Mwakyembe avutia pumzi 'unga' airport

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Kufuatia matukio mfululizo ya kukamatwa kwa watuhumiwa wa dawa za kulevya wanaodaiwa kuwa ni Watanzania kwenye viwanja vya ndege nje ya nchi wakipitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema atalishughulikia suala hilo kama alivyofanya bandarini.

Dk. Mwakyembe ambaye wizara yake ndiyo yenye dhamana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati wa mazungumzo maalumu na NIPASHE kuhusu ufuatiliaji wa vitendo hivyo vinavyoharibu taswira ya nchi kimataifa.

Alisema anafahamu kila kitu kuhusu matukio ya dawa za kulevya, lakini anasubiri mamlaka zilizo chini yake kama vile TAA na bodi yake, uongozi wa JNIA na Polisi, ili wafurukute kwanza kama alivyofanya bandarini kwa lengo la kupima utendaji wao wa kazi.

"Mamlaka ni ‘system', ina ngazi zake, kuna Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na bodi yake, kuna polisi, kuna uongozi wa uwanja wa ndege. Nataka muwabane kwanza hao ili wawaeleze hayo (ma)dawa ya kulevya yanapitaje hapo? Mimi najua kila kitu kuhusu kinachoendelea na iwapo wanawazungusha njooni kwangu," alisema Mwakyembe na kuongeza:

"Haiwezekani ukaenda moja kwa moja kwa Rais, iwapo kuna suala linalomhusu Waziri, atakushangaa na kukuona huelewi kitu. Najua hatua ilipofikia na iwapo kuna mamlaka haijachukua hatua yoyote, mimi nitaishughulikia. Na kama imepita kote na imefikia kwa DPP, najua imefika ngazi ya kiwizara, ni lazima tulishughulikie."

Dk. Mwakyembe aliongeza kuwa, anajua mtandao wa dawa za kulevya ni mrefu, lakini atashughulikia kama alivyofanya katika Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kwani baada ya kusikia ubovu unaotendeka aliwaacha wafurukute kwanza kwa takribani wiki mbili.

Alisema baada ya wiki hizo mbili akiwa na taarifa kamili kuhusu kilichokuwa kinaendelea, aliingia bandarini hapo na kuwafumua baadhi ya watendaji na kwamba ndivyo itakavyokuwa katika mamlaka zinazohusika na viwanja vya ndege kwani kwa sasa anasuburi kuona wanafanya nini kabla hajaingilia kati.

Agosti 27, mwaka jana, Waziri Mwakyembe aliunda Kamati ndogo ya Uchunguzi ya watu saba kubaini chanzo cha matatizo yanayozorotesha ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam na hivyo kukimbiwa na wateja wa ndani na nje ya nchi.

Baada ya uchunguzi huo, Dk. Mwakyembe aliwaondoa wajumbe wote wa Bodi ya TPA na kuteua wapya ili kuweka mazingira mazuri ya utekelezaji wa taarifa hiyo.

Juzi gazeti hili liliwasili katika ofisi za TAA, kwa lengo la kujua kinachoendelea kuhusu matukio hayo, lakini mmoja wa wafanyakazi katika ofisi hizo alisema Mkurugenzi wa mamlaka hiyo yupo, lakini asingeweza kuzungumza na waandishi bila kuruhusiwa kwanza na katibu wake wa mambo ya sheria, Ofisa Uhusiano na mwingine wa tatu ambao nao hawakuwapo hapo ofisini.

Mfanyakazi huyo wa kike ambaye alikataa kutaja jina lake wala cheo chake, alisema ofisi ya Mkurugezni ina watu watatu na utaratibu uliowekwa ofisini hapo ni kwamba, iwapo wafanyakazi hao wote hawapo, hakuna huduma itakayotolewa kwa mtu mwenye shida na Mkurugenzi kwa kuwa hataruhusiwa kumwona.

Hata hivyo, NIPASHE ilifanikiwa kumwona Mkurugenzi wa JNIA, Moses Malaki, ambaye naye alidai kwamba, hawezi kuzungumzia sakata hilo kwa madai kwamba hashughulikii masuala ya dawa za kulevya.

Malaki alisema wanaohusika na suala hilo ni polisi kwa kuwa JNIA wanahusika na masuala ya wasafiri na kwamba anayeweza kuzungumzia sakata hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Suleiman Suleiman.

