Mwakyembe ataka reli ijadiliwe

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harisson Mwakyembe amewataka wadau wa usafiri wanaojadili sera ya reli kutumia utaalamu na uzoefu walionao kupanga aina ya daraja la reli ambayo Tanzania inaweza kuwa nalo na namna itakavyonufaika.
Mwakyembe alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akifungua washa ya siku mbili ya wadau wa reli inayokutana jijini Dar es Salaam kupitia na kujadili mapendekezo ya kamati ya uandaji sera ya reli nchini itakayotumika kama muongoza wa usafiri huo hapa nchini.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Dk Mwakyembe alisema wadau hao wanapaswa kutumia utaalamu na uzoefu wao kupata aina ya reli itakayotumika nchini lakini pia kutengeneza sera itakayosaidia kurejesha hadhi ya usafiri wa reli nchini ambao kwa sasa umepoteza mvuto.

“Umuhimu wa usafiri wa reli katika kukuza uchumi katika kila Taifa duniani uko wazi, kwa hapa nchini siku za nyuma reli ilisaidia kusafirisha mizigo na pia abiria, wananchi walinufauka na gharama nafuu na pia urahisi wake,lakini baada ya ubinafisishaji wa reli ya kati na pia Tazara usafirishaji wa watu na mizigo umekuwa na changamato kubwa,” alisema Mkwakyembe na kuongeza:

“Pamoja na ukubwa wa nchi yetu na ongezeko la watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 40 wamekosa huduma bora ya usafiri wa mizogo na abiri hali hiyo imewakosehsa huduma bora za kiuchumi ambazo ni muhimu kw amaendeleo yao na Taifa kwa ujumla,” alisema.

Alisema nchi imewekeza kwenye barabara ambazo ni gharama kwa kusafirisha mizigo na hata kuzihudumia na wakati huo huo ni rahisi kuharibika na kuliingizia hasara ya matengenezo ya mara kwa mara.

“Kwa sasa Tanzania inashindwa kunufaika na fursa ya kibiashara iliyopo baina ya nchi sita jirani ambazo hazijapakana na bahari za Uganda, Burundi, Rwanda, Malawi Zambia na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo kutokana na kukosekana na usafiri wa reli kutopewa kipaumbele, ninafikiri Tanzania kutokana na hali nzuri nya kijografia inaweza kunuafaika na aina hiyo ya usafiri.”alisema Dk Mwakyembe.

CHANZO:
http://moses-ayoub.blogspot.com/
 
Sijataka kumaliza kusoma thread yako,ila naona hapa kuna viini macho!Watu wameua reli malori yao yapate kazi mpaka wameongeza foleni mjini hapa hasa mida yajioni,mandela rd,kimara morogoro rd kisa magali yao yapate kazi!Wanaharibu miundo mbinu yabarabara kwakuzidisha uzito!Nakwambia hamna haja yakujadili aina yareli tujadili ni namna gani reli yetu yakati iliyolelewa nakizazi kisichochimba dhahabu ikawa nzuri muda wote huo leo mashimo kila mahali kanda yaziwa reli wameua,nasasa wanahamia Tazara!WALAANIWE WAO NAKIZAZI KITACHOLELEWA KWALAWAMA TOKA KWAWATANZANIA.
 
Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amesma sekta ya usafiri wa reli nchini inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo gharama kubwa za uendeshaji, kutoaminika, huduma duni, sheria, sera na mifumo ya udhibiti kutokana na kutokuwepo na uwekezaji wa kutosha usiokuwa na ushindani.

Dk. Mwakyembe alisema hayo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa watalaamu wa sekta ya usafiri wa reli uliokuwa ukijadili rasmu ya sera ya reli nchini ambao ulifanyika jana jijini Dar es Salaam.

Dk. Mwakyembe alisema ili kurejesha sekta ya reli kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, serikali imeamua kuandaa sera ya reli itakayojitegemea badala ya hivi sasa ambapo ipo sera ya uchukuzi ambayo ni pana na inajumuisha mambo mengi.

Alisema miongoni mwa mambo ambayo yanatakiwa kuangaliwa na wataalam hao ni kuona kama Tanzania tuwe na reli ya upana upi, kwani iliyopo ina upana wa mita moja.

Aliongeza kuwa baadhi ya wadau wanaona kwamba upana wa mita moja ni kama umepitwa na wakati japo zipo nchi kama Japana na nchi nyingine barani Afrika zinazotumia reli yenye upana huo.

Dk. Mwakyembe alisema hata kwa nchi za Afrika Mashariki zinahitaji kuwa na mfumo wa reli zenye upana mmoja ambazo ni mita 1.435 ambayo inatumiwa na nchi nyingi duniani.

Alisema kwa nchi kubwa kama Tanzania yenye idadi ya takribani watu milioni 40 kunahitaji kuwa na usafiri wa reli wa uhakika ambao ni muhimu kwa maendeleo ya nchi.

Alisema katika kuhakikisha sekta ya usafiri wa reli inaboreshwa, serikali ipo katika mchakato wa kununua vichwa 13 vya treni na vingine 18 vya kukodishwa.

Hata hivyo, Dk. Mwakyembe alisema kukodisha vichwa vya treni imekuwa ghali sana hivyo serikali inalenga kufufua vichwa vibovu vilivyopo nchini kwa kuhakikisha mafundi wanafanya kazi hiyo usiku.

Mwenyekiti wa kamati iliyopewa jukumu la kutayarisha rasmu ya kutengeneza sera ya reli, Dk. Malima Bundara, alisema wakati wa kutembelea mikoa mbalimbali walibaini hali ya usafiri wa reli ni mbaya na miundombinu yake imechakaa sana.

Dk. Bundara alisema changamoto nyingine walizobaini ni kuvamiwa kwa njia za reli na uwekezaji hivyo kuna haja ya kuwa na miongozo kama serikali katika kuboresha usafiri huo.




CHANZO: NIPASHE

 
Back
Top Bottom