Huyo mstaafu alikua anatafuta nini ofisini mpaka leo,Hapa Kamani anaweza kuona anamkomoa Mwakyembe kumbe anaonyesha udhaifu wake.
sioni chochote ulichoandika hapa zaidi ya u.h.a.r.o tuni shida sana kumpa
mnyakyusa madaraka ....yani mwakyembe yeye ni full kukurupuka ....siju
hata u DR alipataje?
Hata Kama Kweli Mwakyembe kakosea ..KULIKUWA na haja gani ya waziri Kamani kuongea HADHARANI bila kuongea wenyewe kwa Siri ....hata Kama kakosea bado Waziri Mwakyembe anabaki na haki ya kuchukua hatua kwa kuwa wafanyakazi husika ...wamekuwa posted uwanja wa ndege na kuna AGIZO la Rais la kusafisha vitendo Vya RUSHWA ,aibu ,Madawa ya kulevya pale uwanjani ..Sasa Kama waziri anataka kuendelea kuwatumia wafanyakazi wake wa wizara ya Kilimo walioko pale ...Njia rahisi angewapangia tu sehemu nyingine mbali na uwanja wa ndege au Bandarini
Huko ndiko kunaitwa kukurupuka. Lakini pia sina uhakika taratibu za kazi serikalini zinasemaje kama Waziri anaweza kumfukuza kazi mfanyakazi yeyote wa serkali hata kama hayuko kwenye wizara yake!!!!! Nafikiri kwa kuweka mambo sawa Mwakyembe angetangaza kuwafukuza hao wafanyakazi kutoka kwenye nafasi zao ndani ya airport ili warudi kwenye wizara zao na huko angemshauri waziri mwenzake kuwafukuza kazi. Lakini sio yeye kuwafukuza kazi.
Tiba
Duh! huku sasa kuumbuana.kwa nini waziri kamani asimtafute kwanzan Dr. Mwakyembe ili waweke sawa records zao kabla ya kuruka hewani?
Hawa mawaziri wa jk yani ni vichekesho tu
Sasa mtu kama mwakiembe ni mtu wa kukurupuka bila sababu sasa ona kamfukuza mstaafu kazi
Inamaana anafanya vitu bila tafiti za maana aibu!
waziri titus kamani amesema mmoja wa watu waliotangazwa na mwakyembe juwa wamefukuzwa aiport jana alishastaafu tangu 2013 na sio mfanyakazi wa serikali tangu wakati huo.
Waziri kamani amesema ameshangazwa kuona mstaafu anatangazwa kuwa alikuwa mfanyakazi wa wizara yake kama alivyotangaza mwakyembe jana.
Hata hivyo waziri kamani amesema anasubiri taarifa zaidi toka kwa dr mwakyembe kuhusu hatua alizotangaza jana kufukuza wafanyakazi wa wizara yake waliokuwa wakifanya kazi jknia.
Source:radio one habari
ni shida sana kumpa mnyakyusa madaraka ....yani mwakyembe yeye ni full kukurupuka ....siju hata u dr alipataje?
Mkuu hii inaonyesha jinsi ambavyo si makini na anafanya kazi k8majungu majungu tuNi dhahiri kabisa kuchomekwa kwa jina la mstaafu ni njama za mafisadi kutaka kudhohofisha jitihada za Mwakyembe. Hupaswi kulalamika wakati mwenzako anajaribu kufanya kitu kusaidia hali mbaya iliyotawala kwenye ule uwanja. Unapaswa kulaani watu wanaotaka kumuhujumu!
MkuuUkisema hajafanya lolote unakosea, je wajua mapato ya tra bandarini baada ya mwakyembe kuichukua bandari yamepanda kwa kiasi gani? Usiendeshwe na hisia zaidi kuliko uhalisia. Isiwe tu ilimradi mtu atukanwe na kuchafuliwa, hajafikia kufanya vizur sana ila ktk wizara yake anajitahidi na kila mtu analiona. Akifanya vema tumpe pongez na akikosea pia sio tu kila kitu kiwe negative tu. Ina maaana hamuoni rushwa ilivyoshamir uwanja wa ndege? Sasa jamaa anathubutu nyie mnamponda? Sijui mna maana gani?