Wakati wa mazungumzo na gazeti hili ofisini kwake siku hiyo, Malaki, alimpigia simu Suleiman ambaye aliahidi kukutana na NIPASHE jana saa 5 asubuhi ili kutoa ufafanuzi wa sakata hilo.

Hata hivyo, jana mwandishi wa habari hizi alikwenda ofisini kwa Mkurugenzi huyo na kutaarifiwa kwamba amsubiri kidogo kwa sababu yupo kwenye kikao.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa saa nne, katibu muhtasi wa mkurugenzi huyo alimweleza mwandishi kwamba bosi wake amekataa kuzungumzia jambo hadi atakapokuwa tayari.

CHANZO: NIPASH

MMmmmm.... "Mchagua jembe si mkulima" – Swahili Proverb
Roughly translates to "One who is picky about his hoe is not a real farmer."
 
Namkubali Dk. Mkwakyembe. Naamini anatafanya kazi hiyo. Lakini kusema kwamba atageukia airport, nadhani ni kutaka kusema kwamba hiyo mihadarati ibaki humu humu ndani!

Nasema hivyo kwa sababu njia kuu ya kuingiza mihadarati ni ya bahari. meli na majahazi vinatumika sana kuingiza sumu hiyo. Kinachotakiwa hapa ni kuimarisha doria na ukaguzi wa kutosha kwenye bandari na maeneo yote ya bahari. Hii mihadarati inayosafirishwa kupitia airport ni sehemu ndogo sana ya mzigo mzima uliopo nchini.

Namshauri aanze huko bandarini.
 
Songa mbele Dr. Mwakyembe pambana tu huna cha kupoteza maana kama ni sumu ulishakunywa na kama ni kifo ulishakinusa. Hakuna kitu kipya watakachokutisha nacho.
 
Suleiman Suleiman Mkurugenzi TAA naye ni muuza unga (anaogopa kuzungumzia biashara yake haramu)
Ile list aliyonayo Dhaifu inaongezeka..
 
Ile collective responsibility kama ya Richmond huwa ina apply kwenye nishati tu au hata TFF wanaweza kuifuata pia?????
 
We have been in this shit for years now Tatizo la madawa ya kulevya halitakaa liishe Tanzania, kwasababu wanaohusika ndio wenye Tanzania na ndio wenye dola na ndio kila kitu.

Mimi nimekuwa katika hii biashara kwa muda mrefu sasa na nina mafanikio ya kutosha , nisingefanya hii biashara nisingeweza fanya mambo mengi niliyoyafanya katika umri mdogo na kamwe hakuna mtu ambaye atafanya hii biashara ikamtupa angalia hapa Instagram , ninajenga kituo cha polisi kwa fedha zangu hapa Dare es salaam ili nyinyi raia nikiwemo na mimi tulindwe, haya madawa yanapita tuu hapa tanzania hakuna mtanzania mwenye kuyatumia sana, ni punje tuu, pesa nyingi zinatoka nje.

Muheshiwa huyu ni ngumu kumkamata kwasababu ushahidi hakuna anayeweza kuupata RUGS LORDS wako very smart, punda na waswaga punda mara nyingi ndio huwa wanakamatwa, hata mimi wakija polisi hawatapata ushahidi wowote wa kunipeleka mbele za sheria, coz NO EVIDENCE AM NOT GUILTY,..FINISHED...

Cha kushauri nyie vijana wa KItanzania acheni kutumia madawa ili soko liwe hakuna, ila as long as demnad is high, supply is minimal price will be high and that commodity will be expensive and everyone will be looking for it, Kama iyo barua inavyojionesha ni dhahiri kabisa hao wanaosemwa hata polisi inawajua ila uthibitisho ndio hakuna..na kuna viongozi na wafanyabiashara wakubwa hapa tz wanafanya hii makitu, na kuna uwezekano mkubwa tukapata Presoo drug lord, tehe tehe
 
Dr. Mwakyembe is one of Heroes Tanzania has today; he has suffered and almost lost his life defending the country. Many of us traveling on Tanzania passports find it increasingly difficult to even transit through some countries. We are constantly being profiled as peddlers.

