Mwakyembe aibua ufisadi Kivukoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe aibua ufisadi Kivukoni

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by TIMING, Jan 8, 2011.

 1. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amegeuka mbogo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza eneo la Kivukoni jijini Dar es Salaam na kuelezwa asilimia kubwa ya mapato yanayopatikana yanatumika kuendesha kivuko hicho.

  Dk. Mwakyembe aligeuka mbogo baada ya Mkuu wa Kivuko cha Kigamboni, Mhandisi John Gama, kueleza kwamba mapato ya kivuko hicho kwa mwezi ni Sh 221,173,230 wakati matumizi ni wastani wa Sh. 223,314,481 kwa kipindi hicho.

  Gama alieleza pia kwamba gharama kubwa ni ununuzi wa mafuta ambayo ni Sh. Milioni 102 kwa mwezi.

  Taarifa hiyo ilimfanya Naibu Waziri huyo kuonyesha kutoridhishwa na hali ya mapato na matumizi na kueleza kwamba idadi ya watu na magari ambayo yanatumia vivuko kila siku hailingani
  SOURCE: NIPASHE  Ushauri kwako Harry...

  anza na temesa leadership... wanalea ana hao suprvisors, umeondoka huku watu wanamega kisela:tape:
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hivi huyu jamaa bado mpambanaji au baada ya kupata ulaji kafungwa mdomo maana sija msikia akisema lolote juu ya DOWANS/RICHMOND...
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Dah wabongo kwa dili siwawezi ndo maana wanafumuka kweli kweli miili yao.

  Wakijenga daraja pale familia nyingi zitateteleka kwa mpango huu.
   
 4. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2011
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Achunge sana anelewa nini kipo nyuma yake ,wale wanao muwinda ameahidi mara hii hawatafanya makosa waliyo yafanya mara ya mwisho
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mkuu hilo daraja huwezi amini, linapigwa vita hadi na watendaji wengine wa wizara... very sad tunaangalia sana matumbo
   
 6. M

  Mp Kalix2 JF-Expert Member

  #6
  Jan 8, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 5,240
  Likes Received: 1,163
  Trophy Points: 280
   
 7. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2011
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kivuko kile serikali imekuwa inakifanyia mzaha sana miaka yote wakati ni muhimu sana kwa wananchi na kipato cha serikali na ajira.
  Kwanza hakina tena uwezo wa kuhudumia ipasavyo. Kimezidiwa na watu na magari. Nafasi ya watembea kwa miguu haitoshi kabisa na inaonyesha inaweeza tokea ajali mbya pale magogoni, Mungu aepushilie mbali. Lakini serikali inatakiwa ichukue hatua za haraka kukiboresha. Kwa mtazamo wangu ingetakiwa kwa sasa kuwe na vivuko vinne, mbili zinashusha upande mmoja na mbili upande wa pili.
  Ukusanyaji mapato ni mbovu sana sana. Zinatakiwa computerized tickets. Kuna wakati ticket zinabadilika badilika rangi tu pale, sasa hatujui kama kuna walichapisha zao au vipi.
  Kwa hesabu za haraka haraka ni lazima waweze kuingiza zaidi ya Tshs. 250 mln. kwa mwezi. Tatizo kubwa ni lazima litakuwa kwenye mafuta na vipuri na huenda wafanyakazi hewa. Zaidi ya hapo mipango au taratibu ni mbovu kabisa. Kivuko kinapoteza muda mwingi sana ku- "off-load na ku- load". Kwa sababu magari yanatanguliwa na abiria wa miguu kutoka, na hawaelekezwi vizuri kupita upande wa abiria wa miguu na matokeo yake badala ya kivuko kupakua kwa dakika kama nne ~tano tu huchukua hadi dakika 15 na kupakia dakika 20 matokeo yake hata trip tatu kwa saa hazifikii. Na wakkati huo engine zinafyonza mafuta na kuongeza joto la dunia plus pollution.
  Hadi hapo Tanzania itakapoacha kuchagua viongozi vihiyo kwa sababu zao za kisiasa kwenye hizi fani muhimu pamoja na wanasiasa wasio na vision wananchi tutapata shida sana.
  Wakati mwingine serikali yetu huonekana kama inafanya haya mambo kwa makusudi kabisa. Kungoja mpaka mambo yawe mabaya kabisa ili waanze kuwatafuta wale wale wafanya biashara wao mashuhuri na kuwataka wafanye mambo kwa haraka haraka ili kuepuka sheria zote za mannunuzi "procurement procedures" ili Bwana Patel aendelee kuchangia chama. Na ni hao hao wanaofanya mizengwe ili daraja lisijengwe.
  Aibu gani hii baada ya miaka 50 ya uhuru?
   
