhusu Mwakyembe