You wonder why you are being inhumanly searched in both Asia and Europe not knowing someone from Tanzania is running a global drug syndicate that is now making every Tanzanian a potential mule

This is a national embarrassment, and will be so glad to see Hon. Mwakyembe pass a broom in this sensitive organ; the main airport, that is now the conduit to drug consignments. It is a national disgrace, and a HERO is needed to save the face of the nation. Go for it Dr. Mwakyembe, the country is behind you!
 
Namkubali Dk. Mkwakyembe. Naamini anatafanya kazi hiyo. Lakini kusema kwamba atageukia airport, nadhani ni kutaka kusema kwamba hiyo mihadarati ibaki humu humu ndani!

Nasema hivyo kwa sababu njia kuu ya kuingiza mihadarati ni ya bahari. meli na majahazi vinatumika sana kuingiza sumu hiyo. Kinachotakiwa hapa ni kuimarisha doria na ukaguzi wa kutosha kwenye bandari na maeneo yote ya bahari. Hii mihadarati inayosafirishwa kupitia airport ni sehemu ndogo sana ya mzigo mzima uliopo nchini.

Namshauri aanze huko bandarini.

Mkuu Mwakyembe kufanya hicho anachopanga nasema hawezi kwani bila Kikwete kuonyesha juhudi yeye kama waziri hawezi na ataishia kugeuzwa mzungu kabisa maana ile ya albino cha mtoto.
 
Inaonekana wewe ni mmoja wa hao DD's ndio maana inafurahia mateso aliyoyapata Mwakyembe,kwamba mtambadilisha awe mzungu kabisa
 
Namkubali Dk. Mkwakyembe. Naamini anatafanya kazi hiyo. Lakini kusema kwamba atageukia airport, nadhani ni kutaka kusema kwamba hiyo mihadarati ibaki humu humu ndani!

Nasema hivyo kwa sababu njia kuu ya kuingiza mihadarati ni ya bahari. meli na majahazi vinatumika sana kuingiza sumu hiyo. Kinachotakiwa hapa ni kuimarisha doria na ukaguzi wa kutosha kwenye bandari na maeneo yote ya bahari. Hii mihadarati inayosafirishwa kupitia airport ni sehemu ndogo sana ya mzigo mzima uliopo nchini.

Namshauri aanze huko bandarini.

Kuna thread nime ku mention
nimeuliza nyinyi journalist hamuwezi kutusaidia kuwajua waliotajwa na Masogange
huko SA?
hamuwezi hata kumuuliza Manumba?
 
issue iliyopo hapa ni nani atamfunga paka kengele?

Maana huu mtandao wa madrugdealers ni mkubwa sana na wana watuwao hadi kwenye vyombo vyetu vyausalama#
 
Kabla Mwakyembe hajasafishahiyo airport tunataka kwanza
waliohusika na ya Masogange wajulikane
 
Alisema anafahamu kila kitu kuhusu matukio ya dawa za kulevya, lakini anasubiri mamlaka zilizo chini yake kama vile TAA na bodi yake, uongozi wa JNIA na Polisi, ili wafurukute kwanza kama alivyofanya bandarini kwa lengo la kupima utendaji wao wa kazi.

"Mamlaka ni ‘system', ina ngazi zake, kuna Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na bodi yake, kuna polisi, kuna uongozi wa uwanja wa ndege. Nataka muwabane kwanza hao ili wawaeleze hayo (ma)dawa ya kulevya yanapitaje hapo? Mimi najua kila kitu kuhusu kinachoendelea na iwapo wanawazungusha njooni kwangu," alisema Mwakyembe na kuongeza:

Mh. Mwakyembe hiki si kipindi cha kutegeana bali unapaswa kuchukua hatua ili kutimiza wajibu wako. Haimsadii kijana ambaye kesho atakuwa mhanga wa madawa kwakuwa mh. Waziri "anataka kupima utendaji" wa vyombo vyenye jukumu la moja kwa moja. Sasa kutakuwa na tofauti gani kati ya wewe na yule aliyesema analist ya wauza madawa wote na bado hakuna hatua iliyochukuliwa.

Madawa ni tatizo linalowakumba vijana wa kitanzania, na zaidi linaiweka nchi yetu katika aibu ya kuwa kituo cha kusambaza madawa, tunahitaji kukusanya nguvu kama watanzania na kuweka siasa pembeni kushughulikia na tatizo.
 
Back
Top Bottom