Kampuni iliyoingia mkataba wa kujenga jengo la abiria Mwanza Airport kulikoni mbona kimya?

tripof

Senior Member
Apr 2, 2024
183
242
Mkataba umesainiwa kwa vishindo na vigelegele ili uwanja wa ndege wa Mwanza uanze kujenga kwa kile kilichosemwa na Mkurugenzi wa TAA kwa dharura iliyopo hapo uwanjani kuboresha huduma.

Magreda yakasombwa site, Msukuma akasifu, Hamis Tabasamu akatabasamu na kusifu na wananchi waliokusanywa wakacheza kwa furaha na kwa imani, tukaambiwa Mama amekwisha toa fedha bilioni 29 na Makalla akasema bilioni 4 za kuanzia zipo zimepelekwa na kukabidhiwa kutoka halmashauri.

Sasa mbona kimya uwanja huu una mkosi gani au Mzawa Taifa Mining Const. Company ya Rostam ndiyo yenye shida? Mbona ni mapema mno kuanza kusuasua na site mobilization? Haka ka mradi ni kadogo sana mbona hivi? Mwanza tuna kiu na mradi huu, Tabasamu aliomba miezi 5 limalizwe hili, tumeteseka kwa vyakutosha.

Mbona TAA hamueleweki kuhusu uwanja huu, acheni siasa mnamwangusha mama kiaina.
 
Bado unaamini Serikali ,sikiliza serikali imewekeza nguvu kujengq Dodoma 😅😅sio Mwanza ... Wakati Mwanza kitambo walitakuwa kuwa na international airport ila wakapuuza sasa uwanja wa msalato wa juzi tu hapa umefika mbali.
 
Kwa nini kuwapotezea muda wananchi wanajidhalilisha kwa uwongo, Tanzania ya leo si ya miaka ya 1950,waangalie sana nadhani wasingempa Rostam,kosa limeanzia hapo pengine.
 
Mkataba umesainiwa kwa vishindo na vigelegele ili uwanja wa ndege wa Mwanza uanze kujenga kwa kile kilichosemwa na Mkurugenzi wa TAA kwa dharura iliyopo hapo uwanjani kuboresha huduma. Magreda yakasombwa site,Msukuma akasifu,Hamis Tabasamu akatabasamu na kusifu na wananchi waliokusanywa wakacheza kwa furaha na kwa imani,tukaambiwa Mama amekwisha toa fedha bn 29 na Makalla akasema bn 4 za kuanzia zipo zimepelekwa na kukabidhiwa kutoka halmashauri. sasa mbona kimya uwanja huu una mkosi gani au Mzawa Taifa Mining const company ya Rostam ndiyo yenye shida mbona ni mapema mno kuanza kusuasua na site Mobilization, haka ka mradi ni kadogo sana mbona hivi, Mwanza tuna kiu na mradi huu, Tabasamu aliomba miezi 5 limalizwe hili,tumeteseka kwa vyakutosha. Mbona TAA hamueleweki kuhusu uwanja huu,acheni siasa mnamwangusha mama kiaina.
Kama ni kampuni ya Rostam imepewa kandarasi mjue tumeliwa. Hakuna cha maana atafanya zaidi ya kutakwa kulipwa hela bila kazi. Nawaambia lazima ataiba. Kama mnataka kazi ifanyike vunjeni mkataba kabla hamjalipa hela nyingi kisha itafutwe kampuni ya kichina. Wazawa wako wachache ambao wanaweza kufanya kazi hiyo.
 
Back
Top Bottom