 8. K

  Kishalu JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 850
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  kwa mtindo huu ndiyo maana daraja haliwezi kujengwa maana ni mradi wa watu wanajipatia mihela ya kutosha kabisa na kutanulia wanavyopenda; na imekuwa ni kawaida kwa mawaziri kupata ripoti kisha wanawaka na baadaye inakuwa kimya yaani waziri amewaka na hamna kinachoendelea tofauti na kuendelea na kukusanya hela kutoka kwa raia ambao hawana

  Mwisho vipuri vinaisha kabisa wanarudi kwenye kodi zetu

  Amani haipatikana bure wanajf
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu, the fact ni kwamba hiyo pesa inapanda ngazi, kuanzia wakata kiteki hadi wakubwa... naskia kuna very powerful network

  kama mwakyembe yupo sirias inabidi aangile uwezekano wa system overhaul au kupendekeza kigamboni development agency ambayo mbali na infrastructure, pia iangalie mipango yote ya maendeleo

  kuna uswahili sana kwa sasa

  na hao wafanyakazi wa chini ni miungu watu mkuu... viburi kupita kiasi kwani majority wameletwa na watu wao
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  thansk mkuu kwa uchanganuo... ukweli ni kwamba wanahitaji zaidi ya presentation kufanya maamuzi, naona amekomalia injini moja/mbili kuwashwa lakini issue pale ni zaidi ya hiyo..waangalie pia ni watu wangapi wanavuka kila siku
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Jan 8, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  very true... kweli wewe ni mdau wa kigamboni... umeweka vyema sana hali halisi... apart from administration and finance, tatizo kubwa ni logistics management

  Kuhusu procurement, we love emergency procurement... coz there we can dance around

  Mpaka leo sijasikia kama daraja linajengwa au la, ingawa kuna mjuaji mmoja alisema linaanza february mwaka huu

  what i see now ni kwamba the government has either lost it or totally ignored all rosy plans for kigamboni
   
 12. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2011
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Watakula wapi si kama miradi kama hii isiyokuwa na usimamizi angalifu?
   
 13. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #13
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Kwakweli wajenge daraja maana wengine tukiwa tunavushwa sala zote tunamalizia pale kwa uoga.
   
 14. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #14
  Jan 9, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mwakyembe bado hajajuwa kazi yake,muda wa kuibua ufisadi ni wakati alipo kuwa mbunge sasa hivi yuko serikalini ni naibu waziri anatakiwa KUUKOMESHA! Anatakiwa kuwatuma watu wafanye uchunguzi na hatua kuchukuliwa wakati wa kulalamika umeisha,kapewa rungu alitumie.
   
 15. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  sina ushahidi lakini nahisi wanaiba sana hapo kivukoni na mgao unaanza kwa incharge wa hapo hadi wakata tiketi, hivyo kumaliza tatizo ni lazima kuweka utaratibu mpya wa tiketi ambazo ni computerized na kuweka watu wapya ama sivyo kila siku computer zitakuwa mbovu au system down ili waendeleze wizi
   
 16. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Mmmh,
  Habari ya daraja la Kigamboni, sina kumbukumbu hivi iko kwenye Ahadi za JK?? Saa hizi mambo yote ni kujenga fly-overs. By the way kuhamia Dodoma ni aje?? Wenzetu wa Nigeria na Malawi nasikia walikuja kujifunza kwetu na wamefanikiwa sie mmmh!! Solution ni kuhamia Dodoma Tu, kama haiwezekani serikali ya JK itutangazie rasmi. naona nguvu inaelekezwa kukarabati na kujenga majengo mapya ya wizara na taasisi za serikali, kama mpango upo kwa nini taasisi za serikali zisijenge Dodoma??? Akili kwa kichwa....:flypig:
   
 17. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #17
  Jan 9, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ningefurahi sana kama wangeweka barabara na wanashindwa kuiweka kwa sababu ya ufisadi wao tu ili waendelee kula maana wakiweka huu upuuzi unaisha na kigamboni pataendelea kwa haraka zaidi..
   
 18. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #18
  Jan 10, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  [BADO TIKETI HEWA
   
 19. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #19
  Jan 10, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Mwakyembe, nakuomba usiishie kuibua ufisadi!! chukua HATUA za maana!!!
   
Loading...