NusuMutu
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 421
- 87
Namsifu ndugu Mwakyembe,maneno aliyosema ni machache lakini yenye busara ya kiMungu. Binafsi nakuombea afya njema na ulinzi wa Milki ya Mbinguni uwe pamoja nawe. Mnao dhihaki afya na pengine sura yake nawapa pole..., hujafa hujaumbika! Thamani yetu haipo kwenye sura,ipo ktk pumzi ya zawadi ya uhai anayotupa Mwenyezi na matendo yetu ya kiadilifu kwa binadamu wenzetu. Kama mnalipwa na mafisadi ili kumdhihaki nawapa pole tena!