Mwakyembe anavyomlinda Kijazi wa TMAZ

Sep 30, 2012
21
0
Mpaka sasa wafanyakazi wake hawajalipwa na Yeye kila mwezi ni lazima atumie pesa za Taasisi kwenda Ulaya. Wafanyakazi wamelalamika hadi kwa Waziri lakini Waziri kauchuna tu. Mtindo wa kulindwa na Waziri kunaifanya Mamlaka ya Hali ya Hewa kuwa wakiwa na ndiyo maana kuna wkt kazi za utabiri zinafanyika ktk hali duni na kuleta matokeo mabaya kwa sababu ya watendaji bogus kulindwa na wanasiasa
 
Avanti

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,209
1,195

Ninachojua ni Kweli hiyo Mama hupaa sana kuliko hata Mkuu wa kaya, ila kutojali wafanyakazi wake hilo sijui
 
Tanzania Mpya

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
248
225
Kabla hujaandika uwe na uhakika na unachokisema, na hasa pale unapotaka kumtuhumu mtu. Je, una uhakika kwamba wafanyakazi wa TMA wanalipwa kutokana na pesa zao wenyewe ambazo huyu mama anazitumia kusafiri? Na kama wanalipwa na Serikali, basi huu unaoleta hapa ni umbea na uongo. Nachojua mimi, wafanyakazi wa TMA wanalipwa na Serikali. Sasa ulitaka Waziri afanye nini? Ajibu upuuzi usiokuwa na ukweli wowote? Waziri Mwakyembe anaelewa ukweli ndio maana kakaa kimya.

Acha majungu, kama huna cha kuongea basi kaa kimya.
 
Du! Mbona mashambulizi hivyo. Hautaki ukweli usemwe ama vipi? Labda nawe ni mnufaika wa Dg wenu nini?
 
Sep 30, 2012
21
0
Kabla hujaandika uwe na uhakika na unachokisema, na hasa pale unapotaka kumtuhumu mtu. Je, una uhakika kwamba wafanyakazi wa TMA wanalipwa kutokana na pesa zao wenyewe ambazo huyu mama anazitumia kusafiri? Na kama wanalipwa na Serikali, basi huu unaoleta hapa ni umbea na uongo. Nachojua mimi, wafanyakazi wa TMA wanalipwa na Serikali. Sasa ulitaka Waziri afanye nini? Ajibu upuuzi usiokuwa na ukweli wowote? Waziri Mwakyembe anaelewa ukweli ndio maana kakaa kimya.

Acha majungu, kama huna cha kuongea basi kaa kimya.
We uliyejibu hapa najua ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala ambaye mnalipana kinyemela na kuwaacha wafanyakazi wa chini wakinyanyasika. Jitambue acha unyonyaji!
 
Tanzania Mpya

JF-Expert Member
Apr 11, 2012
248
225
Watanzania tuna tatizo moja kubwa. Mtu akiwa na mawazo tofauti tu basi ni adui, au yupo na huyo anayesemwa. Hapa tunaongelea hoja iliyoletwa na sio nani anasemwa. Au mnataka kila mmoja aunge mkono hata kama hoja haina mashiko?

Mleta hoja hoja amechanganya mambo ya mishahara na safari. Tufanye uchunguzi tuone taasisi ngapi za Serikali zinajilipa mishahara zenyewe, ni chache. Tatizo lingine ni kwamba, mimi Nina inamani kubwa na taasisi zinazoongozwa na wanawake kwamba zinakuwa na matumizi mazuri ya fedha, au kwa maneno mengine, viongozi wengi wa kike sio mafisadi kama viongozi wengi wa kiume. Kwa hiyo kabla hujamtuhumu kiongozi mwanamke kwa matumizi mabaya ya kifedha, tafiti kwanza.

Mfumo dume huwa hautaki kuongozwa na wanawake, ndio huu unaokimbilia kuwachafua bila kufanya uchunguzi kwanza.

Tuwavumilie wengine wanaokuja na hoja zenye msimamo kinyume na zile zinazokusudiwa kuvumishwa humu ndani.
 
