Mwakyembe avutia pumzi 'unga' airport

Mwakyembe avutia pumzi 'unga' airport

Kufuatia matukio mfululizo ya kukamatwa kwa watuhumiwa wa dawa za kulevya wanaodaiwa kuwa ni Watanzania kwenye viwanja vya ndege nje ya nchi wakipitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema atalishughulikia suala hilo kama alivyofanya bandarini.

Dk. Mwakyembe ambaye wizara yake ndiyo yenye dhamana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati wa mazungumzo maalumu na NIPASHE kuhusu ufuatiliaji wa vitendo hivyo vinavyoharibu taswira ya nchi kimataifa.

Alisema anafahamu kila kitu kuhusu matukio ya dawa za kulevya, lakini anasubiri mamlaka zilizo chini yake kama vile TAA na bodi yake, uongozi wa JNIA na Polisi, ili wafurukute kwanza kama alivyofanya bandarini kwa lengo la kupima utendaji wao wa kazi.

“Mamlaka ni ‘system’, ina ngazi zake, kuna Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na bodi yake, kuna polisi, kuna uongozi wa uwanja wa ndege. Nataka muwabane kwanza hao ili wawaeleze hayo (ma)dawa ya kulevya yanapitaje hapo? Mimi najua kila kitu kuhusu kinachoendelea na iwapo wanawazungusha njooni kwangu,” alisema Mwakyembe na kuongeza:

“Haiwezekani ukaenda moja kwa moja kwa Rais, iwapo kuna suala linalomhusu Waziri, atakushangaa na kukuona huelewi kitu. Najua hatua ilipofikia na iwapo kuna mamlaka haijachukua hatua yoyote, mimi nitaishughulikia. Na kama imepita kote na imefikia kwa DPP, najua imefika ngazi ya kiwizara, ni lazima tulishughulikie.”

Dk. Mwakyembe aliongeza kuwa, anajua mtandao wa dawa za kulevya ni mrefu, lakini atashughulikia kama alivyofanya katika Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), kwani baada ya kusikia ubovu unaotendeka aliwaacha wafurukute kwanza kwa takribani wiki mbili.

Alisema baada ya wiki hizo mbili akiwa na taarifa kamili kuhusu kilichokuwa kinaendelea, aliingia bandarini hapo na kuwafumua baadhi ya watendaji na kwamba ndivyo itakavyokuwa katika mamlaka zinazohusika na viwanja vya ndege kwani kwa sasa anasuburi kuona wanafanya nini kabla hajaingilia kati.

Agosti 27, mwaka jana, Waziri Mwakyembe aliunda Kamati ndogo ya Uchunguzi ya watu saba kubaini chanzo cha matatizo yanayozorotesha ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam na hivyo kukimbiwa na wateja wa ndani na nje ya nchi.

Baada ya uchunguzi huo, Dk. Mwakyembe aliwaondoa wajumbe wote wa Bodi ya TPA na kuteua wapya ili kuweka mazingira mazuri ya utekelezaji wa taarifa hiyo.

Juzi gazeti hili liliwasili katika ofisi za TAA, kwa lengo la kujua kinachoendelea kuhusu matukio hayo, lakini mmoja wa wafanyakazi katika ofisi hizo alisema Mkurugenzi wa mamlaka hiyo yupo, lakini asingeweza kuzungumza na waandishi bila kuruhusiwa kwanza na katibu wake wa mambo ya sheria, Ofisa Uhusiano na mwingine wa tatu ambao nao hawakuwapo hapo ofisini.

Mfanyakazi huyo wa kike ambaye alikataa kutaja jina lake wala cheo chake, alisema ofisi ya Mkurugezni ina watu watatu na utaratibu uliowekwa ofisini hapo ni kwamba, iwapo wafanyakazi hao wote hawapo, hakuna huduma itakayotolewa kwa mtu mwenye shida na Mkurugenzi kwa kuwa hataruhusiwa kumwona.

Hata hivyo, NIPASHE ilifanikiwa kumwona Mkurugenzi wa JNIA, Moses Malaki, ambaye naye alidai kwamba, hawezi kuzungumzia sakata hilo kwa madai kwamba hashughulikii masuala ya dawa za kulevya.

Malaki alisema wanaohusika na suala hilo ni polisi kwa kuwa JNIA wanahusika na masuala ya wasafiri na kwamba anayeweza kuzungumzia sakata hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Suleiman Suleiman.

Wakati wa mazungumzo na gazeti hili ofisini kwake siku hiyo, Malaki, alimpigia simu Suleiman ambaye aliahidi kukutana na NIPASHE jana saa 5 asubuhi ili kutoa ufafanuzi wa sakata hilo.

Hata hivyo, jana mwandishi wa habari hizi alikwenda ofisini kwa Mkurugenzi huyo na kutaarifiwa kwamba amsubiri kidogo kwa sababu yupo kwenye kikao.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa saa nne, katibu muhtasi wa mkurugenzi huyo alimweleza mwandishi kwamba bosi wake amekataa kuzungumzia jambo hadi atakapokuwa tayari.


CHANZO: NIPASH


E bwana naona mambo mazito sasa.
 
Suleiman Suleiman Mkurugenzi TAA naye ni muuza unga (anaogopa kuzungumzia biashara yake haramu)
Ile list aliyonayo Dhaifu inaongezeka..


Mbona watu wa dini fulani ndio wengi sana kwenye masuala ya sembe?Lipumba atasemaje ?ndio hawa second class citizen?
 
Ninaamini bishara ya madawa ya kulevya Tanzania haijafikia katika kiwango cha nchi kama Afghanistan, Pakistan, Colombia, Jamaica, Mexico, etcetera etcetera.

Siamini kama kwa sasa Tanzania kuna drug cartels ambazo zimejipanga kama za nchi ambazo nimezitaja hapo juu ambapo utendaji wake mara nyingi unakuwa wa makini ukijumuisha vitengo kama hitmen, falcons and drug lords wakati mwingine yanajinasibisha kwa utendaji hata zaidi ya makampuni ambayo yanajulikana duniani.

Muda wa kulishughulikia swala hili ni SASA wakati bado hakujakuwa na ngome imara na nina imani na utendaji wa Dk. Mwakyembe even though action and instinct lazima ziwe zaidi ya zile alizotumia wakati alipoifumua Mamlaka ya Bandari nchini (TPA).

I wish Tanzania kungekuwa na waandishi wa habari makini na siyo hawa corrupt, fake and ill-educated.

Badala ya waandishi wa habari Tanzania kufukuzana na vihabari vya vyama vya siasa, wangeweka nguvu zao kwanza kwenye kugundua mtandao na kilichoko nyuma ya biashara hii chafu na kwa kufanya hivyo, wangeweza kuitendea haki jamii na kwa wakati huo huo, wangeweza kutengeneza pesa sana kwa kuuza habari.

Hii inadhihirisha hata hapa Jf pale thread inapokuja kuhusu madawa kwa jinsi inavyopata watu wengi wanaoisoma.

Hakuna habari nyingine Tanzania ambayo ni HOT CATE kwa sasa kama kugundua mtandao wa madawa ya kulevya.

Watu kama Dk. Mwakyembe wanapaswa kupongezwa kwa maamuzi ya busara na yenye hatari mbele yake.
 
Mwakyembe acha longolongo fanya kazi hawa wauza unga wanaliaribu taifa.
 
>Jk Anayo List ya majina yao.
>Mzee Mwinyi alishakumbwa na kadhia hii.
>B.W.MKAPA alishang'aka kuhusu biashara hii
>Sumaye Naye alishatoa tahadhari.
>I.G.P MWEMA anaijua vyema biashara
>ROBERT MANUMBA mambo yamemzidi anamsukumia zigo kamishina 'Nzowa'
>Pinda mpaka takwimu alitutajia

.......AND LIST GOES ON......

Rais Na vigogo wa hili Taifa Wamefyata Mkia.
MWAKYEMBE Ni nani???

Nchi Hii, Bangi na Mirungi, ndio madawa ya kulevya, hizo zingine ni 'UFADHILI WA SERIKALI YETU'.

R.I.P AMINA CHIFUPA(AC)
 
Back
Top Bottom