Mwakyembe: Joshua Nassari akamatwa akiwa anataka kuingia bungeni na Chupa ya kilevi akiwa amelewa | Page 12 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe: Joshua Nassari akamatwa akiwa anataka kuingia bungeni na Chupa ya kilevi akiwa amelewa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ALWATAN KIZIGO, Apr 20, 2017.

 1. ALWATAN KIZIGO

  ALWATAN KIZIGO JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2017
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 522
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 80
  Leo Bungeni Dodoma, Joshua Nasari(Mb) Arumeru Mashariki amekamatwa na Watu wa Usalama akiwa amelewa huku akiwa na chupa akitaka kuingia nayo Bungeni.

  Mb Joshua alipoanza kuchangia alisema kuwa kamati iliyoundwa na Bunge wakati ule wa Rais Kikwete, kumchunguza Waziri Mkuu wa wakati huo Edward Lowassa juu ya tuhuma za Richmond haikutenda haki kabisa.

  Akijibu tuhuma hizo kwa kujiamini kabisa, Mh. Harrison Mwakyembe alisema yafuatayo:

  "Kwanza niwashukuru vijana wa Usalama kwa kutekeleza majukumu yao hasa ya kumshika Mh. Nasari na chupa hiyo ya kilevi, maana angeweza kutapikia bendera ya Taifa hivyo kulidhalilisha Bunge lote kwa ujumla...

  Kuhusu Edward Lowassa na tuhuma hiyo ya Richmond hawezi kusafishika kamwe kwa hali yoyote ile...Tumeshawachoka sana na hatuwezi kuwavumilia tena....

  Kamati yangu iliwahoji zaidi ya mashahidi 75,huku kabla ya kuhojiwa kwake na kamati hiyo Edward Lowassa alikimbilia kujiuzuru ghafla...Sasa bhasi kama kuna mtu yeyote hapa Bungeni anayejiamini alete hoja ya kurudisha tuhuma hizo za Richmond kuhusu Edward Lowassa tuanze kuijadili upya..

  Na siku tukianza kuijadili upya tuhuma hizo, ntamwomba Mh. Rais JPM anipumzishe Uwaziri ili nilishughulikie hili suala kikamilifu.

   
 2. Bams

  Bams JF-Expert Member

  #221
  Apr 21, 2017
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 4,119
  Likes Received: 3,991
  Trophy Points: 280
  Una uhakika na unachoongea au kwa sababu Mwakyembe ametamka? Sidhani kama huyu Mwakyembe ni mtu anayeaminika kiasi cha kuamini kinachotoka kinywani mwake.

  Mwakyembe amepoteza heshima hata ya kuweza kuaminika kutokana na kauli zake za hovyo hovyo siku hizi. Pamoja na unafiki wote wa kujipendekeza kwa JPM sidhani kama atadumu kwenye uwaziri. Sioni kama amewahi ku-deliver chochote tangu alipoingia kwenye siasa.
   
 3. mbikagani

  mbikagani JF-Expert Member

  #222
  Apr 21, 2017
  Joined: Dec 5, 2014
  Messages: 2,428
  Likes Received: 968
  Trophy Points: 280
  UKIWA UNASIMAMA NA KUMTETEA LOWASSA ETI SIYO FISADI, UTAKUWA UNALETA GIZA MBELE YA POPO UKIZANI ATASHINDWA KUONA.
  KAMA WAPINZANI TULIMZOMEA SANA LOWASSA NA KUMSIFIA MWAKYEMBE WAKATI ANAISOMA RIPOTI.
  TUNAPASWA TUSIMAME KWENYE UKWELI ILI WANANCHI WATUELEWE.
   
 4. E

  Eja One JF-Expert Member

  #223
  Apr 21, 2017
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,063
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Wewe unasema mchungaji? Hata baba yake angekuwa Yesu..as long as aliyezaliwa ni binadamu wa kawaida na sio malaika hiyo sio guarantee.
  Me nimesoma chuo na watoto wa wachungaji tena wametoka seminari kule wamezoea divai na wine ni walevi balaaa..
   
 5. E

  Eja One JF-Expert Member

  #224
  Apr 21, 2017
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,063
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Mwakyembe hakusema haya chumbani au uchochoroni...pale ni bungeni..kama amesema uongo mwambieni Lisu aombe mwongozo wa spika alafu hansard ziletwe kama hamjaomba bunge lisirushwe live.
   