Nambarione

Member
Sep 3, 2013
62
125

Naona ndugu yangu wamekushika patamu, maana unajitetea sana. Hata Petro alipoulizwa na yule mwanamke wakati Yesu amekamatwa na wayahudi kuwa ni mmoja wao, alikana mara 3. Habari ya mfumo dume inatoka wapi hapa? Mtu amehoji kuwa TMA iko hoi kifedha, na sababu kubwa ni safari za DG. Unatakiwa ujibu hoja hiyo, Je, TMA haipo hoi kifedha? na je, DG hasafiri sana nje ya nchi? Ufanisi wa taasisi ya umma sio watumishi kulipwa mishahara pekee, bali kuwepo kwa fedha za uendeshaji. Mtoa mada nadhani alilenga huko. Mimi nachukia sana watu ambao wanatumia muda wao kutetea uovu. Mtu anapoleta mada inayokemea uovu unaofanywa na viongozi wetu, tafadhali tusiikandia bila hoja za msingi. Tutaendelea kuua nchi hii. Namjua Mwakyembe ni Waziri makini, atalichukua hili na kulifanyia kazi.
 
Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,100
1,195
We uliyejibu hapa najua ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala ambaye mnalipana kinyemela na kuwaacha wafanyakazi wa chini wakinyanyasika. Jitambue acha unyonyaji!

Na wewe unayelalamika utakuwa mlinzi au secretary! Umeshaambiwa Serikali ndio inalipa mishahara ya Mamlaka bado unalalamika. Umewahi kuona secretary au mlinzi wanasafiri kikazi???

Au unaajira ya mkataba hapo au uko field sasa umeona wakubwa wanafaidi roho inakuuma. Kasome bwana mdogo. Kuna tofauti kubwa sana kati ya Doctor na Nesi.
 
Issue sio kwamba mfanyakazi wa chini analipwa mshahara mdogo, lah! ni kucheleweshewa mshahara. Mbona Taasisi zingine za Serikali hata mishahara ikichelewa wanatumia fedha zao ambazo mishahara ikitoka hurudishwa. Iweje huyu mama yeye fedha zinazokuwepo atumie yeye tu kwa safari badala ya kuwalipa wafanyakazi. Hata hivyo kusafiri kwake unakujua wewe? Hamna uhalali wowote, kila mwezi mtu anaenda Geneva, si ni bora ijulikane ofisi yake ipo huko!
 
JICHO TAI

JF-Expert Member
May 27, 2013
1,110
2,000
We uliyejibu hapa najua ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala ambaye mnalipana kinyemela na kuwaacha wafanyakazi wa chini wakinyanyasika. Jitambue acha unyonyaji!

inawezekana watu huwa wanasikia raha kuropoka tu! hii ni taasisi ya serikali na nijuavyo mimi mishahara ya wfanyakazi inatokea hazina tena inaingia moja kwa moja kwenye account ya mamlaka na pesa ndo zinaenda bank mbalimbali kwenye accounts za wafanyakazi kutokana na payroll ambayo TMA wameshaandaa. sasa DF anajilipa vipi na CEO?
 
Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,955
2,000
Watanzania tuna tatizo moja kubwa. Mtu akiwa na mawazo tofauti tu basi ni adui, au yupo na huyo anayesemwa. Hapa tunaongelea hoja iliyoletwa na sio nani anasemwa. Au mnataka kila mmoja aunge mkono hata kama hoja haina mashiko?

Mleta hoja hoja amechanganya mambo ya mishahara na safari. Tufanye uchunguzi tuone taasisi ngapi za Serikali zinajilipa mishahara zenyewe, ni chache. Tatizo lingine ni kwamba, mimi Nina inamani kubwa na taasisi zinazoongozwa na wanawake kwamba zinakuwa na matumizi mazuri ya fedha, au kwa maneno mengine, viongozi wengi wa kike sio mafisadi kama viongozi wengi wa kiume. Kwa hiyo kabla hujamtuhumu kiongozi mwanamke kwa matumizi mabaya ya kifedha, tafiti kwanza.

Mfumo dume huwa hautaki kuongozwa na wanawake, ndio huu unaokimbilia kuwachafua bila kufanya uchunguzi kwanza.

Tuwavumilie wengine wanaokuja na hoja zenye msimamo kinyume na zile zinazokusudiwa kuvumishwa humu ndani.

