Mwakyembe: Joshua Nassari akamatwa akiwa anataka kuingia bungeni na Chupa ya kilevi akiwa amelewa

Kama ni kweli basi huyo ni mjinga. Kwani hajui taratibu za pale Bungeni? Wabunge wa upinzani hawatakiwi kufanya mistakes za kipumbavu pumbavu namna hiyo. Wanapaswa kujua "wanawindwa" kwa kila namna; any trivial mistake ni furaha kubwa sana kwa adui.
 
Kijana mdogo kama huyo kukamatwa pombe ni fedhea kubwa kwa wapiga kura wake.

Inaonyesha hajui Nini wajibu wake katika kipindi hiki cha bunge la bajeti.

Hii ndio maana hata bunge kutorushwa live ni sahihi.
Utategemea Nini kutoka kwa wabunge model hii?. Ni matusi na viloja.
 
Mtoto wa Pastor kunywa pombe huyo si wa kwanza kama ni kweli, ila mleta mada dadafua kwa maelezo kidogo manake watanganyika kwa kutoa hukumu bila kubalance habari hatushindwi japo ni kosa kabisa kuzusha na kuhitimisha bila ushahidi...
 
Nataka uthibitisho ili niweze kuamini. Vinginevyo naichukulia kama uzushi usio na maana!
 
Kuna mtu alisema hakuna cha profesa wala profyoko. Mtu akiwa profyoko kuna kiwango cha utahira kinaongezeka nadhani.
Maprofesa wa ukweli ni lazima ugoogle ndo utawaona
 
Haishangazi hilo, mods wenyewe si ndio kina marehemu Isango, ila hili lazima tulishupalie tu, haiwezekana mbunge kwenda bungeni akiwa amelewa pombe, ndio maana wengine wanaishia kutukana matusi ya nguoni kabisa kumbe akili za pombe na bangi.
Na ndio sababu kunwa kubwa sana walipinga hoja ya kuwekwa vifaa vya kupimwa ulevi mlangoni wanapoingia...hahaha
 
Naamini tetesi zilizosema kuwa baada chadema kushindwa 2015, miongoni mwa mikakati ilikua ni kumnunua mange kimambi na kuiteka jamii forum kuhakikisha hakuna zuri la serikali litapewa nafasi, na pia kulinda maslahi ya wanachadema bila kujali maovu yao.....[HASHTAG]#konyagibungeni[/HASHTAG]...
 
Swala la ulevi kwa wabunge wetu limekuwa tatizo sugu. Hii ni aibu kwa Taifa kuwa na wabunge wasiotambua wajibu wao kwa wananchi. Kuingia Bungeni akiwa amelewa muda wa kazi ni dharau kwa wana arumeru mashariki ambao wamemwamini na kumpa jukumu la kuwawakilisha bungeni. Sioni kama ni sahihi kwa wabunge wa aina hii , wasioheshimu wajibu wao kurudi tena bungeni bunge lijalo.

Mh. Spika tunakuomba uwe unaweka waangalizi kwa wabunge kabla ya kuingia bungeni, ili kuepusha aibu kama hii, na kuligeuza bunge letu kijiwe cha wahuni.
Hoja ni Richmond.Sio konyag
 
Hana lolote Mwakyembe ni njaa tu inamsumbua. Hapo ajibu hoja aache kulalama, eti ibueni tena hoja ya Richmond, kwani yeye hawezi kuibua? Mtaibuaje wakati hela mshawalipa akina PAP aache kutishia watu nyau.
Kwa hili nakubaliana na Mwakyembe

Upinzan Tanzania hakuna hata mmoja.Dr.Slaa ndiye alikuwa mpinzan wa kweli

CDM wanakula matapishi yao.N vgumu kabisa upinzan kuchukua nchi kama Lowasa mlimwita fisadi namba moja then mnakuja kumsafisha nakukumpa nafas kugombea uraisi.Shame on you guys!!
 
Hata mama yake mzazi hawezi kujihaminisha hivyo kwa mwanae..so strange wewe mtu baki unajiaminisha kwa 100%
Rudia tena hayo maandishi yangu halafu unambie hiyo 100% nimeisemea wapi? Soma uzi wa mtu ukiwa huna ushabiki then utachangia pia ukiwa umeelewa uancho changia, ulicho kifanya hapa ni hasira tu wala sio mchango.
But again, kwa kua nimepewa ubongo kichwani na ninawajua sana hawa watu wa magamba still nina mashaka na taarifa ya mwakiwembe, naomba kujua baada ya kupimwa dogo janja alikutwa na alcohol % ngapi? Msanii darasa aliimba, acha maneno weka music. Mzee wa upako alikutwa na pombe na akaenda kupimwa na tukatangaziwa kiasi cha pombe alichokua nacho, Nasari alikutwa na ngapi? Kusema tu alikutwa na chupa ya Konyagi that is not a case, yawezekana kwenye hiyo chupa ya Konyagi kuna Asali, who knows? But remember yote hayo yamekuja baada ya kugusia issue ya Richmond, kwangu mimi issue ya Richmond still ni dude Fulani lililojificha; lina siri yake kubwa huko serikalini so kusikia na Nasari nae amekunywa but with no vipimo lazima nitie mashaka. Kumbuka sijasema hakunywa, nimetengeneza tu maswali kichwani.
 
Back
Top Bottom