 6. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #225
  Apr 21, 2017
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,374
  Likes Received: 6,840
  Trophy Points: 280
  Acha kukurupuka, ni wapi nimemtetea Lowassa? Hivi unajua msimamo wangu toka najiunga JF? Mnazidi kulidhalilisha hili jamvi kwa kelele zisizokuwa za lazima.
   
 7. E

  Eja One JF-Expert Member

  #226
  Apr 21, 2017
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,063
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Bunge sio mahakama na halina uwezo huo...bunge linapendekeza hatua za kuchukua kwa mamlaka yake ya uteuzi..Muulize yule mliyepiga kelele za kummiss alichukua hatua gani
   
 8. Yugu

  Yugu JF-Expert Member

  #227
  Apr 21, 2017
  Joined: Dec 18, 2014
  Messages: 1,073
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  huyu mwakyembe ile sumu imeanza tafuna ubongo.
   
 9. E

  Eja One JF-Expert Member

  #228
  Apr 21, 2017
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,063
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Mkuu, kubenea leo ukimuuliza kama alimwagiwa tindikali anaweza akakukana mita 1000..anaweza sema lile kovu pale usoni aliungua na uji enzi za utoto..hatari sana hawa upinzani
   
 10. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #229
  Apr 21, 2017
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,739
  Likes Received: 860
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe yupo sahihi 100%.Kumsafisha Lowassa inabidi utumie pombe kali kwanza.
   
 11. k

  kabombe JF-Expert Member

  #230
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 16,780
  Likes Received: 9,644
  Trophy Points: 280
  Chadema hakuna mwenye uthubutu wa kumuonya Nasari.Wote wanywa viroba
  Tunaposema chadema ni chama cha wanywa viroba tunamaanisha mambo kama haya ya Mbunge mzima kuingia bungeni na konyagi
   
 12. mbikagani

  mbikagani JF-Expert Member

  #231
  Apr 21, 2017
  Joined: Dec 5, 2014
  Messages: 2,428
  Likes Received: 968
  Trophy Points: 280
  IF THAT THE CASE, KIJANA ANAPASWA AWEKWE KITIMOTO ASEME NINI KIMEMSIBU.
   
 13. E

  Eja One JF-Expert Member

  #232
  Apr 21, 2017
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,063
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Akili yako nzito sana aisee...Yaani aliyekuwa m/kiti wa iliyokuwa kamati teule ya bunge ya kuxhunguza sakata la Richmond aende mahakamani??? Hivi unajua mamlaka ya bunge yanaishia wapi aisee??
   
 14. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #233
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,996
  Likes Received: 6,704
  Trophy Points: 280
  In short ...ufisadi wa EL is not questionable?
   
 15. E

  Eja One JF-Expert Member

  #234
  Apr 21, 2017
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,063
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
   
 16. TUNDALI

  TUNDALI JF-Expert Member

  #235
  Apr 21, 2017
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 60
  Huyu Bwana Nassari wakati anaanza kuomba kura jimboni kwake kila Mkutano wake alianza na sala na kumaliza na sala, Sasa alishapata Ubunge kasahau kusali amegeukia Pombe hadi Bungeni...! Hii ni Laana kwake.
   
 17. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #236
  Apr 21, 2017
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,925
  Likes Received: 3,175
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa upinzani leteni Hoja, bungeni
   
 18. flagship

  flagship JF-Expert Member

  #237
  Apr 21, 2017
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 1,625
  Likes Received: 1,069
  Trophy Points: 280
  Mwakieeembe ni shangingi wa madaraaaa madaraaa.
   
 19. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #238
  Apr 21, 2017
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 9,919
  Likes Received: 5,258
  Trophy Points: 280
  Dr Mwak, prof Majimarefu, prof Lipu nawaweka kapu moja
   
 20. flagship

  flagship JF-Expert Member

  #239
  Apr 21, 2017
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 1,625
  Likes Received: 1,069
  Trophy Points: 280
  Wakiongozwa na kitwanga.
   
 21. C

  COPPER JF-Expert Member

  #240
  Apr 21, 2017
  Joined: Dec 28, 2012
  Messages: 1,821
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Maam
  Yalikuwa maazimio ya Bunge na sio kamati ya Mwakyembe.
   
Loading...