Mtoa hoja yupo sahihi. Usichokijua wewe ni kuwa wanawake si mafisadi.Hapo sasa unahitaji kufanya tafiti mpya.Kijazi ni fisadi.Wafanyakazi hadi leo hawajalipwa mishahara yao.Mbaya zaidi hataki kuulizwa swali na wafanyakazi.Yeye kila kukicha ni safari za Ulaya na Afrika Kusini.Ni fisadi aliyepitiliza.
 
Jun 11, 2008
53
95
Nijuavyo mimi, safari za viongozi nje ya nchi lazima ziwe na kibali cha Waziri wa Wizara husika na Ikulu. Hivyo ni vigumu huyo mama kufanya safari za hovyo hovyo zisizokuwa na tija kama unavyotaka kutuamisha huku mamlaka husika zikiwa kimya. Hata akina kapuku kama mimi ilibidi nipate vibali hivyo nilivyosafiri nje ya nchi!
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
40,878
2,000
Mtoa hoja yupo sahihi. Usichokijua wewe ni kuwa wanawake si mafisadi.Hapo sasa unahitaji kufanya tafiti mpya.Kijazi ni fisadi.Wafanyakazi hadi leo hawajalipwa mishahara yao.Mbaya zaidi hataki kuulizwa swali na wafanyakazi.Yeye kila kukicha ni safari za Ulaya na Afrika Kusini.Ni fisadi aliyepitiliza.

Mkuu nimevutiwa sana na hizi quaotation zako.Nilikuwa sijawahi kuzisikia wala kuzisoma mahali popote.Hakika ni maneno ya busara sana kwa maisha ya kila siku ya mwanadamu.

"An empty stomach is not a good adviser" na hii "poverty is the parent of revolutio and cime".Sana sana nimeipenda hiyo ya kwanza ya empty stomach ya the great Albert Eisnten.
 
Mundu

JF-Expert Member
Sep 26, 2008
2,708
2,000
Wezi wa fedha za uma ni mafisadi tu...wasemeni hata kama watatokea vifuu tundu wa kuwatetea humu....
 
Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
8,552
2,000
Kabla hujaandika uwe na uhakika na unachokisema, na hasa pale unapotaka kumtuhumu mtu. Je, una uhakika kwamba wafanyakazi wa TMA wanalipwa kutokana na pesa zao wenyewe ambazo huyu mama anazitumia kusafiri? Na kama wanalipwa na Serikali, basi huu unaoleta hapa ni umbea na uongo. Nachojua mimi, wafanyakazi wa TMA wanalipwa na Serikali. Sasa ulitaka Waziri afanye nini? Ajibu upuuzi usiokuwa na ukweli wowote? Waziri Mwakyembe anaelewa ukweli ndio maana kakaa kimya.

Acha majungu, kama huna cha kuongea basi kaa kimya.

Well said mkuu, kwani TMA ina mradi gani wa kujihingizia PESA!! Na kwa kuwa ni Mwanamke basi watamzulia mambo chungu MZIMA, kuna baadhi ya Watanzania na akili zao timamu huwa hawapendi kabisa kufanya kazi chini ya akina MAMA.
 
Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,726
1,500
yaelekea wewe unajua zaidi kinachoendelea. hebu tulia na utupe habari juu ya huyu kijazi kusafiri kwenda ulaya kila kukicha kwa kutumia kodi na rasilimalizetu ambazo anatakiwa azilinde kama mtu aliyepewa dhamana,

Kabla hujaandika uwe na uhakika na unachokisema, na hasa pale unapotaka kumtuhumu mtu. Je, una uhakika kwamba wafanyakazi wa TMA wanalipwa kutokana na pesa zao wenyewe ambazo huyu mama anazitumia kusafiri? Na kama wanalipwa na Serikali, basi huu unaoleta hapa ni umbea na uongo. Nachojua mimi, wafanyakazi wa TMA wanalipwa na Serikali. Sasa ulitaka Waziri afanye nini? Ajibu upuuzi usiokuwa na ukweli wowote? Waziri Mwakyembe anaelewa ukweli ndio maana kakaa kimya.

Acha majungu, kama huna cha kuongea basi kaa kimya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom